CCM original
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 373
- 68
Mimi ni mwajiri wa Dr. John Pombe Magufuli, nimemwajiri kunitumikia, alete maendeleo kwangu na kwa taifa zima.
Nitakuza kichaa endapo nitaacha kumshauri, kumsema na hata kumkosoa pale anapokosea. Ni ajabu mtu nimemwajiri halafu nisimseme, kumkosoa na kumshauri.
Naona kwa sasa umezuka mchezo wa kumfanya mh. Rais ajione yuko sahihi kwa kila jambo. Na mtu anayetazama kwa mbali kuonekana mhaini, mbaguzi, mwongo, ana inda, ana uchama, ukanda nk.
Kwa hapa niko tofauti na chama changu, chama cha Mapinduzi.
Mbona Kikwete hakulindwa kwa nguvu hizi? Tena hata yeye alikuwa anaona anavyotukanwa, lakini akaruhusu watu waoneshe hasira zao ili ajue wapi kakosea.
Mh. Rais ana kasi nzuri, ya kutia matumaini, ila wanaotofautiana mawazo ktk mambo flani huenda hata kutoa lugha isiyofaa, utumike utashi wa kisiasa, waachwe watapike hasira zao. Hapo tutakuwa tunaona wapi anakosea nasi kama wanachama wa chama cha Mapinduzi kumshauri mh. Rais.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi!!