#COVID19 Tuache upotoshaji kutumia dini kupinga chanjo ya COVID-19

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,980
4,075
Soma hii kwa kumaanisha

Tanzania tunachanjo 15 ikiwemo hii tunayoikimbia zote ni za mabeberu,Wameshindwa kukuua kirahisi ukiwa Mchanga leo umepata akili ndio unamkimbia nyoka uliyelalanae mpaka unataka kuvunja mguu,Acha ushamba Wahi chanjo ziko chache usisahau maisha ni yako.

Corona sio mpya,Mpya ni huyu Upotoshaji, Corona imekuwepo tangu mwaka 1918 ni zaidi ya miaka 100 sasa, wanaosema huu ugonjwa ni wa mpiganga kristo Wakasome historia ya Corona imekuwapo kabla ya kuwapo UKIMWI mwaka 1920,Wahi Chanjo ziko chache usisahau maisha ni yako.

Kama unazini,Unasema uongo, Unakula rushwa, Unaiba, Unatukana hovyo, Unatembea na wake|waume za watu wewe tayari ni mpinga kristo|Mtume sasa huyo wakwenye chanjo ni mpinga kristu|Mtume yupi unayemkimbia? usipotoshwe Mungu wetu anaweza kujitetea mwenyewe nenda kachanjwe Chanjo ni chache maisha ni yako.

Biblia na Koroani tukufu tunazozitumia kupinga Chanjo za Corona toka kwa Mabeberu zimetoka kwa Mabeberu kama Mkuu wa Roma amechanjwa na U.A.E alikozaliwa Mtume zaidi ya 80% wamechanjwa wewe ni nani au, Je sisi ni zaidi ya wamarekani 165M waliopata chanjo au wachinina 223M waliochanjwa? acheni mzaha Corona inaua Siasa wekeni pembeni maisha ya watu ni zaidi ya hizi Siasa zenu , Wahi chanjo ni chache na maisha ni yako.

Hayati Rais Magufuli kwenye nyungu alikuwa sawa na Mama Samia kwenye Chanjo yuko sawa tofauti ni muda na hatua za Corona,Hii corona ya sasa ni kali na inastukiza,Waliochanjwa maambukizi yamepungua sana someni (google) kila kitu kiko wazi,Wahi kachanjwe chanjo ni chache tuko wengi usisahau maisha ni yako.

Ufanisi( effectiness) wa chanjo ya Corona ni Kati ya 80% na 100% ukichanjwa kupata Corona ni bahati mbaya sana, Heri nusu shali kuliko Shari kamili,Jihakikishie uhai kwa zaidi ya 80-100%,wahi kachanjwe chanjo ni chache usisahau maisha ni yako.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom