Tuacheni unafiki jamani: Kanumba na Sokoine waliishi ukristo upi?

Setuba Noel

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
426
210
Hao watu wamefariki, safari yao ya duniani imeisha mengine anayajua Mungu huko mbele ya safari. Lakini huku bado tuna vimbelembele mara maaskofu mara wachungaji wanaotaka kutudanganya kuwa hawa walikuwa wakristo sana, wa kuigwa! Ya kweli haya jamani au ni unafiki tu? Mtu aliyekufa katika mazingira ya ulevi na ugomvi na mtu anayedaiwa ni mpenzi (si mke) wake, ameishi ukristo gani? Au mwenye wake wawili anafuata ukristo gani? Au mtu akishakuwa maarufu ndiyo basi maaskofu wanamwona ni 'kete' ya kujipandishia chati? Tukubaliane kuwa hawa watu walikuwa maarufu na wazuri kwa vigezo vya mambo yaliyowapa umaarufu, ambayo hayawafutii mifano ya kupinga ukristo waliyoonesha. Tuwasifu kwa waliyotufurahisha nayo na si kwa kutumia ukristo maana hawakuwa mabalozi wa ukristo hawa. Nimemwona Kardinali Pengo akimsifia Sokoine kuhusu uimara na umakini wa imani ya kikristo, nikashangaa sana. Najua marehemu Sokoine alizingatia imani yake ya kimasai na hata akawa na wake wawili kwa mujibu wa mila zake, hilo ni sawa na ni sahihi sana kwa mujibu wa mila zake, lakini ni tofauti na imani ya kikristo. Tumpongeze kwa msimamo wake wa kisiasa, wa dini tuuache maana hakuifuata hivyo. La marehemu Kanumba nililiona na kulisikia siku ya ibada ya mazishi iliyoongozwa na yule askofu wa AIC. Jamani sifa za uongo hazimpeleki mtu mbinguni. Kanumba anazo sifa zake za kutosha zinazotokana na kazi zake za usanii, hizo nyingine za kumtungia baada ya kifo acheni jamani zitawapotosha wakristo wengine wanaojitahidi kufuata imani ya kikristo.
 
amini Mungu yupo na uendane na yale anayoyataka ila usiwe mshabiki wa dini. Utapotea hapa duniani na umaskini ukikuandama. Kuna wengine wamechagua moja, bora wale raha duniani na wakateseke mbinguni. Kuna wengine wamechagua mateso ya kote kote. Waliochagua raha ya mbinguni tu ni wachache sana! Ukiwa mshabiki wa dini utafuata kila mchungaji analokwambia hata kama ni kudhulumu mali za wasiojiweza.
 
Hao watu wamefariki, safari yao ya duniani imeisha mengine anayajua Mungu huko mbele ya safari. Lakini huku bado tuna vimbelembele mara maaskofu mara wachungaji wanaotaka kutudanganya kuwa hawa walikuwa wakristo sana, wa kuigwa! Ya kweli haya jamani au ni unafiki tu? Mtu aliyekufa katika mazingira ya ulevi na ugomvi na mtu anayedaiwa ni mpenzi (si mke) wake, ameishi ukristo gani? Au mwenye wake wawili anafuata ukristo gani? Au mtu akishakuwa maarufu ndiyo basi maaskofu wanamwona ni 'kete' ya kujipandishia chati? Tukubaliane kuwa hawa watu walikuwa maarufu na wazuri kwa vigezo vya mambo yaliyowapa umaarufu, ambayo hayawafutii mifano ya kupinga ukristo waliyoonesha. Tuwasifu kwa waliyotufurahisha nayo na si kwa kutumia ukristo maana hawakuwa mabalozi wa ukristo hawa. Nimemwona Kardinali Pengo akimsifia Sokoine kuhusu uimara na umakini wa imani ya kikristo, nikashangaa sana. Najua marehemu Sokoine alizingatia imani yake ya kimasai na hata akawa na wake wawili kwa mujibu wa mila zake, hilo ni sawa na ni sahihi sana kwa mujibu wa mila zake, lakini ni tofauti na imani ya kikristo. Tumpongeze kwa msimamo wake wa kisiasa, wa dini tuuache maana hakuifuata hivyo. La marehemu Kanumba nililiona na kulisikia siku ya ibada ya mazishi iliyoongozwa na yule askofu wa AIC. Jamani sifa za uongo hazimpeleki mtu mbinguni. Kanumba anazo sifa zake za kutosha zinazotokana na kazi zake za usanii, hizo nyingine za kumtungia baada ya kifo acheni jamani zitawapotosha wakristo wengine wanaojitahidi kufuata imani ya kikristo.

kwani mtu kuwa msafi ni kutokuwa na weke wawil? Jibu nadhan c kwel hivyo basi hakuna alie msafi kwa kjihakikishia yeye mwenyewe wewe angalia matendo yako na safari yako ya kuelekea huko
 
ah una hasira sijui ungepewa cheo cha kuwa Mungu kama tungekua hai!

acha kuhukumu usiyoyajua maana kama walifanya toba sekunde ya mwisho hujui
 
Muanzisha hoja umesema ukweli. Wanaokupinga wana ugonjwa wa ukanumba. Kanumba alikuwa mzinzi kama mimi na sote hatustahili kuitwa wacha Mungu. Askofu aliyemsifia kuwa ni mcha Mungu katoka ukoo wa lusuferi. Walaaniwe wote waushabikiao uzinzi na ubakaji kama alivyofanya Kanumba.
 
Pumbavu sana! Sio lazima kuchangia.
 
amini mungu yupo na uendane na yale anayoyataka ila usiwe mshabiki wa dini. Utapotea hapa duniani na umaskini ukikuandama. Kuna wengine wamechagua moja, bora wale raha duniani na wakateseke mbinguni. Kuna wengine wamechagua mateso ya kote kote. Waliochagua raha ya mbinguni tu ni wachache sana! Ukiwa mshabiki wa dini utafuata kila mchungaji analokwambia hata kama ni kudhulumu mali za wasiojiweza.

note: Hakuna mateso mbinguni bali kuzimu au jehenam
 
kwani mtu kuwa msafi ni kutokuwa na weke wawil? Jibu nadhan c kwel hivyo basi hakuna alie msafi kwa kjihakikishia yeye mwenyewe wewe angalia matendo yako na safari yako ya kuelekea huko

Wala sijasema hivyo. Kuwa na wake wawili au hata wangapi zaidi ni sahihi kulingana na imani ya mtu anayofuata, lakini si fundisho la kikristo, kwa hiyo katika ukristo si sahihi.
 
Setuba Noel
siku ukifiwa/ukifa haya maneno tutayasema
kwa ajili ya ndugu/yako, je utajisikiaje.

Waache wafu wawazike wafu wao.

Ninachosema ni kuwa askofu angefanya ibada ya mazishi aishie hapo, na siyo kuwaaminisha watu kuwa huyu alikuwa na mfano bora wa imani wakati watu wanaona tofauti. Ni kuwapotosha watu. Fanya ibada ya mazishi, mwachie Mungu hukumu yake.
 
Muanzisha hoja umesema ukweli. Wanaokupinga wana ugonjwa wa ukanumba. Kanumba alikuwa mzinzi kama mimi na sote hatustahili kuitwa wacha Mungu. Askofu aliyemsifia kuwa ni mcha Mungu katoka ukoo wa lusuferi. Walaaniwe wote waushabikiao uzinzi na ubakaji kama alivyofanya Kanumba.

umenichekesha saaaaana!
Eeh Mungu kama ungehesabu maovu yetu, nani angesimama!?
 
imeandikwa usihukumu kwani nawe utahukumiwa, kwa kipimo kile kile ulichopimia wenzio nawe utapimiwa hicho hicho.....

Hakuna binadamu msafi, kikubwa ni kumuomba mungu akusamehe.....hatujui kina kanumba na sokoine wakati wa kukata roho kama waliomba msamaha au la, hatujui kama wakiongea na Mungu wao au la......

Kikubwa ni kujitahidi kuishi kama maandiko yasemavyo ....... Kanumba na sokoine walifuata au hawakufuata maandiko...huko muachie Muumba...
 
Back
Top Bottom