Joshua justine
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 793
- 1,007
Wakati wawakilishi wetu wanapambana kule bungeni wakikemea na kuwaweka kati mafisadi ,sisi kama raia tunapaswa kuwaunga mkono katika jambo hili.
Jambo hili ni letu sote, pesa ni za wavuja jasho wa kawaida kabisa nchi hii wanaolipa kodi halali usiku na mchana.
Hii ni vita ya kulikomboa taifa kutoka katika mfumo wa utumwa na ukoloni wa ndani ambao baadhi ya watanzania waovu walikuwa wanauandaa kwa muda mrefu tu.
Kama watu na makundi mbali mbali ya kiraia walivyoonyesha kuunga mkono jitihada za kudai uhuru wakati ule, ama kuandamana kuliunga mkono azimio la Arusha wakati ule, basi na sisi leo haya mapambano ni yetu pia, tusikae kufurahia tu U - TUBE kama tunaangalia movie iliyochezwa huko Hollywood, Nollywood ama Bollywood ambayo haituhusu hivyo kwetu ni kama burudani tu.
Jambo hili linatuhusu, sio burudani hii, tuamke kuwaunga mkono wabunge na bunge letu, ili juhudi hizi zisiishie kama mbio za sakafuni bali iwe ni badiliko litakalodumu la kitabia katika nchi hii. Hata vijana wanaokuja wasije kuja kujidanganya tena na kale kamsemo ka " CHUKUA CHAKO MAPEMA" , Utamaduni huo wa chukua chako mapema uishie hapo, na pesa zetu wananchi zituletee maendeleo yetu kama nchi.
Naunga mkono hoja, na nawachallenge makundi mbalimbali ya raia kufanya maandamano halali nchi nzima kuunga mkono bunge la 12 mkutano wa 9 kwa kazi nzuri waliotuonyesha watanzania.
# Aluta continua na kazi iendelee !
CRITICAL THINKING ;
Jambo hilo limewaudhi sana hao mafisadi jeuri, je vipi ikiwa ni wao ama watu wao ndio wanakuja na hoja ya kwamba ," wabunge wenyewe waliingia kwa kuiba kura", ? , Zinazotolewa hapa chini,
Fikiria tu