The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,449
- 17,148
Kwa kweli mimi nimeinua mikono kwa internet ya TTCL. Ni internet ya hovyo sijawahi kuona.
Kuna mtu aliwahi kuandika humu kwamba mshikaji wake anaishi Tabata, anatumia mtandao wa TTCL, akilalia ubavu wa kulia anapata mtandao ila akibadilisha akalala ubavu aa kushoto ama akalala chali hakuna mtandao watu tukafikiri utani, mimi sasa nimeamini.
January mwaka huu nilipewa simu ya ofisi na line TTCL ili kurahisisha shughuli za ofisi, kila mwezi wanaweka salio kubwa tu la kufanyia mawasiliano.
Toka nimeanza kutumia hii laini hasa upande wa internet ni majanga, na mbaya zaidi ofisi zetu ziko mjini city centre lakini TTCL internet yake ni hovyo sijawahi kuona. Unaweza kukaa nusu saa au zaidi haipo kabisa, ila ikija dakika 2 inakuja kwa spidi kali sana kisha inatoweka nusu saa tena.
Muda mwingi mtandao wa TTCL haupatikani. Wakati mwingine natumia simu yangu nyingine kuweka hotpot kuunganisha na hii simu yenye laini ya TTCL ili niwe hewani niendelee kufanya mambo yangu wakati TTCL nina ma GB ya kutosha mengi sana.
TTCL wakileta ile option ya kuhamisha salio la kawaida kwenda mtandao mwingine, hela itakua ikiingia tu naihamishia mtandao mwingine, huu labda voice calls tu ila internet intakufedhehesha tu.
TTCL kuweni serious na business.