Tuache siasa uzalishaji wa makaa ya mawe ni tani elfu 35 na mahitaji ni zaidi ya elfu 71 kwa mwezi

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,867
Data hizo sasa tujadiliane nini kifanyike?

1. Yawezekana kampuni za uchimbaji zimepewa mgodi kirafiki hawana vifaa vya uchimbaji.
2. Hatuna wataalamu wa kuendesha sekta ya madini.
3. Gharama kubwa ya uchimbaji
IMG_20161212_051305.jpg
 
Data hizo sasa tujadiliane nini kifanyike?

1. Yawezekana kampuni za uchimbaji zimepewa mgodi kirafiki hawana vifaa vya uchimbaji.
2. Hatuna wataalamu wa kuendesha sekta ya madini.
3. Gharama kubwa ya uchimbajiView attachment 445180
Sasa hapo hatutakiwi kulialia.
Kwa style hii undertaker hutapata maendeleo kamwe...hata ya binafsi.
Hii ni changamoto yenye fursa kibao.
Umepata soko zaidi wa uwezo wako lakini raslimali ipo.
Ongeza uzalishaji...
ongeza raslimali fedha na raslimali watu,
funga mitambo ya kisasa, weka mikakati ya muda mfupi na mrefu ya kuongeza kiwango na ubora wa uzalishaji.
Fungua ajira,
Kuza uchumi.

Sasa Mungu akupe nini. Gunia la chawa...yaani unapata soko la bidhaa yako afu unabweteka na kulialia????
Unataka kuacha??
Changamoto ni fursa....tena fursa kubwa.
 
Nilitegemea useme kiasi tulicho nacho cha makaa ya mawe ni kidogo kuliko mahitaji !!?
Magazeti mengine ni yakupita wima tu
Uandishi wa kupinga,kubeza na kuzusha wao ndio kazi yao.

Nisuala la kuongeza uzalishaji kulingana na ongezeko la mahitaji
 
Hiyo ishu bado haijawa solved
I solve....
Hicho ndo kinatakiwa sio kuchulia tu na kubeza....
Ndo nyie mnapewa mkate unabeza, unapewa ugali unabeza, unapewa pilau unatukana matusi...
Hakuna kitu kinafit kila kitu...
Toa jasho, chemsha bongo, tunisha msuli...tatua changamoto...piga mzigo wa ukweli...
akili kama za dizaini hii ndo hukimbia hata familia wakati wa shida.
Yaani wakishindwa kuongeza uzalishaji kukidhi mahitaji ya hiki kiwanda kimoja nitawananihii....
 
Kuna umbali mkubwa kutoka sehemu makaa ya mawe yanapochimbwa na yanapopakiwa.
Kampuni haina vifaa vya kisasa vya kusafirisha hayo makaa ya mawe kutoka sehemu yanapochimbwa mpaka yanapopakiwa.
 
Hivi yule mzee alishanyanganywa ule mgodi wa makaa ya mawe yeye na mkewe?

Tanzania ya viwanda haitawezekana kamwe,sasa ni wazi kwamba hata wakuu wameshindwa kulitolea maamuzi ya haraka suala la nishati,nilitaraji mkuu mwenyewe atoe wiki moja au mwezi dangote awe kafikishiwa gesi kwenye kiwanda chake ambacho kiko kilomita mbili tu kutoka gesi inapozalishwa.

Kasi iliyotumika kwenye mambo mengine kama utumbuaji mbona haionekani huku?
mbona jambo dogo tu kuagiza gesi ipelekwe? au ule.mgodi wa makaa ni wa nani?
 
Nilisikia shida ya mgodi wa makaa ya mawe ni wawekezaji waliopo production yao ni ndogo sana na unakuta maroli yameenda kuchukua makaa ya mawe km ya dangote maroli kumi kwa wiki nzima yanarudi 3 na kiwanda kinaitaji tani za kutosha kwa siku ndio maana dangote aliamua aanze kuagiza makaa ya mawe kwa madiba.ila magu alichunguze na hili huyu mwekezaji wa huu mgodi mahitaji yamekuwa makubwa je ataweza km awezi asepe wapewe wanaoweza kuchimba zaidi ya tani laki moja kwa mwezi na tuuze nje ya nchi.
 
Hivi Kelele hizi zoote ni dangote Tu ?anatekeleza nchi ya viwanda! Jifunze zoez la nyani kulinda shamba!mkigeuka huku wamemaliza
 
Nilitegemea useme kiasi tulicho nacho cha makaa ya mawe ni kidogo kuliko mahitaji !!?
Magazeti mengine ni yakupita wima tu
Uandishi wa kupinga,kubeza na kuzusha wao ndio kazi yao.

Nisuala la kuongeza uzalishaji kulingana na ongezeko la mahitaji
Nini mantiki ya kuzuia uagizaji makaa Africa Kusini kabla uzalishaji kuongezeka? A case of putting the cart before the horse.
 
Kuna umbali mkubwa kutoka sehemu makaa ya mawe yanapochimbwa na yanapopakiwa.
Kampuni haina vifaa vya kisasa vya kusafirisha hayo makaa ya mawe kutoka sehemu yanapochimbwa mpaka yanapopakiwa.
cha ajabu gesi iko kilometa mbili tu kutoka kiwanda cha dangote!
ingeweza kusogezwa tu ndani ya mwezi mmoja!

nani mmiliki wa mgodi wa makaa?
 
Hv nani wamemilikishwa huu mgodi inawezekan. Kuna maslai binafsi ya watu kuna lile sakata la kiwira liliishia wapi kuhusu watu flani kujimilikisha huo mgodi wa makaa ya mawe...........
 
Wachimbaji wasingeweza kuendelea kuchimba makaa mengi bila ya kuwa na wateja wa uhakika,uwezo upo na vifaa vipo,tatizo lilikuwa ni wateja wa uhakika.Si unajua maswala ya operating costs!Sasa zimekuja gari 600 kwa ajili ya kusomba ndio utagundua kuwa uwezo upo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom