Tuache visasi! Tuishi kama Mandela

CHA The GREAT

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
651
853
Kusamehe si jambo rahisi pale inapotokea mtu umetendewa vibaya na mtu fulani. Ila kama huyo aliyetendewa vibaya ni mcha Mungu, hakika kusamehe ni jambo rahisi sana.

Nelson Mandela alifungwa jela miaka 27 na makaburu, ila aliachiwa huru na kuwa Rais wa nchi hiyo yenye nguvu za kiuchumi na kijeshi barani Afrika.

Naweza kusema ucha Mungu wake na kutii maandiko matakatifu, vilipelekea Mandela kuwasamehe wote waliomfunga jela na kumtesa kwa miaka 27. Kama Mandela angekuwa mtu wa visasi (avenger) au angeamua kulipiza visasi dhidi ya wazungu (makaburu) ilikuwa rahisi sana kwa sababu hata watu wake walitamani iwe hivyo na yeye mwenyewe alikuwa ndiye mkuu wa nchi hiyo kama Rais ila hakuona sababu ya kufanya hivyo kwa sababu aliamini, an eye for an eye would make the whole world blind. Aliamini kuwa hata yeye aliwahi kumkosea Mungu siku fulani sehemu fulani ndiyo maana akafuata maandiko matakatifu kwenye Mathayo 6:14...kwamba...'Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa'

[HASHTAG]#TujifunzeKusameheNaTusiishiKwaVisasi[/HASHTAG]

Mandela_Inspire.jpg
 
Kujua Kusamehe inatokana na malezi, na busara!
Wengine kusamehe ni kipaji.
Na wengi wetu hatupendi kujifunza kusamehe!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom