Tuacheni utani, Frank Lampard ni bonge la kocha

Mayala B

JF-Expert Member
May 13, 2019
1,450
3,379
Kama kichwa kinavyosomeka hapo juu

Tukiacha tu utan aliyekuwa nyota wa Chelsea na sasa kocha wao frank lampard ni bonge la kocha

Kwanza hana mchezaji tegemeo wa kuweza amua matokeo kama team zingine

Pili hajasajili kabisa

Tatu hazard alisepa na kuicha team mkiwa

Nne ana vitoto vya academy masikin wa Mungu vitoto ambavyo hata havijulikan vilicheza wapi kama vi mason, tomori, Abraham sijui na ki james kile kidogo ambacho hata league kuu England hakijawahi kucheza lakin juzi kilicheza kwenye UEFA zidi ya lile

Huyu jama ni bonge la kocha nina uhakika top four kwake lazima
 
Kiongozi top four bado sana hii ligi Ina laana kama sio ladha miaka ya nyuma Manchester ilikuwa ikifika krismas halafu anaongoza hiyo ilikuwa hamna namna zaidi ya nyinyi wengine mtafute nafasi ya pili au nafasi ya tatu lakini baada ya viwango vya timu kufanana,betting,na mambo mengine yaani bingwa sasa inabidi tusubiri mpaka mwezi wa tano,lampard kwa siku chache nilizomuona anaugonjwa wa kushindwa kufanya maamuzi ya kufanya sub,kwenye mbinu naona hapo baadae anaweza kufuata nyayo za Alex,mou,na babu wa Bayern
 
Namuunga mkono mtoa mada lampard ni bonge la kocha imagine Chelsea wameondokewa na hazard ambaye alikuwa ni top score wa timu na most assist wao lakini kwa muda mfupi tangu atue lampard
Chelsea wameshamsahau hazard teyali.pia amembadilisha jorginho kutoka jorginho wa kupiga back pass kuwa wakupiga forward pass lakini pia kumuongezda makali Abraham ambaye alikosa penati dhidi ya Liverpool kwa kocha mwingine asingemuamini tena Kama Mourinho alivyomuuza lukaku akiwa Chelsea baada yakukosa penati lakini lampard kamuamini na sasa Abraham yupo kwenye kiwango Cha juu.hata ukiangalia inavyocheza Chelsea haionekani Kama ni team inayotengenezwa unaonekana ni team yenye wachezaji waliokaa muda mrefu kutokana na chemistry nzuri aliyotengeneza lampard kwa muda mfupi.hii ndio tofauti ya olegunar na lampard.kwangu namuona anaingia top 4 kabisa.
 
Nimeangalia mechi chache za Chelsea msimu huu lakini naona kiwango chao kinakuwa kwa kasi sana kila siku. Lampard ni bonge la kocha ila tu asije akapata tamaa ya kuja kuongeza wachezaji wengi mastaa huko baadae watamuharibia timu. Akikaa na hawa wachezaji miaka mitatu mfululizo akaongeza wachezaji wachache wenye uwezo lakini wasio na majina makubwa hakika hakuna atakayeikamata Chelsea sioni Uingereza tu bali duniani kote.
 
Uyu jamaa kuna kitu anacho ata akifugwa kuna kitu kinaonekana alikuwa anatafuta ila mwisho ligi bado mbichi
 
Hata yule Mmasai wa Man u alianza hivi hivi mpaka akapewa mkataba mrefu
 
Shida ipo kwenye beki line na kipa...hapo akiweza kuja kuparekebisha basi chelsea ileeeee itarudi tena
 
Kama kichwa kinavyosomeka hapo juu

Tukiacha tu utan aliyekuwa nyota wa Chelsea na sasa kocha wao frank lampard ni bonge la kocha

Kwanza hana mchezaji tegemeo wa kuweza amua matokeo kama team zingine

Pili hajasajili kabisa

Tatu hazard alisepa na kuicha team mkiwa

Nne ana vitoto vya academy masikin wa Mungu vitoto ambavyo hata havijulikan vilicheza wapi kama vi mason, tomori, Abraham sijui na ki james kile kidogo ambacho hata league kuu England hakijawahi kucheza lakin juzi kilicheza kwenye UEFA zidi ya lile

Huyu jama ni bonge la kocha nina uhakika top four kwake lazima
Wameachieve nini mpaka sasa?
 
Namsuburia December pale kwenye mengi za mfululizo. Mara nyingi sana kazi ya wanaume na wavulana huanza kuonekana December
 
Back
Top Bottom