Tuambiwe ukweli, Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na wengine wote wamelala wapi? Halafu tusameheane

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,308
2,000
Unaweza kushangaa kwanini nimeileta hoja hii upande wa jukwaa la HISTORIA, wakati ni jambo lililozungumzwa ktk mkutano wa kampeni za uchaguzi.

Kati ya mwaka 1964 na 71,Khassim Hanga, Idris Abdalah Majura, Abdul Aziz Twala, Mdungi Ussi, Saleh Sadalah, Jaha Ubwa, Juma Ringo, Othman Sharif, na wengine, walikamatwa na vyombo vya dola vya Zanzibar, na hawajapatikana mpaka leo hii.

Jana katika mkutano wake wa kampeni wa, Tundu Lissu aliwataja wahanga hao wa siasa za Znz. Itakumbukwa kwamba aliwahi kuwataja tena katika Bunge Maalum la Katiba la mwaka 2013.

Umpende, au umchukie, Tundu Lissu, ni mwanasiasa ambaye akizungumza huwezi kuchoka kumsikiliza.

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
22,308
2,000
..sina uhakika kama kuna mwanasiasa wa Tanganyika ambaye amepata kuwataja wahanga hao waliopotezwa Zanzibar.

..ukiacha hao wa miaka ya 60 na 70 kuna waliouwawa baada ya uchaguzi wa 2000 nao wanapaswa kufutwa machozi na kufarijiwa.
 
Bill

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
6,531
2,000
Unaweza kushangaa kwanini nimeileta hoja hii upande wa jukwaa la HISTORIA, wakati ni jambo lililozungumzwa ktk mkutano wa kampeni za uchaguzi.

Kati ya mwaka 1964 na 71,Khassim Hanga, Idris Abdalah Majura, Abdul Aziz Twala, Mdungi Ussi, Saleh Sadalah, Jaha Ubwa, Juma Ringo, Othman Sharif, na wengine, walikamatwa na vyombo vya dola vya Zanzibar, na hawajapatikana mpaka leo hii.

Jana katika mkutano wake wa kampeni wa, Tundu Lissu aliwataja wahanga hao wa siasa za Znz. Itakumbukwa kwamba aliwahi kuwataja tena katika Bunge Maalum la Katiba la mwaka 2013.

Umpende, au umchukie, Tundu Lissu, ni mwanasiasa ambaye akizungumza huwezi kuchoka kumsikiliza.

Labda tumwamahe Karume RIP atuonyeshe walipo, ukituuliza sisi ni sawa na wewe tu hatuna majibu.
 
Makala josee

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
284
250

Nini kilisababisha kukamatwa kwao...!? Jibu ya swali hili ni muhimu ili kuboresha mjadala.

..Vyombo vya dola, na CCM, wamekuwa kimya kuhusu suala hili kwa muda wote.

..Hawaelezi kwanini walikamatwa. Na haielezwi nini kiliwakuta. Na haielezwi miili yao iko wapi.

cc Mohamed Said
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,233
2,000
..Vyombo vya dola, na CCM, wamekuwa kimya kuhusu suala hili kwa muda wote.

..Hawaelezi kwanini walikamatwa. Na haielezwi nini kiliwakuta. Na haielezwi miili yao iko wapi.

cc Mohamed Said
Asante kwa majibu.

Kama nitakuwa sikubebeshi mzigo mzito, Naomba msaada wa hili.
Labda, kwa kunisaidia ili niwajue vizuri; naweza kupata wasifu wa kila mmoja mpaka muda wanatoweka? Yaani hasa shughuli walizokuwa wakizifanya na hata ukaaji wao kwa jamii na mahusiano yao na uongozi wa nchi kwa wakati huo.

Natanguliza shukrani.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,522
2,000
Dah!

Ndugu yangu JokaKuu umenikumbusha mbali sana kuhusu siasa za Zanzibar... siasa zilizojaa chuki, uhasama, hinda, na kila hiyana kwa miongo na miongo!

Siasa za ASP na "Hizbu" ambazo bila aibu zimekuja kurithiwa na CCM!

Itabidi nitafute wasaa ili niirejee!
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,522
2,000
Asante kwa majibu.

Kama nitakuwa sikubebeshi mzigo mzito, Naomba msaada wa hili.
Labda, kwa kunisaidia ili niwajue vizuri; naweza kupata wasifu wa kila mmoja mpaka muda wanatoweka? Yaani hasa shughuli walizokuwa wakizifanya na hata ukaaji wao kwa jamii na mahusiano yao na uongozi wa nchi kwa wakati huo.

Natanguliza shukrani.
Nikipata wasaa hapo baadae, naweza kueleza machache kuhusu hao wengine endapo JokaKuu atakuwa hajafanya hivyo bado. Lakini kwa haraka harka, hususani kupitia suali lako la awali, ngoja nimuelezee kwa uchache Abdallah Kassim Hanga!

