Tuacheni utoto, mnataka Viongozi wa CHADEMA wafanye nini zaidi?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Humu kwenye mitandao kuna utoto mwingi sana!

Utoto hubeba dhana ya kudhani kila kitu kinawezekana kwa mwingine wakati wewe huwezi kukifanya.

Kwa mfano, mtoto anaweza kukulamikia akitaka umpe pesa wakati yeye hawezi kuitafuta!

Inashangaza sana unaposoma mabandiko ya baadhi ya watu eti wakilalamika na kutoa lawama kwa viongozi wakuu wa CHADEMA wakiwataka wafanye jambo/mambo ambayo wao wenyewe hawawezi.

Mtu yuko nyuma ya keyboard/keypad lakini eti anatoa lawama kwa viongozi wa CHADEMA wakidai uongozi umewashinda. Huu ni ujinga au ubinafsi na unafiki wa hali ya juu!

Utoto wao ambao unajengwa na ujinga unawafanya washindwe kuelewa kuwa kwa sasa walichonacho viongozi wakuu au maarufu wa CHADEMA ni kikubwa au kina gharama kubwa kulingana na uwezo wao ukilinganisha na kile watoto wa kwenye mitandao wanakitaka.

Kwa mfano Pesa anazoingiza Mbowe kutokana na miradi ya kisiasa na kibiashara ni nyingi zaidi kushinda mchezo wa kamari ya kisiasa kupitia maandamano yasiyo na ridhaa ya polisi. Katika kuhakikisha maisha yake yako salama, ndio maana kwa sasa amejificha huku akifanya mazungumzo na serikali kuona ni jinsi gani wataimaliza kadhia ya kuandamana bila ridhaa ya polisi.

Lowassa ni bilionea anayetegemea ulinzi wa serikali katika biashara zake na familia yake ndio maana aliomba kuonana na Rais ili kuweka mambo yake sawa. Usitegemee kumuona Lowassa kwenye maandamano ambayo yeye huita ni siasa za kitoto au kiharakati.

Lema, Msigwa, Sugu kwa sasa ni wafanya biashara na Mamilionea ambao kabla ya kuingia bungeni walikuwa ni 'makapuku'. Hawa hawawezi kujiingiza tena kwenye mtego wa kuhatarisha biashara na familia zao kwa jina la siasa kupitia maandamano wakati wanajua athari watakazozipata ni kubwa zaidi ya kile walichonacho hasa ikizingatiwa kuwa hawana tishio la kupoteza biashara na ubunge wao ambao unazidi kuwaingizia faida hata kama hawataandamana.

Wanachokifanya viongozi wakuu wa CHADEMA ni sawa na mtu aliyefanikiwa katika malengo yake kutokana na uwezo wake halafu anajitokeza mtu/kikundi kingine na kuanza kumtaka acheze kamari kwa kutumia mafanikio yake. Haiwezi kutokea akacheza kamari ya aina hiyo.

Hizi ni kanuni za kimaisha ambapo binadamu anapofikia kiwango fulani cha utajiri huanza kulinda zaidi afya yake/maisha yake kwa ujumla kutokana na hofu ya kupoteza maisha.

Kwa upande mwingine, mtu asiyekuwa na utajiri mkubwa yuko tayari kucheza hata kamari ya uhai kwa sababu uhai kwake sio suala muhimu sana ukilinganisha na utajiri.

Kipindi ambacho Lema, Msigwa na Sugu wakiwa masikini kabla yakuwa wabunge ndio kipindi ambacho walikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha maandamano yasiyo na ridhaa ya polisi kiasi kwamba Arusha, Mbeya na Iringa ilikuwa ni uwanja wa mapambano.

Kama kuna mtu bado hajajua kanuni za kibinadamu basi huyo atasubiri sana maandamano kutoka kwa viongozi wakuu wa CHADEMA.
 
It's possible when God was throwing intelligence down to the Earth, you were holding an umbrella.
 
Mitandaoni kuna nguvu kubwa inatumika kuwakatisha watu tamaa juu ya kuandamana.

Mmemkodi Musiba.

Jana kuna mtu kaleta hoja kama hii.

Leo mapema tu uzi mwingine umekuja.

Mnachofeli ni hoja na kuvaa viatu vya wahusika.

Katika elfu saba unayopewa Lumumba nitumie elfu tano tu nikuandikie kitu chenye mashiko cha kudiscourage maandamano.
 
Back
Top Bottom