Tuamue leo kuwa na Taifa lenye kuongozwa na vijana ama wazee wabinafsi wasio na vision! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuamue leo kuwa na Taifa lenye kuongozwa na vijana ama wazee wabinafsi wasio na vision!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Hunter, Mar 29, 2012.

 1. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kimsingi narejea hali halisi ambayo nchi yetu imekumbana nayo toka tulipopata uhuru
  Vijana wengi wenye moyo walisahauliwa katika nafasi za kiuongozi na kimamlaka huku wakipoozwa na maneno ya vijana taifa la kesho,
  Sisi wote ni mashuhuda nafasi nyingi toka ukuu wa wilaya mpaka ukatibu mkuu wa wizara, uwaziri na ukurugenzi hata uraisi umekuwa ni maalumu kwa wazee na wastaafu wa majeshi ama wateule wachache, kundi dogo la vijana lililopata kuambulia nafasi hizo either ni lile lenye undugu na ubini na watawala or nyumba ndogo za watawala.

  Tukikumbuka matukio kama ya Bulyankulu ni wazee hawa hawa waliuza na kuruhusu wazawa kufukiwa kwenye mgodi ule.
  Pale shinyanga pamebaki mashimo na mahandaki, vumbi na mabaki ya kemikali hii nikutokana na maamuzi ama ruhusa toka kwa wazee hawa, kama mtakumbuka uncle Benny alipozawadiwa ndama wa dhahabu nini kilitokea.

  Kitalu C, na vingine vingi pale mererani vilipomilikishwa kwa wageni kipindi cha bwana Lyatonga akiwa waziri kilipelekea yote tunayoyaona Arusha leo, hakuna kazi vijana wamechoka, wamebaki kubeba mizigo ya watalii kama punda, na kuuza maziwa mjini.

  Tukubali sasa yatosha, vijana wapewe nafasi ya kufanya maamuzi na kuongoza, tumeshaona mifano ya vijana ambao wamefanya ama wanafanya mambo makubwa kwenye majimbo yao mfano Ndugu Mnyika,ndugu Filikunjombe, ndugu Kabwe, ndugu Lema, ndugu Joseph Mbilinyi, ndugu Mdee Halima.

  NB
  Wazee wetu wachache kama kina Silaa, Mbowe, Lipumba, Marando, ambao wamejitahidi kuielimisha jamii na kuwapa nafasi vijana nyie ni nguzo yetu, tutawakumbuka na historia itawaenzi
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hujafanya research ya kutosha. hao unaowaona viongozi wazee leo walianza uongozi wakiwa vijana. mfano JK, Lowasa, Lukuvi kutaja wachache. ma DC vijana ni wengi kama Nape, Shigela walianza na u DC.
   
 3. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Safi. nakupa tano kwa namna ulivyojitahidi kutokumtaja ZITTO. Umejaribu, umeweza, songambele. ila sielewi kwanini umefanya hivi. ntakufuatilia uko tuendakp.

  Kimsingi nakubaliana na wewe asilimia nyingi tu, lakini tukumbuke kuwa hata vijana wa sasa umri wao hausimami, na wazee wa leo walikuwa vijana wa jana au juzi. Namkumbuka kaka yangu ambaye kunapindi alikuwa mwanamichezo alikuwa analalamika kwamba taifa limewasahu vijana, hivi sasa ni mzee.

  Uko tunakoelekea definition ya vijana tutaipanua zaidi na ni lazima tu act. ama sivyo kuna hatari moto huu wa kutaka vijana kuchukua nchi kuwa ni propaganda ambazo hazijawahi kukoma tangu mwanzo wa dunia hii na hazijawahi kumaterialize.
   
 4. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nchimbi, Magesa Mulongo, Seif Khatib ni mifano ya walioanza uongozi wakiwa vijana.
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Walikuwa vijana je walionyesha uzalendo? Ama fikra zao zilibaki kuwa mgando kama hawa wazee tu
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu embu fanya kurudia kuisoma upya hiyo post hapo juu uone kama hajamtaja mnafiki zitto
   
 7. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha Kamtaja aisee, Ile Ndugu aliyoianzishia mbele ya Kabwe ndio imenichanganya, hata Zitto mwenyewe akisoma anaweza asigundue kama katajwa.

  Unajua tatizo ZITTO ni huku kuandamana kwake na Magamba mimi binafsi kunanichanganya sana, yeye akiulizwa anasema anafanya siasa za kistaraabu, kasahau ukikaa na waridi utanukia waridi.

  samahani kwa kwenda nje ya hoja, naomba nimseme ndugu Kabwe kidogo,
  Zitto anatakiwa ajue kwamba kama ni swala la mvuto wa kisiasa hata NAPE,Mwinyi,Sioi,Ridhiwan,Malisa,Masha,Ngeleja,Malima wanao pia, lakini tunawakataa sababu ya UCCM wao. CCM is pathetic na wakati tunaichinja hatujali kilio chao cha huzuni tunachinja hivyo hivyo.

  Cha kustaajabisha kesho unaona yuko nao, tena anashiriki kweli kweli kudesign projects zao.

  I am fed up with this. He has to change or we will change
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  lusinde,chanda,shigella,malisa,millya,ridhiwani nape wote ni vijana lakini akili zao ni kama wassira,.vijana wengine wa upinzani kama kafulila na kabwe ni popo kama mzee shibuda..ujana sio kigezo kabisa,kuna wazee kama kitine na lwaitama wapo vizuri upstairs na wazalendo kuliko vijana 100 combined
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kama vijaa wenyewe ni lusinde na mwigulu... Then ni bora kuongozwa na mbwa
   
 10. J

  Jhung tiao Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo ni nja na uchu wa madaraka ndo maana wazee wanangangani kwenye kiti hawana lolote
   
Loading...