Tuambizane: Ni ipi hatma ya Wanafunzi wa Kidato Cha Sita waliopata Div.III?

MAKA Jr

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
256
185
Kuna wanafunzi wanalalamika, kwa nini wanapoomba au ku-apply kwenye vyuo na mitandaoni wanaambiwa hawana vigezo ili hali walifaulu kwa kupata Division III?

Au ndio kupanda kwa viwango vya elimu huku? Tuambizane wadau!
 
Na hii ni dalili kuwa wataendelea kusota tena watoto wa masikini.
 
Waachane na kufikiri juu
Wanatakiwa waanze kufikiri chini kwa sasa alafu huko juu watafika tu wakiwazaa degree wataozea mtaani na vyuo vinapunguzwa usije sikia vinafutwa vyote avina ubora si unajua chama cha mama...
 
kwa klerruu ni 2 Principal Passes,kwenye Hisabati na Sayansi,au kwa waliomaliza O-level na kupata ufaulu wa daraja la I-III wenye sifa za Credit katika masomo mawili ya ufundi ikiwemo Drawing,Hisabati,Engineering Science au Kemia.
 
Degree zenyewe hazilipi kama wanaweza waanze kujiajiri huko huko

Nilimuacha form four . Nikaenda high school,nikaenda chuo,miaka almost sita

Narudi mtaani naanza kufanya alichofanya yeye the last six years,
 
Nenda kaombe direct Chuo cha Maji, Ubungo kama uko na interest, only diploma.
 
Kuna wanafunzi wanalalamika, kwa nini wanapoomba au ku-apply kwenye vyuo na mitandaoni wanaambiwa hawana vigezo ili hali walifaulu kwa kupata Division III?

Au ndio kupanda kwa viwango vya elimu huku? Tuambizane wadau!

Div III omba katika vyuo vya Diploma levels. NACTE wametangaza course za diploma wahi
 
Back
Top Bottom