GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Wanabodi, Sukari inapopanda bei ni jambo la heri kwa upande wa kiafya, hii sukari ya madukani au artificial ina madhara makubwa sana kiafya.
Watu ni wagonjwa wa kisukari lakini kutokana na uraibu wa vitu vyenye sukari kuacha inakuwa ngumu.
Leo hii magonjwa yasiyoambukiza kama presha na kisukari ni Janga la kitaifa. Serikali ilijaribu kuanzisha mazoezi sio kwa kupenda bali gharama za tiba kwa magonjwa haya zimeongezeka mara dufu.
Tusiendekeze kila kitu tunachopika kujaza sukari, Tujifunze kupunguza baadhi ya vitu.
Ni mambo ya kusikitisha familia ya watu wanne au watatu wanamaliza mfuko wa sukari kwa siku moja kupikia keki, maandazi na kunywa chai, hii familia itakuwa na afya?
Wakati huu sukari inapopanda bei tushukuru izidi kupanda bei zaidi, Mazoezi watu hawafanyi kupunguza kiasi cha sukari mwilini bali wanahitaji sukari iongezeke mwilini.
Wale watu wa kati na wa chini wanaotumia bima za afya ya Taifa, Kuna madawa ya haya magonjwa yameondolewa kwenye listi inakupasa ujinunulie mwenyewe.
Chukua hatua, chukua tahadhari, Jikinge na magonjwa yasiyoambukiza kisukari na Presha.
Povu linaruhusiwa kwa watu wenye uraibu na sukari bila sukari wao hawawezi kuishi.