Tuache uongo, jela zina kila aina ya watu, nimejionea na kupewa maelezo

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,895
22,659
Ukiwa JamiiForums unaweza kudhani jela za Tanzania zimejaa wamasiasa wa upinzani na wanaharakati wanaopinga Serikali tu kumbe uongo mtupu hawazidi hata 1% ya wafungwa wote ambao hukadiliwa kuwa 36000 hivi nchi nzima .

Leo nilikuwa Segerea kwa shughuli za kawaida nimeona kuna walimu,wajasiriamali,wanajeshi,polisi,wakristo,waislamu,wahindi,wachina,watu wa Ethiopia na Somalia,wastaafu askari magereza,madereva,waadishi wa habari, viongozi wa dini zote, kila aina na kuhakikishiwa hali ipo hivyo Ukonga na jela nyingine nchini. Kiufupi nimeona aina zote za watu humu as sample of all jail

Walioko jela wanawashangaa kusikia eti mtu mmoja hasa wenye majina makubwa anaonewa huruma na jamii bila kujua ukweli kisa anajulikana maana wao wapo kula hakuna anayewapigia kelele waachiwe , kama ni mwanasiasa amekosea acheni aande jela kama ni mwanahabari,mtumishi wa umma au mkulima mwacheni akae jela huko wako kila watu na ndio maana ya jela.

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo ulienda jela kufanya interview na wafungwa maana unasema eti wanataka watu wawalilie wote sio mtu mmoja ambaye ni mwanasiasa.

Kwanza ungewahoji kama wako jela kwa kuonewa au kihalali

Pili hao wanasiasa walioko jela umewahoji wamesema wamefungwa kwa kuonewa au kwa haki?

Ikiwa watu tumetofautiana hadhi na power katika jamii.Wanasiasa ni watu maarufu na wanajulikana.Kwako unaona sawa wanasiasa 1%walioko jela kwa sababu zisizo na maana za uonevu.

Kisha hapo unaona unamtetea magufuli au unamchonganisha.Polepole awe anawafundisha namna ya kujenga hoja angalau miongoni mwa mwenye akili kama sisi.
 
Hayo mambo mara nyingi husukumwa na mihemko ya kisiasa... Kwamba gereza limejaa watu wa namna hii.... Na kumbe kule kuna watu wa aina zote.
 
Kwa hiyo ulienda jela kufanya interview na wafungwa maana unasema eti wanataka watu wawalilie wote sio mtu mmoja ambaye ni mwanasiasa.
Kwanza ungewahoji kama wako jela kwa kuonewa au kihalali
Pili hao wanasiasa walioko jela umewahoji wamesema wamefungwa kwa kuonewa au kwa haki?
Ikiwa watu tumetofautiana hadhi na power katika jamii.Wanasiasa ni watu maarufu na wanajulikana.Kwako unaona sawa wanasiasa 1%walioko jela kwa sababu zisizo na maana za uonevu.

Kisha hapo unaona unamtetea magufuli au unamchonganisha.Polepole awe anawafundisha namna ya kujenga hoja angalau miongoni mwa mwenye akili kama sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jela kila mtu anafika na kuona wafungwa hata wewe nenda na ulete mrejesho hapa

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom