Tuandae Ziara Maalumu Ya Kuwapa Pole Wagonjwa Mahospitalini

aiseee, unafanya kitu kizuri sana Pasco, ila pole pia kwa ajali.

Mkunde asante kwa kulisema hili, mimi nilikuwa ni mtu wa mitoko sana, tukibadili viwanja kwa starehe na kuponda raha za kila aina kama vile hakuna kufa!.

Siku ya siku yakanikuta ya kunikuta, nikapata ajali mbaya, nikalazwa hospitali kwa miezi 6!. Kufuatia taarifa za awali za hali yangu, kuwa nimepata paralysis na nitakuwa confined to wheel chair!, marafiki karibu wote tuliokuwa tukistarehe pamoja, walinikimbia!, katika muda mfupi niliweza kujua kwangu nani ni rafiki wa kweli na nani rafiki wa raha!. Muhimbili walijitahidi walivyoweza, walipofikia mwisho wao, tukajaribu na kwingine na kwingine tena, hatimaye nikasimama na hatimaye kutembea!.

Ni katika kujaribu huko huku na kule, ndipo nikajigundua kumbe mimi ndio afadhali!. Kuna watu wanateseka mpaka unajiuliza hivi huyu Mungu anawaachia nini?, si awaite tuu awapumzishe!. Kwa kulizingatia hali za wenzangu, nilipata nguvu na hadi sasa, japo bado sijakamilika lakini nasimama, natembea na maisha yanakwenda!.

From then, from time to time, huwa nikipata nafasi, hupita Muhimbili, na kuwasilisana na ofisa uhusiano wa hapo na kuwaulizia wagonjwa wasio na ndugu, nawabebe chochote kitu. Na katika kuwatembea hao wagonja wasio na ndugu pamoja na kuwabebea mahitaji madogo madogo, pia huwa nakuwa "liquid" hivyo kuwapitia na wengine on my way na kuwapa "pole" wasizozitarajia!, na mwisho wa siku hujikuta niko gratified na serenity ya ajabu!.

Wanajf tukiamua!, we can do something!.
Pasco
 
kweli watu wakitulia wanaweza kuwa na ma pwointiii

wazo zuri mleta mada.
 
Back
Top Bottom