King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 51,657
- 68,615
Tunajenga kwa fedha zetu za ndani.Ujenzi wa mabwawa makubwa kama hili letu huwa unaambatana na mikopo mikubwa ambayo ishawahi kusababisha uchumi kuanguka katika nchi za Turkey, Brazil, Mexico, na Yugoslavia ya zamani
kwa mfano bwawa la Tarbela kwenye mto Indus huko Pakistan.Mwaka 1968, kiliwekwa kipengele cha interest ya 7.5 kwa ajili ya ku cover inflation na ucheleweshaji wa mradi. lakini mradi haukukamilika hadi 1984, ulichelewa kwa miaka 8, inflation ikawa imefikia asilimia 380 . Bwawa hilo likagharimu mara nne ya gharama iliyokadiriwa na kuongeza deni la taifa la pakistani kwa mara nne zaidi
Mabwawa huchukua average ya miaka 8.7 kujengwa na mara nyingi matatizo yanapotokea na waanzilishi mradi hawapo madarakani basi waliopo madarakani huangushia lawama wale waliotoka
Mnyika wa chadema siyo mjinga kutaka kuona mkataba wa Stiglers Gorge ,hata catherine Ruge alipodai the real cost ni 21 trliion na siyo 7 trillion she has a point
Kwanza huu mradi tunaambiwa ni fedha za ndani okay tuseme ni hivyo ila kweli ndiyo utachukua miaka mitatu??????,hiyo Gorge yenyewe ina urefu wa kilometa 8 na mita 100 kushuka chini sina hakika mradi uta cover eneo kisasi gani lakini selous ni kubwa zaidi ya nchi ya Uswis na ni 4/5 ya nchi ya Ireland,vilevile katika ujenzi wa mabwawa kuna hatua lazima ujenzi usimame ili kingo zishike vizuri,mistakes zikifanyika tujue ni KLIO KWA UCHUMI kwa miaka mingi ijayo NA MAISHA YA WATU. kwa mfano:
*Bwawa lilokuwa linajengwa huko nchini laos lilipasua kingo na kusababisha mafuriko yaliyoua watu 200 na kuwaacha wengine 6000 wakiishi kwenye mahema
*Mmonyoko wa ardhi ulisababisha uharibifu mkubwa katika bwawa la Ituango linalojengwa huko colombia na kusababisha watu 25,000 kuhamishwa huku mradi huo wa dollar bilion 5 ukiwa matatani
*Miaka mitatu iliyopita bwawa refu huko marekani liitwalo Oroville Dam lililopo kaskazini mwa California, nusu lipasuke na kusababisha kuhamishwa kwa watu 190,000 na matengenezo yaliyogharimu dola bilioni1.1
*.
mwisho kabisa,Ujenzi wa mabwawa kama ya kwetu una historia mbaya duniani kote.HUAMBATANA NA RUSHWA KUANZIA TENDA ZINAVYOTOLEWA,WANASIASA CORRUPT HUJIFAIDISHA,wengi hawaweki wazi mikataba ila mwisho wake gharama mradi unapoisha zinaongezeka siyo zile zilizosemwa mwanzo
Mfano mzuri ni kichekesho huko Congo,wanataka kujenga bwawa katika mto congo kwa gharama za dollar billion 80 na litakuwa bwawa kubwa duniani ila ni Mungu anajua tu what that means kwa nchi kama Congo
-NI JAMBO JEMA KAMA MRADI HUU WETU AMBAO UKIKAMILIKA LITAKUWA BWAWA LA PILI KWA UKUBWA AFRIKA UENDE KI UWELEDI
*mazingira ya Ecology yazingatiwe
*mkataba uwekwe wazi tujue nchi itabebaje mzigo miaka ya mbeleni tusidanganyane eti bwawa la pili kwa ukubwa Africa litakamilika kwa 3.6 bilion dollars
*Hii story ya kwamba litakamilika ndani ya miaka 3 ndiyo inanipa wasiwasi na this whole issue,ni kwamba mnafosi kwa ajili ya masifa au?hizo KINGO ZITAKUJA KUPASUKA na roho zitakazopotea zitakuwa juu yenu,maana siyo chini ya watu laki moja watakufa na vile vinyumba vya udongo yarabi toba