Hanga alikuwa ni miongoni mwa wasomi wa mwanzoni kabisa ambae baada ya kumaliza High School Westminster College, London, baadae akaenda Lumumba University- Moscow.

Akiwa Soviet, Hanga alibahatika kuacha damu yake, mwanamama Elena Hanga (Yelena Khanga).

Huyu Elena ni Mwandishi wa Habari, amefanya sana TV Talk Shows, na kwa kifupi, ni maarufu sana kule Urusi ingawaje kwa sasa anaishi US.

Kwenye video hapo juu, kuanzia dakika ya 14:55 unaweza kumuona Elena Hanga!!

Back to Hanga, kabla ya kwenda Moscow kusoma, alikuwa na nia ya kwenda kusoma US lakini inasemekana akabaniwa Viza!! Lakini kukataliwa huko hakushangazi kwa sababu wanafunzi wengi kama sio wote kutoka Zanzibar waliokuwa UK walikuwa ni Marxists.

Miongoni mwao ni pamoja na Abdulrahman Babu aliyekuwa ameegemea China, huku Hanga kama walivyokuwa wengine wa ASP aliegemea Soviet Union.

But unlike Mzee Karume ambae alikuwa ni kiongozi mwenye msimamo wa wastani, Abdallah Kassim Hanga alikuwa radical.

REMEMBER: Mwanzoni Babu alikuwa ZNP... Maarufu kama Hizbu au "Chama cha Waarabu". Wazalendo wengine ambao hadi kesho "hawajasemehewa" na wanazi wa CCM kule ZNZ na bado wanaitwa Waarabu kwa sababu tu walikuwa ZNP ni pamoja Salim Ahmed Salim (SAS).

Wote, Babu na SAS waliitumikia ZNP kwa posts za juu huku Babu akiwa Secretary-General na SAS aliwahi kuwa Deputy Chief Representative of the Zanzibar Office ambayo ilikuwa Cuba, na wakati huo alikuwa just a young boy of 21 years.

Babu na SAS nimewadokezea hapa kwa sababu historia zao zinafanana fanana na Abdallah Kassim Hanga. Mosi, wote hawa walikuwa wasomi, pili wote walikuwa Wakomunist, tatu walionekana kama radicals.

Hawa radicals wa Umma Party (from ZNP) na wale wa ASP, mapema tu walitia nia ya kuuondoa utawala wa ZNP/ZPPP uliokuwa chini ya Sultan wa Zanzibar.

Ni kutokana na hiyo extremism traits ndio maana haishangazi kuona Babu na akina Ahmed bin Abubakar Qullatein , maarufu kama Badawi Qullatein walijitoa ZNP na kuunda Umma Party ambayo pia SAS alikuwa ni mmoja wa vijana wa Umma Party.

Baada ya mapinduzi kufanyika, Abdallah Kassim Hanga akatangazwa kuwa PM na Mzee Karume kama Rais. Inasemekana Mzee Karume hakupenda kabisa huo "Urais" ambao kwa mfumo ambao ulikuwepo ZNZ kwa wakati ule, PM alikuwa ndie Mtendaji Mkuu... British System!

Lakini kwavile mfumo huo ulikuwa ndo ule ule aliokuwa ameuacha Sultan (monachy system), baadae cheo cha PM kikafutwa na Hanga akateuliwa kuwa Makamu wa Rais.

Baada ya mapinduzi na baadae muungano na Tanganyika, wale radicals wa Umma Party na ASP bado hawakuaminika na Karume! Mtu kama Babu hakuaminika hata Nyerere possibly kwavile walionekana bado wana ile damu ya kimapinduzi huku wakiwa wafuasi wakubwa wa Ukomunist.

Huo Ukomunist wao uliwafanya waangaliwe jicho la kwa tahadhali hata na watu wa Magharibu, kiasi kwamba vijana wa Umma Party waliokuwa wamepelekwa Cuba kuchukua mafunzo ya kijeshi, baada ya kurudi wengine walikuwa wanadhania ni wa-Cuba kutokana na muonekano wao .

Umma Party.png

So, baada ya muungano, Mzee Karume (possibly kwa kushirikiana na Nyerere) akaamua wale "Wakorofi" wawe mbali na SMZ, na katika kufanikisha hilo, Babu na Hanga wakapelekwa kuhudumu Serikali ya Muungano, na SAS akapelekwa Ubalozi Egypt.

Aidha, tukumbushane kwamba Hanga alikuwa ni rafiki mkubwa sana, tena sana wa Oscar Kambona!!

Kilichotokea hasa ni nini, ni ngumu kufahamu lakini pamoja na madai ya Karume kuwahofia sana wasomi na wanamapinduzi, inasemekana pia Karume alimuhofia Hanga kutokana na kukubalika kwake na watu wengi wa ZNZ.

