Tuache utani TTCL hawako serious kwenye biashara ya internet

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,436
17,081
Kwa kweli mimi nimeinua mikono kwa internet ya TTCL. Ni internet ya hovyo sijawahi kuona.

Kuna mtu aliwahi kuandika humu kwamba mshikaji wake anaishi Tabata, anatumia mtandao wa TTCL, akilalia ubavu wa kulia anapata mtandao ila akibadilisha akalala ubavu aa kushoto ama akalala chali hakuna mtandao watu tukafikiri utani, mimi sasa nimeamini.

January mwaka huu nilipewa simu ya ofisi na line TTCL ili kurahisisha shughuli za ofisi, kila mwezi wanaweka salio kubwa tu la kufanyia mawasiliano.

Toka nimeanza kutumia hii laini hasa upande wa internet ni majanga, na mbaya zaidi ofisi zetu ziko mjini city centre lakini TTCL internet yake ni hovyo sijawahi kuona. Unaweza kukaa nusu saa au zaidi haipo kabisa, ila ikija dakika 2 inakuja kwa spidi kali sana kisha inatoweka nusu saa tena.

Muda mwingi mtandao wa TTCL haupatikani. Wakati mwingine natumia simu yangu nyingine kuweka hotpot kuunganisha na hii simu yenye laini ya TTCL ili niwe hewani niendelee kufanya mambo yangu wakati TTCL nina ma GB ya kutosha mengi sana.

TTCL wakileta ile option ya kuhamisha salio la kawaida kwenda mtandao mwingine, hela itakua ikiingia tu naihamishia mtandao mwingine, huu labda voice calls tu ila internet intakufedhehesha tu.

TTCL kuweni serious na business.
 
Mtoto wa kambo siku zote ndio anakuwaga makini sio mtoto real wa mother house! Serikali na biashara wapi na wapi,mi nilikuwaga nayo yaani inaweza goma hata mwezi na ikakataa kabisa hata kusoma Salio,kuingiza Salio network inaweza futika hata masaa manne,hawanaga hasara mwisho wa mwezi mshahara upo na dividend wanatoa kama kawaida

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mtumishi mmoja wa TTCL aliwahi kutuambia wanao iuwa hiyo kampuni ni serikali wenyewe....maana kwenye huduma ya internet wenyewe ndio wanao wauzia mitandao mingine,jiulize sasa kwa nini wao wawe slow halafu wanao uziwa wawe fasta?

-Miaka ya 2013 tulitembelea TTCl makao makuu ya mkoa flani....jamaa wana miundo mbinu ya kufa mtu kwenye upande wa telecom nadhani kwa bongo watakuwa wanaongoza,hadi server za mitandao kama tigo kwa mikoani zilikuwa ndani ya ofisi za TTCL na wachina ndio ma engineer wanaondesha kila kitu.

Hata hiyo njia ya fiber optic mitandao mingine inachukulia TTCL sasa haya madudu yanatoka wapi?

Labda wizara/waziri wa mawasiliano aje atoe ufafanuzi kuhusu upupu huu wa TTCL.
 
Shida ya hilo shirika limejaza wazee. Mzee na internet wapi na wapi

Back
Top Bottom