Tuambizane ukweli: Ikiwa Viongozi na Wanachama wa CHADEMA hawajui mambo madogo kama haya kuhusu uchaguzi! Wanawezaje kushinda uchaguzi?

Wasalaam wanajamvi

Nikiri wazi kuwa wanachadema na viongozi wao wanajua kila jambo na wao ni wataalam wa kila taaluma!

Lakini kinacho shangaza zaidi inakuwaje hawa magenious wanashindwa kufatilia vitu vidogo kama hivi kuhusu uchaguzi na taratibu zake?

Bado najiuliza ikiwa hawajui vitu vidogo kama hivi watatumia mbinu gani kushinda uchaguzi?

Nitaweka mambo machache yanayoshangaza kuhusu magenious wa chama cha demokrasia na maendeleo!

Moja, Mpaka leo hii wanachadema na viongozi wao hawajui kuwa hawataweza kupiga kura mahali popote ...bali ni pale walipo jiandikisha mpaka leo hii bado wanaulizana kwanini wakati hilo jambo liko kisheria na kanuni na linawasaidia hawa magenious wasilie kuwa tumeibiwa kura!

Mbili, hawa magenious hadi leo hawajui kuwa orodha ya wapiga kura ilishawai kubandikwa vituoni na ipo kwenye tovuti ya NEC na bado itabandikwa tena hadharani siku nane kabla ya kupiga kura! Lakini inashangaza imekuwaje wasomi hawa nguli hawajui vitu vidogo kama hivi? Hawa magenious kweli watashindahe uchaguzi?

Tatu, Hawa magenious hawajui kuwa mawakala wao watapewa orodha ya wapiga kura ya kituo husika na watakuwa nayo kituoni na hii inawasaidia kutokujidanganya na kudanganyana kuwa wataibiwa kura kwani kila mpiga kura atajulikana! Bado najiuliza ikiwa hawa magenious wetu hawajui vitu vidogo vidogo kama hivi kweli watashinda vipi uchaguzi?

Nne,Hawa magenious hawajui kuwa hadi leo hawana mamlaka ya kuchunguza mfumo wa kujumlisha kura wala kuugusa lakini wanadanganya wanachama!


Hivi kweli hawa magenious watashinda vipi uchaguzi.......
Wasikilizeni wananchi, mmewekeza nguvu kubwa sana CHADEMA CHADEMA, ACT ACT, MBOWE MBOWE ZITTO ZITTO.

Utafikiri hayo ndio matatizo ya watanzania.

MaCCM yamepewa MADARAKA na wananchi kwaajili ya kutatua matatizo yao ya MAJI, UMEME, AJIRA, AFYA UHURU yenyewe yako busy na vyama vya upinzani
 
Hawa ma genious pia hawajui kwamba baada ya uchaguzi wa wenyeviti kutowaridhisha wengi hawakuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kura. Walizira na kuanzisha kampeni nchi nzima ya kususia mchakato wa wa kuboresha taarifa zao na kuthibitisha kwamba wengi hawakujiandikisha walidhihaki sana takwimu za serikali kuhusu waliojiandikisha.
So wengi walioboresha taarifa zao moja kwa moja ni wana Ccm so wanaposema wanategemea ushindi unajiuliza watashinda vp wakati hawatapiga kura?
 
Back
Top Bottom