Tuambie kama ungeweza kuzirudisha siku nyuma, ungetamani urudi kipindi kipi na ungelifanya nini?

Ndengaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
7,355
13,152
...Natamani kingerudi kile kipindi nilichokua na baba na mama wakiniambia fanya hichi, na mimi nafanya kile kwakuona kuwa mimi ni bora kuliko wao, kwakweli ningewasikiliza kila lililo jema kwao na kulitekeleza bila kuhoji,...!

Na wewe je... ? Maana wanasema majuto ni mjukuu!.
 
-Kitu pekee tunachojidanganya walimwengu ni kwamba haya maisha tunayopitia ni sisi wenyewe ndo tumeyataka.

-Uhalisia ni kwamba Mungu ana makusudi na wewe hapo ulipo, hata kama ukaamua irudishe miaka nyuma, kama kusudi lake uwe hivi basi hauwezi kuwa vile.

-Kitu pekee ni wewe kumuomba Mungu utambue kusudi lake ni lipi mpaka kukufikisha hapo wewe ulipo, ukijua kusudi ni utafurahia zaidi hapo ulipo na utakuwa na amani ya Mungu.

***Zawadi ya Mungu ni haya maisha tunayoishi****
 
Kuna demu mmoja alikuwa ni mzuri hatari, alikuwa ananipenda sana ila mimi nilikuwa naogopa kumuanza kwa kuwa nilikuwa nahisi ile ilikuwa ni mitego tu ili nimtongoze halafu ajichukulie point 3 kwa kunitolea nje.
Baada ya kumaliza shule kila mtu alienda kwao. Hapo ndipo alipoanza kuniambia kuwa ananipenda sana, na anasikitika kuwa kipindi chote tulipokuwa shule nilishindwa kuligundua hilo (ingawa nilikuwa najua, ila sikutaka ajue kuwa nimeshajua kuwa ananipenda). Nadhani alifunguka hivyo kwa alijua sio rahisi yeye kukutana na mimi tena (na hatukuwahi kukutana tena hadi tulipopoteza mawasiliano kabisa)

Hapo ndipo unaponitamanisha mkuu..!
 
1.1.2015

Hii siku ingewezekana kurudi ningebadilisha kila kitu siku hiyo wallah!!

Siku mbaya sana hii
 
Muda nlio upoteza kwa mambo ya kibwege ningeutumia vzr huenda nsingekuwa hapa nlipo
 
Ningerudi hadi mwaka 2005 na kumwambia mtu mmoja namna alivyo muhimu kwangu. Kwa sasa ni mwana ndoa huko aliko and I'm happy that she enjoys life there.
 
...Natamani kingerudi kile kipindi nilichokua na baba na mama wakiniambia fanya hichi, na mimi nafanya kile kwakuona kuwa mimi ni bora kuliko wao, kwakweli ningewasikiliza kila lililo jema kwao na kulitekeleza bila kuhoji,...!

Na wewe je... ? Maana wanasema majuto ni mjukuu!.
Ningetamani niwe tena kijana halafu itokee siku hiyo nilikua na mwanafunzi chumbani kwangu nikakamatwa nae na polisi
 
Nataman light ngesoma
Nkazngatia ushaur wa wazaz
Kuwa soma n kwa faida yako

Nsingekua nalilia uchumi
Now dhaaa

Somen wajamen mnao somaaa
 
2008 nilivyochukua mkopo wa pesa na kuchanga na mpenzi wangu ili tufanye biashara...

Baada ya miez miwili akakata mawasiliano na mimi.. Nilihangaika sana kurejesha lile deni..

Mungu mkubwa nilimaliza cha ajabu jamaa hakufanya kitu cha maana zaid ya kuhonga hawara zake... Duuuu kweli mwanaume sio ndugu yako..
 
Japo sasa mm ni mtu mzima lakini ck zngerud nyuma nimemiss nimwone mama angu aliyefarik mwaka 1996 nikiwa darasa la kwanza. MPAKA LEO NAMKUMBUKA SANA MAMA ANGU.
 
...Natamani kingerudi kile kipindi nilichokua na baba na mama wakiniambia fanya hichi, na mimi nafanya kile kwakuona kuwa mimi ni bora kuliko wao, kwakweli ningewasikiliza kila lililo jema kwao na kulitekeleza bila kuhoji,...!

Na wewe je... ? Maana wanasema majuto ni mjukuu!.
Although its imagination.

Binafsi nikirudi ubachelani ili nifikirie upya wazo langu la kuoa. Maana she is a pain in my ass right now.
 
Back
Top Bottom