Aidha, inasemekana kwamba baada ya rafiki mkubwa wa Hanga, yaani Kambona kuhitilafiana na Mwalimu na hatimae kutorokea Uingereza, Hanga nae akapoteza interest kutumikia serikali ya Nyerere, jambo ambalo lilipelekea kufutwa nafasi ya uwaziri.

Labda kwavile alishaanza kunusa hatari huku Swahibu wake akiwa amekimbilia uhamishoni, Hanga nae "akakimbilia" Conakry, Guinea.

Wakati akiwa Guinea, kukawa na tuhuma kwamba kuna watu walipanga kumpindua Mzee Karume, na watu hao walipanga mapinduzi yakishafanyika basi Abdallah Hanga arejee ZNZ na hatimae kuwa Rais!

Inavyoelekea, Mwalimu akala njama na Karume kumtaka Hanga arejee nyumbani. Katika kufanikisha hilo, Mwalimu akaongea moja kwa moja na Rais wa Guinea ili amweleze Hanga arudi nyumbani kwa ahadi kwamba asingefanywa chochote!

Na kwa kuwa Hanga aliamini hakuwa na tatizo na Mwalimu, na kwa kuwa Mwalimu huyo huyo alipata kum-defend mara mbili Othman Sherrif ambae kama ilivyokuwa kwa akina babu, baada ya muungano yeye alitupwa ubalozi US, Abdallah Kassimu Hanga akajiona yupo safe na kwahiyo akarejea TZ.

Baada ya kutua TZ, kuna maelezo ya aina mbili! Kuna maelezo yanayodai baada ya kutua TZ, Mwalimu aliamrisha Hanga apelekwe ZNZ, lakini kuna maelezo mengine yanayodai baada ya kutua TZ, aliwekwa kizuizini lakini baadae akaachiwa!

So, kufuatia zile tuhuma kwamba alikuwa amepanga mapinduzi ya kumuondoa Karume madarakani, hiyo theory ya pili ndo ina-conclude hatimae Karume akasafiri hadi Dar kukutana na Mwalimu kwa lengo la kumtaka Mwalimu amsafirishe Hanga to ZNZ huku akiwa na "ushahidi" kuhusu uhaini wa Hanga dhidi ya SMZ!

Mwalimu akatiii, na hatimae Abdallah Kassimu Hanga akasafirishwa to Zanzibar ambako hadi leo "hajulikani alipo" manake hata kaburu lake "hakuna anayejiua" lipo wapi!
 
core22

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
536
1,000
Unaweza kushangaa kwanini nimeileta hoja hii upande wa jukwaa la HISTORIA, wakati ni jambo lililozungumzwa ktk mkutano wa kampeni za uchaguzi.

Kati ya mwaka 1964 na 71,Khassim Hanga, Idris Abdalah Majura, Abdul Aziz Twala, Mdungi Ussi, Saleh Sadalah, Jaha Ubwa, Juma Ringo, Othman Sharif, na wengine, walikamatwa na vyombo vya dola vya Zanzibar, na hawajapatikana mpaka leo hii.

Jana katika mkutano wake wa kampeni wa, Tundu Lissu aliwataja wahanga hao wa siasa za Znz. Itakumbukwa kwamba aliwahi kuwataja tena katika Bunge Maalum la Katiba la mwaka 2013.

Umpende, au umchukie, Tundu Lissu, ni mwanasiasa ambaye akizungumza huwezi kuchoka kumsikiliza.

Tafuta KUMBUKUMBU ZA MZEE AMAN THANI AKIELEZEA ALICHOKIONA NA YALIOMFIKA
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
10,139
2,000
Labda tumwamahe Karume RIP atuonyeshe walipo, ukituuliza sisi ni sawa na wewe tu hatuna majibu.
Sema hivi... 'ukiniuliza mimi hakuna ninachojua'.... And not 'ukiniuliza sisi' maana wewe peke yako ndiyo hujui lakini kuna wengine kama akina Lissu wanajua. Acheni kabisa hii tabia mbaya ya shida zako binafsi kuzifanya za wote au sisi.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,233
2,000
Kwenye video hapo juu, kuanzia dakika ya 14:55 unaweza kumuona Elena Hanga!!
Asante sana, Mkuu. Kwa maelezo ya kina. Mkuu, Post yako ime'summarise' vizuri sana maelezo mengi niliyopitia jana juu ya K. Hanga (R.I.P).

Pia nashukuru, Umeniwezesha leo kumuona 'mtanzania' mwenzetu Elena. Nina imani, akiamua kurudi nyumbani tutamkaribisha.
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
17,233
2,000
Mwalimu akatiii, na hatimae Abdallah Kassimu Hanga akasafirishwa to Zanzibar ambako hadi leo "hajulikani alipo" manake hata kaburu lake "hakuna anayejiua" lipo wapi!
Asante sana Mkuu, Post yako ime'summarise' vizuri sana maelezo mengi niliyopitia jana juu ya K. Hanga (R.I.P).
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom