Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,487
Hii idea ya kuhujumiwa mi naikataa kabisa. Hakuna kitu kama hicho. Ni mawazo potofu tu ambayo viongozi wazembe wamefanikiwa kuwapandikizia wananchi ili viongozi hao waendekee kukwepa wajibu wao.
Juzijuzi hapa wamefanikiwa kupandikiza tena "kijana usilalamike tu, toa suluhu". Na sisi tumeidandia hiyo slogan, viongozi wazembe officialy wamefanikiwa ku-justify uzembe wao.
Wewe kiongozi tumekuweka hapo coz umesoma utusaidie kutatua matatizo, halafu unasema 'usilalamike toa suluhu'. Hiyo ofisi tuliyokupa kwa kigezo cha ujuzi wako maana yake ni nini sasa!!! Tungemtafuta std seven leaver tumpe ofisi then wananchi wanakuja na suluhu zao, nchi inakwenda. Cha ajabu, kiongozi anasema wananchi muache kulalamika. Baada ya wiki anakuja tena anasema shirika linahujumiwa. Kasahau alituambia sisi tusilalamike, leo na yeye kaja kulalamika. Halafu analalamika wakati nyenzo zote ziko within his/her reach. Kuna awamu mpaka President alikuwa analalamika pamoja na organs zote ambazo katiba na wanachi tumemuhalalishia. Hii sio sawa kabisa.
Hakuna shirika la uma linalohujumiwa. Serikali ndiyo imeshika hatamu na inaendesha haya mashirika na ina mkono mrefu, inahujumiwaje na mwananchi kwa mfano???. Labda kichwa changu kizito kuelewa. Kitendo cha officer wa ttcl kupewa pesa na kutangaza ticket zimeisha, hiyo haina tofauti na police wa barabarani kuchukua pesa na kuacha bus bovu liendelee na safari. Tofauti ni kwamba officer wa ttcl anakwenda kuuwa shirika, polisi wa barabarani anakwenda kuuwa abiria.
Ni uzembe tu wa haya mashirika na kutokuwa na ubunifu wa kibiashara na utamaduni wa 'kama kawaida' (business as usual).
Hujuma unaonekana ni msamiati mkubwa sana ambao haiwezekani kuudhibiti. Na ukubwa wa huu msamiati ni kutokana na historia kipindi ambacho taifa moja hutafuta njia ya kunyanyuka juu ya taifa jingine. Kwa mwananchi, taifa moja kufanya hujuma dhidi ya taifa jingine, ni swala kubwa sana ambalo mwananchi hawezi kushughulika nalo. Na msamiati wa 'hujuma' ukawa unatumika kwa maswala makubwa ya uzito huo. Viongozi na wanasiasa wazembe wakagundua 'hujuma' ni msamiati mkubwa sana ambao wakijificha nyuma yake, hawataonekana. Basi wakawa wanautumia na kutuaminisha wananchi asa if hujuma ni swala la kumuachia Mungu, liko nje ya uwezo wa sisi sote. Ukichanganya na hujuma za taifa juu ya taifa, ndio kabisa tunaona ni swala zito kabisa. Viongozi waligundua watanzania ukiwaambia ni 'hujuma' huwa hawahoji, ni swala la kumuachia Mungu.
Ndio maana nakataa hakuna shirika lolote la serekali linalohujumiwa.
Mbona kwa huduma mbovu za hospitali za serikali hatusemi hospitali za serikali zinahujumiwa???. Pale kijijini kwenu kata ina zahanati moja tu, nani anahujumu ili zahanati yake binafsi ipate wateja????
Kimsingi, serikali isiyoweza kutoa huduma kwa wananchi wake kwa usahihi kamwe haitoweza kufanya biashara kwa usahihi. Na mzizi wa tatizo hilo ni mmoja, uzembe na mfumo wetu wa kufikiri. Kibaya zaidi viongozi na waliopewa madaraka wanajua jinsi ya kucheza na akili za wananchi.
Watanzania na Afica bado tuna safari ndefu ya kugeuza mitazamo na namna ya kufikiri kulingana na matatizo yanayotukabili.