Tuambie jambo/kitu unalo/unachokumbuka kipindi ukiwa unakua.

King Shaat

JF-Expert Member
Aug 30, 2013
863
835
Habari WanaJF,

Poleni na majukumu ya maisha.

Kumradhi kama kuna uzi ulishawahi kuwepo wenye maudhui kama kichwa cha habari kinavyosema.

Emb tukumbushe mambo/vitu/mitindo yaliyokuwa yakitia fora kipindi ukiwa unakua; iwe ulivyokuwa mdogo, katika harakati za elimu, mtaani/kwenye jamii, n.k.

Binafsi, nakumbuka mazingaombwe enzi zile za shule ya msingi. Enzi hizo kina Power Mabula (sijui kama jina nimelipatia) na wanamazingaombwe wengine wakija mashuleni af inabidi ulipie shilingi 100 kama sikosei ili uweze kuona "maajabu" wanayofanya.
Hivi, siku hizi bado yanafanyika mashuleni?

Pia nakumbuka kuna kipindi sherehe mitaani zilikuwa hazinogi kama wimbo wa Awilo au Vulindela haujapigwa.

Na sasa kila nyimbo ya Bongo Fleva za enzi zile, 2000 - 2010s mwanzoni, kuna namna zikiplay (hata tu kichwani), zinakumbusha enzi hizo sana. Nyimbo kama Starehe ya Ferooz, Hakuna Kulala ya Juma Nature, Mikasi, n.k.

Emb tuambie kile unachokumbuka wewe!
 
Nakumbuka nilipigwa mnooooo baada ya kuiba pesa ya kwenda kununulia daftari la shule.nilimuomba mama pesa ya daftari akaniambia nitakupa Kesho wewe nenda shule…nikajitia kichwa ngumu.jamani nilipigika mfano hakuna

Ilinipa funzo kwenye maisha yangu ya ukuaji.Siwezi kuchukua kitu ambacho sio mali yangu.ile hofu mpka sasa ipo😂😂
Kama sijakosea ilikuwa 1999/2000😃😃nishazeeka hakyamama tena😂
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom