Tuacheni ujinga, unafiki na mihemko. Afande Sele aachwe asisumbuliwe kabisa

Kuna clip inaonuesha Sheikh anaomba Sele afe ndani ya siku saba, nimemshangaa sana......sijawahi ona wala kusikia dini inaombea mtu afe hata kama ametenda dhambi gani......
Hebu fikiria huyo Sheikh ndio afe hapo cheo cha ushekhe tutampa Sheikh Afande Sele
 
Unataka mpaka umuone kwa macho yako?
Kwa nini unafikiri hivyo? Kipi kimekufanya uamini hilo mpaka kuuliza swali hili?

Unajua kusoma kwa ufahamu na kufuatilia mantiki?

Mtu anayebishia uwepo wa Mungu kwa kuangalia mantiki na proof by contradiction kwa nini unafikiri anahitaji kumuona Mungu?

Una uwezo wa kufuatilia mantiki?

Kwani nikisema kimantiki ya hesabu square root ya mbili haiwezi kuwa kubwa zaidi ya mbili, ni lazima niione hiyo square root ya mbili?

Unajua kusoma kwa ufahamu?
 
Afande kaomba msamaha na kawaambia mashehe nao waombe msamaha kwa sababu wanampangia Mungu kazi.
Mungu hapangiwi cha kufanya.
Mashehe kwa nini wanataka yeye afe ili awaache watoto wake yatima?
 
Na wengi wanaoshupalia Afande Sele akamatwe wengi wao walikuwa wanakufuru kwa kusifu na kuabudu mtu asiyekuwa Mungu
 
Hata nikiunganishwa, hilo halitathibitisha Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.
Wew jamaa kazi zake huzioni kama bahari,mito watu aina tofauti mazao wanyama majira mbona vitu ni vingi tu kaumba vinaonekana...
 
Wew jamaa kazi zake huzioni kama bahari,mito watu aina tofauti mazao wanyama majira mbona vitu ni vingi tu kaumba vinaonekana...
Unajuaje hivyo vyote ni kazi za Mungu kweli na habari kwamba ni kazi zake si hadithi za kutungwa na watu tu?
 
Katiba inasema kuna uhuru wa kuabudu. Afande Sele alitoa audio moja ambayo haikuwa na maadili au maneno mazuri. Alimtukana mungu.

Kuna watu wanataka ifanya issue.mimi naamini kwa uwezo wake mungu huyo anaweza jipigania. Mungu mkuu hahitaji jeshi la wanadamu kumpa support.

But zaidi sikusikia akimtaja mungu wa mtu yeyote. Why sasa muanze ifanya kuwa ni issue? Ni kukosa kazi,kutokuwa na elimu,kutokuwa na ufahamu na uwezo wa kufikiri.

Yeye anaamini mungu si kitu na ametoa lugha ya kuudhi kwa mungu.wewe unapata wapi ujasiri wa kusema kamtukana mungu wako? Na je mungu akiitwa aje atoe ushahidi ameumizwa kiasi gani na maneno ya afande sele atakuja?

Lakini ikiwa zikapita siku hizo zilizotamkwa na asipokufa je itamanisha huyo mungu hana lolote? Na je akifa ndani ya siku hizo itaaminisha wengine kuwa mungu alichukia?kuna tofauti gani ukagombana na jirani mchawi akasema kesho hufiki na usiku ukafa?je naye ni mungu?

Na sisi tumemkufuru mara ngapi kwa kutenda dhambi ? Afande Sele hajawah kuwa na akili timamu toka miaka mingi imepita wenye akili wala hatuhitaji kuhangaika naye. Zaidi mna m promote tu.

But simuungi mkono kwa lugha chafu aliyotumia. Mimi naamini Mungu wangu ana uwezo mkubwa na atajionesha uwezo wake. Si lazima mpaka afande sele amtambue. Hana haja. Na walio karibu naye wamuase kuacha tumia vitu vinavyomchanganya akili.
Kwanza Kwa nini anaitwa Afande wakati siyo askari? Tukomalie hapo kwanza, hayo ya Mungu mtaendelea wenyewe
 
Kosa la Afande Sele ni kutumia lugha ya matusi na kurusha mitandano basi.

Kila mtu ana uhuru wa kuabudu anachopenda, kama Sele haamini uwepo wa mungu hilo ni swala lake binafsi asiingiliwe.

Kama, kwa hakika, Mungu yupo basi atamuwajibisha mwenyewe badala ya kusaidiwa na wanadamu.

TZ ina atheists (wasio amini uwepo wa mungu) kibao ila wanaogopa kujitokeza sababu ya kushambuliwa na watu badala ya mungu mwenyewe.
 
Back
Top Bottom