Tuanze kubadilika sisi wana JF, ndondo sio chururu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuanze kubadilika sisi wana JF, ndondo sio chururu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nteko Vano, Jun 3, 2012.

 1. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF
  Tumekuwa mstari wa mbele kukemea matendo ya kifisadi ambayo watumishi wa serikali wamekuwa wakiyafanya hususan yale makubwa ambayo yametambuliwa kama vile EPA, Richmond, ubadhirifu wa fedha kulingana na ripoti ya CAG na mengineyo mengi.

  Ukiangalia kwa haraka haraka wahusika ni watendaji wa serikali, sekta binafsi, wafanyabiashara na taasis mbalimbali. Humu JF kuna watu wa aina mbalimbali wanasiasa, wafanyakazi wa serikalini na sekta binafsi, wafanyabiashara, wanafunzi, wakulima n.k.

  Nimejiuliza sana hivi wewe na mimi ambao ni maafisa wadogo serikalini kusubiri ile funga mwaka na kuchakachua fedha hata wakati mwingine kujifanya unasafiri lakini huendi safari wakati umechukua hela ya ofisi au kuandaa mikutano hewa ukipata mwanya wakuwa mkubwa si utakuwa balaaa wewe unaweza ukawa kama Chenge, Balali, Maige, mkurugenzi wa TBS na wengineo tunaowafahamu! Nawe mfanyabiashara mwenzangu ambaye sasa hivi tunafanya juu chini kuwalangua wananchi kitu sh 3 tunataka kuuza kwa sh 9 yaani faida mara 2, sukari, mafuta ya taa na bidhaa nyingine tunaficha sasa hivi ili tuje kulangua kipindi chake, tuna misheni town nyingi hata kuleta vitu bandia hivi ukipata nafasi ya kuwa kama Rostam, Manji na wale wengineo walioshiriki kwenye EPA na richmond si tutakuja kuangamiza! Tusijisahau wale wa benk wenzangu tunaodokoa sh 200 kwenye akaunti za watu tukipelekwa BOT si tutakuwa kama akina Balali na Lyumba! Wale wa sekta binafsi tunaokula hela za NGOs ambazo wahisani hutoa na mengineyo mengi ambayo wewe uliopo huko unajua unavyofanya. Na sisi wale ambao hatujaorodheshwa hapa lakini tunajijua jinsi tunavyopigania mkate wetu kwa njia ya mkato ambayo unaona kabisa kama tukipewa chaka tunaweza tukawa kama akina maige, lowasa, rostam nk tujitambue.

  Basi hayo makundi yote kama tunaingia humo na wale ambao sikutaja tujipime na tubadilike ili isije siku mbeleni tukanyoonyewa sisi vidole. Kama tunahitaji ukombozi wa kweli tubadilike wadau naamini kwa njia moja au nyingine tunashiriki hata kama ni kwa kiasi kidogo ila ipo siku itakuwa kwa kiasi kikubwa kama hatutabadilika.
   
Loading...