Tuache utani: Tanga sio ngome ya CUF, kwa afya ya UKAWA

SHILLINGS

Senior Member
Oct 24, 2013
160
648
Ipo dhana iliojengeka kwamba mkoa wa Tanga kwa upande wa vyama vya upinzani ni ngome ya CUF hivyo dhana hii kushindwa kukidhi mahitaji chanya ya kuikomboa Tanga kwenye makucha ya kinyonyaji ya Chama Cha Mapinduzi kuelekea uchaguzi mkuu.Dhana hii inapingana na matokeo ya uraisi ya 2010, matokeo ya uchaguzi wa Rais 2010 Mkoa wa Tanga kwa vyama chama cha CUF na CHADEMA ni kama ifuatavyo:

1. Tanga Mjini
CHADEMA:7,353
CUF:20,188

2.Mji wa Korogwe
CHADEMA: 3,135
CUF: 394

3.Wilaya ya Handeni
CHADEMA: 4,453
CUF: 3,939

4.Wilaya ya Kilindi
CHADEMA:1,788
CUF: 458

5.Korogwe Vijijini
CHADEMA:4,201
CUF:2,067

6. Bumbuli
CHADEMA: 1,674
CUF: 733

7. Lushoto
CHADEMA:1,910
CUF:1,515

8. Mlalo
CHADEMA: 2,268
CUF: 1,559

9.Muheza
CHADEMA:4,611
CUF: 3,991

10.Pangani
CHADEMA: 856
CUF: 3,253

11. Mkinga
CHADEMA: 1,083
CUF: 6,480

Kwa matokeo haya ni dhahiri CUF ina nguvu kwa baadhi ya maeneo ya Tanga (Tanga Mjini,Mkinga na Pangani) na sio Tanga nzima (kama mkoa) hivyo combined effort ya CHADEMA na CUF kuanzia ngazi ya kitaifa inahitajika haraka wakati zoezi la BVR litakapoanza tarehe 18.06.2015.

Ikumbukwe pamoja na CHADEMA kuongoza kwenye majimbo kama Bumbuli, Lushoto, Kilindi na Mlalo kampeni za mgombea wa uraisi haikufika kwenye maeneo hayo.Tanga ina mila na desturi tofauti kulingana na maeneo na tofauti za mapokeo ya kisiasa.Hivyo tutarajie matokeo makubwa jitihada za makuaudi zikifanyika katika kipindi kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu.

UKAWA SAFARI YA UHAKIKA,MAAMUZI SAHIHI,KWA WAKATI SAHIHI.MABADILIKO NI LAZIMA.
 
Sasa mbona unajiumbua mwenyewe!

Ukijulisha hizo kura zote za mkoa mzima, mbona CUF anamucha chadema kwa mbali sana tu!

Kwahiyo ktk overall Tanga ni ngome ya CUF !
 
Ebu weka na za CCM hapo ili tuone kwa kuungana kuna gap gani zinapungua
 
Content imekaa vizuri ila tittle naona kama imekaa kishari fulani hivi. Naungana na wewe kuwa UKAWA ndio suluhisho la kumaliza tatizo la kugawana kura miongoni mwa wapinzani
 
Sasa mbona unajiumbua mwenyewe!

Ukijulisha hizo kura zote za mkoa mzima, mbona CUF anamucha chadema kwa mbali sana tu!

Kwahiyo ktk overall Tanga ni ngome ya CUF !

Ni kweli kwamba overall CUF ipo juu lakini ni ukweli usiopingingika tunahitaji wastani mzuri wa asilimia kwa kila jimbo dhidi ya CCM.

Tukiacha Tanga Mjini,Pangani na Mkinga ambapo CUF inakubalika kwa asilimia kubwa,tunahitaji kuongeza kura za UKAWA kutoka majimbo yote kupata wastani mzuri wa kura dhidi ya CCM hivyo combined effort ya UKAWA inahitajika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom