Tetesi: Tuangalie na Hili.

Don san tan

JF-Expert Member
May 23, 2015
522
500
Jamani tafadhali sana, Msiihusishe na CCM pale matamko uchwara yanapotokea. CCM Ipo makini na Serikali yake bila kubagua ni Chama gani. Na inatenda haki kwa kila mtanzania.
Niombe tu Serikali isifuate maneno ya watu, wengine ni wapinzani wanataka Kiki ili waweze kukamata dola. Endapo tutafanya kazi kwa kufuata maneno ya watu ni dhahiri Shairi tutapotea. Kuongoza Serikali kwa kufuata kila Mwananchi anasemaje tutashindwa. Tufanye yale yanayoonekana kuwakera wananchi wote bila kujali Maeneo gani wanatokea Tamko kama hili linalosema Ndalichako "Walimu wa sanaa
wanatosha. Serikali haiwezi kuajiri
walimu wa masomo hayo kwa sasa" Lakini nimeshindwa Kuelewa kama tamko hili limetolewa kweli na Mh Waziri wa Elimu Sayansi na Technology Mh Professor Joyce Ndalichako au wale wapinzani wameamua kurukia upande wa Elimu? Na kama hili tamko limetolewa na Mh Waziri mwenye dhamana hii haipendezi wala haina mashiko kwa wananchi walio wengi katika nchi yetu. Kwani walimu walio wengi ni wa Sanaa hili naomba tu nikiri kuwa Walimu walio wengi wamesoma katika mazingira magumu sana na hao ndio wanyonge anaozungumzia Mh Rais wetu. Kama utawaminya waalimu wa Sanaa maana yake umeiminya jamii iliyo kubwa kule Kijijini. Kwa sababu walimu wengi wamesoma Shule za Kata ambazo masomo yaliyo makuu kwao ni Ya Sanaa. Hii ilotokea kwa sababu ya ukosefu wa waalimu wa Sayansi na vitendea kazi pamoja na maabara kwa mafunzo ya Sayansi.
Naiomba Serikali iangalie upya katika Suala la kuwaajiri walimu hao wa Sanaa. Mh Professor Joyce Ndalichako angalia wapi na maeneo gani yanahitaji sana walimu wa Sayansi na maeneo gani yanahitaji walimu wa Sanaa ili tujaze nafasi hizo bila kujali.
Unapotoa Ajira unazisaidia family nyingi intems of their life. Naomba kama kauli hii imetolewa na Waziri husika ajaribu kuangalia upya. Maisha ya mnyonge anza na Mwalimu ambaye ana kazi ngumu na Sio kumfanya kama Chombo cha kutolea matamko yasiyo na kichwa wala miguu. Naomba Watanzania tushirikiane kupaza sauti ili Mambo ya matamko yasijitokeze. Yaani mtu anatoka tu huku bila kujaji na kusema "Tangu sasa hakuna Ajira" hapo wewe mwenyewe upo Ajirani What can you imagine? unataka wenzako wafe njaa?
Labda angejitokeza kiongozi akasema "Tangu sasa tulioajiriwa miaka ya nyuma tuna ng'atuka na kuwaachia vijana" na kutekeleza mara moja huyo tungempongeza kweli kweli.
Niombe tu waalimu wa Sanaa msiwe na Shaka tutalitatua hili tatizo na mtarajie nanyi kuajiriwa kama walimu wengin. Kama kweli kauli hiyo imetolewa na Mh Waziri na chelea kusema kuwa Wanyonge wameanza kuwatenga, kwa sababu watoto wa wakubwa hakuna aliye mwalimu wengi ni Doctors, Lawyers n.k. Ajira kwa wote, mbona Miaka ya nyuma hakuna kitu kama hicho? Niliowakwaza wanisamehe 7x70.
.

HAKI SAWA KWA WANANCHI WOTE, BILA KUBAGUA AINA GANI YA ELIMU UMEIPATA.


MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom