Tuache ung’ang’anizi................. ..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
shutterstock_53154142.jpg

Huwa tunashuhudia vituko vingi vinavyotokana na uhusiano au ndoa. Hebu fikiria kwamba umemchoka mpenzi wako na unamwambia au kumwonyesha kwamba, humtaki tena, wakati yeye anahisi na kuamini kwamba, bado anakutaka.

Kwa kuona mwenzako anakutaka bado wakati wewe humtaki, unaanza kufanya visa. Hebu chukulia kwamba, unamwambia huyo mwenzako kwamba, una mwanamke mwingine, au unajidai kumuomba radhi kwamba, umefanya mapenzi nje, juzi au jana ili akasirike na kuondoka, lakini yeye hajali na ndiyo kwanza anajaribu kuhalalisha kitendo chako hicho na kukuhakikishia kwamba amekusamehe. “hamna shida mume wangu mpenzi nimekusamehe, najua ni shetani amekupitia tu, kwani sio tabia yako kabisa kunisaliti….” Atasema hivyo akimtetea mume mzinifu.
confront.png

Unadhani utafanyaje?

Kumbuka kwamba, kuna watu wengi sana ambao huwafanyia visa wapenzi wao ili wachoke na kukereka sana na hatimaye kuamua kuondoka. Kuna wakati visa hivyo hufanikiwa na kuna wakati hugonga ukuta kwani mpenzi anakuwa havijali. Hebu tujiulize kwa dhati, inasaidia nini kama tumechokwa na sisi kuendelea kung’ang’ania kwa wale tunaowaita wapenzi wetu. Kuna wakati wanaume au wanawake huamua kuwauwa wapenzi wao ili kuwa huru kutoka kwao. Wanaambiwa kwa kauli, “sikutaki,” halafu wananza kufanyiwa visa, lakini wamo tu, hawataki kuondoka. Hatimaye, mtu anaamua kuuwa kabisa.
street-hollas-401x450.jpg

Kuna wakati mpenzi anaambiwa kabisa na mwenzake kwamba hatakiwi, lakini yeye anasema, “tutabanana humu humu hatoki mtu hapa.” Bila shaka hiki ni kichaa cha aina fulani. Mtu akishasema sikutaki, maana yake hakuna tena kinachoweza kuwaunganisha, yaani hisia za upendo. Kulazimisha kuishi na mtu asiyekutaka ni kujifanya mtumwa bila sababu. Inabidi tuamke na kuwa sisi kamili kabisa.

Ndoa za Kiislamu zina uzuri mmoja….. mke au mume akimwambia mwenzake sikupendi au sikutaki tayari ndoa hiyo inahesabika kuwa batili. Bila shaka huu ndio ukweli ambao inabidi tuukubali kwa mkabala wa hisia na tabia za binadamu. Kulazimisha kuishi na mtu asiyekupenda ni kujiingiza matatizoni……………
 
mmnnhhh, haya ngoja tufuate ya wazungu haya ambayo labda wao wanatamani kuwa huku tuliko ila hawajui walipotelea wapi.

Kuachana achana kuna raha gani lakini???
Tuna watoto 7, tuachane kisa tumechokana miezi 6, kweli??

Vishengele vya mapenzi vipo tu but with time huwa vinapita.
 
mmnnhhh, haya ngoja tufuate ya wazungu haya ambayo labda wao wanatamani kuwa huku tuliko ila hawajui walipotelea wapi.

Kuachana achana kuna raha gani lakini???
Tuna watoto 7, tuachane kisa tumechokana miezi 6, kweli??

Vishengele vya mapenzi vipo tu but with time huwa vinapita.

Subiri mpaka uwekewe sumu ya panya, ndio utatia akili............. ujinga ukutoke.
 
Nilishawahi kumuacha binti kwa namna hii nilikoma..
Kukatisha mapenzi ya mtu kwako inataka moyo sana kwa sababu moyo wa kupenda haupoi haraka..
Inawezekana ukawa unafanya vitimbi mwenzio anakusamehe tu!!!
 
"Kuna wakati mpenzi anaambiwa kabisa na mwenzake kwamba hatakiwi, lakini yeye anasema, "tutabanana humu humu hatoki mtu hapa." Bila shaka hiki ni kichaa cha aina fulani"

Hata me huwa nahisi wamepungiwa.


 
Nilishawahi kumuacha binti kwa namna hii nilikoma..
Kukatisha mapenzi ya mtu kwako inataka moyo sana kwa sababu moyo wa kupenda haupoi haraka..
Inawezekana ukawa unafanya vitimbi mwenzio anakusamehe tu!!!



Bila shaka ulimwambia hana sifa za kuwa nawe. Kiukweli unatamani ungendelea kuwa nae Na ukikutana nae lazima umtake tena
 
Hebu someni kituko hiki cha jamaa aliyetaka kumuacha mke king'ang'anizi................

Florida nchini Marekani mtu mmoja ambaye anaonekana alimchoka mkewe kupindukia na pengine kila visa alivyomfanyia kugonga ukuta, aliamua kufanya kisa ambacho kiliacha gumzo. Mtu huyo baada ya kuona mkewe anajifanya anajua sana kupenda na hivyo kutojali visa vyake aliamua kufanya kisa kikubwa zaidi.

mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Teddy Akin alimwambia mkewe kwamba amemuuwa mtu ambaye alimuomba lifti na kumzika porini. mume huyo alitoa pochi na kumwonyesha mkewe akimwambia kwamba, baada ya kumuua mtu huyo alichukua pochi yake. ni kweli pochi hiyo ilikuwa ni ya mtu fulani na ilikuwa na vitambulisho vyake na nyaraka nyingine pamoja na pesa. bila shaka alimwambia mkewe kwamba, yeye (mume) kuuwa kwake ni kawaida akiamua.

Kuona hivyo mke wa jamaa aliripoti kwa Polisi ambao walifika na kumtia mikononi Teddy Akin. hata alipofikishwa polisi bado aliendelea kusisitiza kwamba alimuuwa mwenye pochi ile na kuichukua. hii yote ikiwa ni juhudi yake kumfanya mkewe yule king'ang'anizi ajue na kuamini kuwa anang'ang'ania muuaji.

alisema bele ya Polisi na mkewe kwamba, alimuuwa mtu huyo kwa kumpiga kiswasawa shingoni na kwamba baada ya kufanya hivyo, mtu huyo kabla hajafa alivutia roho kwa kutisha na kutoa sauti yenye kugumia vibaya. Alisema yote hayo ili kumtisha mkewe aone kwamba, yeye ni muuaji hasa, ili mke huyo afanye uamuzi wa kuondoka amwache huru.

Lakini kabla kesi hiyo haijapelekwa mahakamani, polisi walibaini kwamba, mtu aliyedaiwa kuuawa na jamaa huyo alikuwa salama na mzima wa afya. mtu huyo alipopewa taarifa kwamba alikuwa ameuawa alishangaa sana. Aliwaambia polisi kwamba, pochi yake ilikuwa imeibwa siku mbili tatu nyuma..............

Polisi walipomhoji Teddy sababu ya kufanya hivyo alidai kwamba baada ya kuokota pochi ya mtu huyo aliamua kufanya jaribio hilo ili kumtisha mkewe kwamba yeye ni muuaji hatari ili mke huyo aondoke, baada ya mbinu kadhaa kushindwa kufanya kazi. polisi walishindwa kumuelewa, wakamwambia mkondo wa sheria utafuata njia yake................
 
Eeeh.... Makuubwa haya... Sasa hivi vitimbi ninavyofanyiwa inawezekana nami sitakiwi lakini nimeng'ang'ania tuu... Mmmh... Baba Ngina asante kwa kunifumbua macho.. Ngoja nitafute ustaarabu mapema nisije wekewa sumu..
 
Eeeh.... Makuubwa haya... Sasa hivi vitimbi ninavyofanyiwa inawezekana nami sitakiwi lakini nimeng'ang'ania tuu... Mmmh... Baba Ngina asante kwa kunifumbua macho.. Ngoja nitafute ustaarabu mapema nisije wekewa sumu..

acha king'ang'anizi cha kukesha lol
kalale now lol
 
Teh teh teh, aisee mi ni mmoja wao, mi huwa kauli ya "akufukuzae hakwambii toka" haifui dafu kwangu, mpaka mtu anichanie makavu laivu ndio najitoa...............

anyway huwa napenda kumuudh anayejarib kuniudh kwa kumpotezea...............,
 
Wakati mwingine si kwamba watu hawaondoki kwa kuwa ni vichaa au ving'ang'anizi...ila wanachukulia kama njia ya kulipiza kisasi...ku make your life a living hell. Kuna wanaobaki lakini wewe unarudi saa nane yeye anarudi saa kumi...na anakwambia ataondoka akipenda yeye si kwa kufukuzwa...unacheza.

Hivyo si kila anayebaki ni weak...wengine ni kinyume chake..wababe.
 
Wakati mwingine si kwamba watu hawaondoki kwa kuwa ni vichaa au ving'ang'anizi...ila wanachukulia kama njia ya kulipiza kisasi...ku make your life a living hell. Kuna wanaobaki lakini wewe unarudi saa nane yeye anarudi saa kumi...na anakwambia ataondoka akipenda yeye si kwa kufukuzwa...unacheza.

Hivyo si kila anayebaki ni weak...wengine ni kinyume chake..wababe.

ikifika hapo ndo inanoga zaidi!sio kila ukiambiwa toka unatoka?unakomaa na akili mukichwa!
 
mmnnhhh, haya ngoja
tufuate ya wazungu haya ambayo labda wao wanatamani kuwa huku tuliko ila
hawajui walipotelea wapi.

Kuachana achana kuna raha gani lakini???
Tuna watoto 7, tuachane kisa tumechokana miezi 6, kweli??

Vishengele vya mapenzi vipo tu but with time huwa vinapita.

vishengele?umenikumbusha mbali
 
Kiukweli mimi binafsi nawa-admire sana ving'ang'anizi, hasa wale ambao tayari wako kwenye ndoa.
Sio mtu umehangaika weee kwa kushirikiana na mwenzio kutafuta maisha, pengine Mungu amewajalia mmepata kijumba chenu ama kigari chenu halafu ghafla unaambiwa umechokwa na kutakiwa kusepa ili mwingine aje kuponda raha, hapo ni pagumu sana.

Kuna dada mmoja jirani yangu kwakweli amenifanya niwapende ving'ang'anizi. Mume wake ni dereva wizara ya nishati na wameishi kwenye ndoa zaidi ya miaka 10. Yule dada alikuwa mama wa nyumbani lakini akawa mchakarikaji akaanza biashara ya genge hadi wakafanikiwa kununua kiwanja na wakajenga nyumba. Baada ya muda mumewe akaanza vitimbi, si vya kuchelewa kurudi nyumbani tu bali na kipigo juu. Kama hiyo haitoshi jamaa akaamua kuleta na mwanamke hapo nyumbani.

Yule dada alikomaa nao hadi mume akanyoosha mikono na kuhama nyumba. Mambo aliyoyafanya ni magumu hata kuyaandika hapa kwani binafsi sijapata kuyashuhudia. Sasahivi anaishi kwa raha mustarehe ndani ya nyumba yake na maisha yanaendelea.
Kwahiyo akina dada msiwe wepesi wa ku-give up, uking'ang'anizi unalipa wakati mwingine.
 
Babu, nadhani hapa inategemea unag'ang'ania katika mazingira ya namna gani - kama ni singo au tayari mpo ndani ya ndoa!!!
 
Back
Top Bottom