Tuandamane kumpinga Kiongozi Anayedhurumu haki za watu kuishi

mkamanga original

JF-Expert Member
Jan 21, 2015
614
597
Marekani ni taifa kubwa duniani lililojikita katika kuamini kulinda haki za raia duniani na dunia inakuwa sehemu salama ya kuishi limeshatoa adhabu na kutuonyesha njia.

Wanaopinga waje na data, marekani ametuonyesha njia tuchukue hatua dhidi ya kiongozi aliyetajwa na wote wengine watakao tajwa huko mbeleni.

Watanzania wenye akili tulitegemea Makonda angesha jiuzuru wadhifa wake lakini kuendelea kubaki ofisini ni kiburi na dharau kwa watu anao waongoza.

Sasa ni wakati wa kuchukua hatua, marekani hajawai kumwonea mtu wala nchi yeyote watu wanaotoa mifano ya Saadam Hussein, Gaddafi na wengineo hao wote walishiriki kugandamiza haki za raia wao pamoja na kwamba walikuwa na mambo mazuri lakini hicho tu cha kuonea watu na kujifanya miungu watu ndio kiliwaponza.

Wauaji wamebainishwa na wamepigwa ban hakuna uwoga tena twendeni kwenye maandamano kifua mbele kwamba huku tukimshukuru Marekani

Kama una mawazo kama yangu weka neno kuunga jitihada hzi za kumuondoa DAB
 
Sisi wabongo bado hatujajielewa, hilo unalolisema lingekuwa ni sehemu nyingine wangeshalifanya mapema kabla hata ya Marekani kuwabainisha. Maana kitendo cha watu kuuwawa, kutekwa na kupigwa risasi bila ya uchunguzi wala ripoti zozote za kueleweka, ni dhahiri kuna uovu unafanywa kwa makusudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom