Kwisense
JF-Expert Member
- Sep 7, 2017
- 475
- 1,138
Kuna 'options' kadhaa.. Tutumie "AU" katika kutoa ushauri wetu kwa wanasiasa wa upinzani haswaa CUF na CHADEMA na NCCR-MAGEUZI kwenye mtanziko huu wa kisiasa.
"AU" YA KWANZA..
Wabunge wa upinzani ambao wapo bungeni, aidha wajiondoe katika ubunge wao, waliache bunge likiwa na upande mmoja wa CCM kwa sababu ni wazi hawataki kuona upande wa upinzani ukishamiri ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano. mtakuwa tayari kwa hili? Ngumu kidogo.
"AU" YA PILI.
Viongozi wa Taasisi hizo watangaze sasa rasmi kurejesha vuguvugu la UKUTA. hii ni Moja ya 'AU' ngumu, yenye hatari nyingi lakini yenye manufaa makubwa sana. Wataumia watu, watakufa lakini nafikiri baada ya hapo mambo yatakuwa sawa. UKUTA ni muhimu sasa kuliko hata septemba mosi ya 2016. UMOJA WA KUPAMBANA NA UDIKTETA..... Simama, tuhesabiwe.
"AU" YA TATU
Endeleeni na ubunge wenu, lakini ndani ya UKAWA na ikiwezekana na wengine wenye kuwaunga mkono, endelezeni 'harakati' za kuitaka katiba Mpya kwa machozi, jasho na damu. Katiba yenye kutambua muundo Mpya wa tume ya uchaguzi, yenye sheria Mpya ya uchaguzi na kanuni zake. Hii ni kabla ya 2019. Hii pia Kuna kupoteza UHAI na kupata majeraha. Lakini ni bora.
"AU" YA NNE.
Tuendelee kuisho kwa maigizo haya yanayoendelea sasa. Watu wenu na ninyi wenyewe mkiendelea kuteswa na kuumizwa. Mkiendelea kuishi kwa 'hofu' ndani ya nchi yenu wenyewe. Naamini, wale wachache wenye KUKEMEA ndio wapo kwenye hatari, wale wenye kunufaika na siasa hata wakiwa upande huu wa 'upinzani' wataendelea kuwa salama, maana sio 'wakosoaji'.
"AU" YA TANO.
Kuchagua kufanya siasa zenye kuwapendeza watawala. Lakini zenye kuwaondolea 'uaminifu' kwa wapiga kura. Kuchagua kuendelea na HARAKATI au kuachana na HARAKATI na kuchukua mkondo wa HARAKATI katika siasa za kidhalimu za Afrika. Siasa za Afrika pasipokuwa na HARAKATI ni uongo. Mikakati iwepo, isiachwe lakini muhimu ni HARAKATI. watawala hawapendi HARAKATI.
MMM