Tuangalie Tanzania tunapata nini Kenya ukiondoa kujipendekeza na wao wanapata nini kwetu?

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,398
8,883
Ukiangalia mambo simple sana mfano tu mdogo kwamba sisi tunajipendekeza zaidi, Dar kuna Barabara ya Kenyata, inaitwa Kenyata drive ni kwa wadosi huko ni moja kati ya barabara bora muhimu kabisa Dar wakati Nairobi mtaa wa Nyerere haufiki hata km 2 na ukimuuliza Mnairobi wa kawaida wapi Mtaa wa Nyerere ulipo haujui, wakati Dar karibia kila mwana Dar anajua Kenyata drive.

Haya akaja Kikwete akafuta barabara ya kihistoria inayotoka Ikulu kupita Baharini akaita Barack Obama kumbuka Kenya kwenyewe sijui kama kuna Mtaa maarufu wa Barack Obama ile barabara mpya ya Kawe ambayo ni posh area inakwenda kilometa kibao Kikwete kaita Mwai Kibaki ukiuliza Mwai Kibaki kaifanyia Tanzania kustahili heshima kama hiyo sioni wakati sijaona Mtaa wa Kikwete au Kikwete road Nairobi, tena Kikwete hata alienda kuwasuluhisha walivyopigana vita lkn mbona hakuna kumbukumbu yake popote Kenya? Kibaki kaifanyia Tanzania unaweza kuniambia?

Hayo ni mambo machache tu ambayo yanaonekana kwamba hatuna uhusiano bali tuna kujipendekeza, hakuna Mwanasiasa wa Kenya ambaye atakuwa na matatizo na Serikali ya Kenya akakimbilia Tanzania lkn kinyume chake ni kawaida, Samia alienda Kenya no body cared, Uhuru Kenyata kuja Dar utafikiri yeye ndiyo Raisi wa Tanzania yupo kila mahali media zote, hata hapa JF ni yeye tu.

Raisi wetu kutwa kuomba msamaha kwa Kenya lkn sijawahi kusikia Raisi wa Kenya akiomba msamaha popote kwa Tanzania pamoja na kwamba wametufanyia ushenzi mwingi tu, Watanzania walifurumushwa na kufukuzwa kutoka Nairobi mbona Uhuru hajaomba msamaha kwetu?
 
Walalamikaji ni kundi moja la watu wapumbavu sana.

IMG_20211203_111536.jpg
 
Mpumbavu ni yule anayeingia kwenye mahusiano kama loser halafu anajisifu!
Juha ni yule anaeishi kwa kujishuku shuku muda wote na kutokujiamini kwa vitu ambavyo hata havijui.

Wewe subiri Chaggadomo watangaze maandamano au Diamond atoke Kwa Zari South ukamookee Airport.

Huna akili.


Tena sasa hivi usiposhtuka utajikuta umebaki peke yako.

Watu wanapiga kazi na kudaka fursa. Wewe endelea kupanua mdomo mitandaoni Mboweeee mboweee mboweee
 
Mpumbavu ni yule anayeingia kwenye mahusiano kama loser halafu anajisifu!
Sasa mahusiano ya kimapenzi ndio unataka kuyalinganisha na ya kiuchumi?!!wewe vipi, yaani hadi leo hujui kenya wana mchango kiasi gani kwenye uchumi wetu?!!nchi inayokuzidi uchumi hasa inapokuwa jirani yako ni faida sana kwako kujipendekeza kwake kuliko yeye, mbona mnaing'angania burundi?zile sera za marehemu za kumuona kila aliyekuzidi ni adui yako, zilishapitwa na wakati huko.
 
Sasa mahusiano ya kimapenzi ndio unataka kuyalinganisha na ya kiuchumi?!!wewe vipi, yaani hadi leo hujui kenya wana mchango kiasi gani kwenye uchumi wetu?!!nchi inayokuzidi uchumi hasa inapokuwa jirani yako ni faida sana kwako kujipendekeza kwake kuliko yeye, mbona mnaing'angania burundi?zile sera za marehemu za kumuona kila aliyekuzidi ni adui yako, zilishapitwa na wakati huko.

Ni wapi nimetaja neno mapenzi ?
 
Back
Top Bottom