Tuache Siasa, Riba ya Mabenki ya biashara kukopesha Raia ni suala la Vihatarishi na sio maamuzi ya Serikali

Yes Data zilipikwa sana wakati ule, Na sisi ndio tuliokuwa tunaeneza Propaganda Uchumi unakua na Ajira kedekede huku tukifahamu mambo magumu, Tulifahamu vijana wana hali mbaya na elimu wanayopewa haipo OK kupambana na mazingira ya teknolojia

Siasa ni tofauti na uhalisia, Siasa zinaendeshwa na watu wenye nguvu, Kama unapenda kuishi lazima uchague upande wenye usalama na maslahi

Wale wabunge unaowaona sio wote pale wapo kusimamia story za majimbo, Wengine ni chambo wa kusukuma agenda za wafanyabiashara na agenda za mtawala husika kwa wakati huo,

Umeambiwa Nenda kasifie tozo zina leta Maendeleo utampinga aliyekutuma, Hata wewe utajisikiaje mwanao Unamwambia aseme Baba na Mama wanafaa Yeye akasema hawafai, Lazima achague kuhama nyumba au aunge mkono

Unaamini shule za Private zinazidiwa elimu na shule za kata? Propaganda za kutaka watu wa amini shule za kata zina elimu bora

Je? Kuna mtoto wa wanasiasa na mawaziri wanasoma shule za kata

Propaganda Propaganda na hii ni kazi ngumu na hatari sana

Angalia Waziri wa afya na Gwajima yanayotokea sasa, Waziri wa afya alifanya Propaganda ya Covid wakati ule, Asingefanya ingekula kwake, Leo amegeuka. Ndio siasa lazima uchague upande

Tulisema na kupiga kelele kutetea maslahi na nilishaomba msamaha hapa JF

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana Mkuu 🤣 🤣 🤣 -Nimekuelewa
 
Ebu fafanua, inakuaje BOT wakubali kushusha rates zao kwa ma bank ila bank bado waone kwao hailipi ? Riba za Tz kiukweli ki kubwa sana, utakuta mtu amepigwa riba ya 18 % tena non reducing rate, after 5 yrs huyu ni kama amelipa 90% riba, sasa huu si wizi .
Ukisoma point No 1 na No 2 ya mleta UZI ndio utapata jibu la swali ulilouliza mkuu.
 
Mkuu usiongelee porojo-Be specific kwendana na policy requirements manake naona unazunguka zunguka tu,Hapa tunaongelea legal issues.
Mkuu hiyo sio mara ya kwanza kutokea au Serikali kufanya hivyo, Sera nyingi sana serikali imezifanya, Hiyo sera sio mara ya kwanza

TIB zamani mbona hayo yalifanyika na vigezo kibao mwisho wa siku Bank ikagawanywa, Biashara sio sera, Biashara ni kazi kazi na kuangalia faida basi

Unakumbuka mabilioni ya kikwete wakati anaingia madarakani yalipelekwa NMB Bank wakopeshe watu

NMB ilizipokea hizo billions za kikwete na kukopesha watu kama njugu kama serikali ilivyotaka,

Mwisho wa siku unafahamu Kilichotokea kwenye hizo pesa za bure za serikali kwenda NMB

Hizo pesa sio sustainable kwa Bank
Bank inatakiwa iwe na Customer Strong Deposit na sio hizo temporarily Injections za BOT

BoT kuna muda inasaidia Mabenki sana lakini wakiona wanawapa msaada bado wanashindwa ku mobilize Customer deposit wanaamua kufunga Bank husika

Achana na Siasa, Hizo pesa zinaweza pelekwa huko lakini hazitazaa matunda yeyote

Je Bank ya wakulima kwanini wanapambana si wana mtaji wa serikali na Serikali ina inject pesa huko, Hapa Bank lazima ijipange kutengeneza Strong Deposit Base na Strong Credit rating ya kutoa mikopo

Lini hizo policy zilifanya kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna Jambo ambalo muandika mada hulielewi hapa,
BOT kwenye hii policy mpya anatoa punguzo la riba kwa mabenki yatayokopa BOT kwa kukubaliana na hii policy maalum.Mabenki ambayo yatakubaliana na Policy hii maalum ya BOT yatapaswa kisheria kushusha riba chini ya 10% kwa lazima.Benki zitakazokubaliana na masharti ya BOT watapewa motisha mbalimbali ikiwemo kupunguziwa reserve ratio requirement and etc.Benki itakapokubaliana na kupokea hii financing kutoka kwenye hiyo basket ya 1Trillion itafungwa kisheria automatically kushusha riba kwa lazima kwendana na requirement za policy.
Kingine, hii relif hii ilitolewa kwenye mikopo ya kilimo hasa. Kama rate ya kukopesha kwenye kilimo ni ndogo sana relief ya BOT huipati.
 
Wachumi wanatuambia kazi mojawapo ya bot ni kusimamia kiwango cha Riba kisiyumbe au kutetereka na kiwe kidogo kadri inavyowezekana.
Na kwa namna hio inakuza kasi ya ukuaji wa uchumi
 
Kuna Jambo ambalo muandika mada hulielewi hapa,
BOT kwenye hii policy mpya anatoa punguzo la riba kwa mabenki yatayokopa BOT kwa kukubaliana na hii policy maalum.Mabenki ambayo yatakubaliana na Policy hii maalum ya BOT yatapaswa kisheria kushusha riba chini ya 10% kwa lazima.Benki zitakazokubaliana na masharti ya BOT watapewa motisha mbalimbali ikiwemo kupunguziwa reserve ratio requirement and etc.Benki itakapokubaliana na kupokea hii financing kutoka kwenye hiyo basket ya 1Trillion itafungwa kisheria automatically kushusha riba kwa lazima kwendana na requirement za policy.
Ujumbe uliotolewa na B.O.T ndio huu ulioandika hapa,pia umeskip kipengele kimoja muhimu sana kulingana na maelezo ya B.O.T hizo bank ambazo wataingia makubaliana inatakiwa mikopo itolewe kwenye shughuli za kilimo na sio vinginevyo
 
Siyo kilimo pekee Mkuu, ingawa kilimo ni one of the priority sectors
 
Siyo kilimo pekee Mkuu, ingawa kilimo ni one of the priority sectors
"Kuanzishwa kwa mfuko maalum wa kukopesha mabenki na taasisi za fedha ili ziweze kukopesha sekta binafsi. Benki Kuu imeanzisha mfuko maalum wenye thamani ya shilingi trilioni moja ambao utatumika kukopesha mabenki na taasisi za fedha kwa riba ya asilimia 3, ili taasisi hizo ziweze kukopesha sekta binafsi. Benki au taasisi ya fedha itakayofaidika na mfuko huu itatakiwa kukopesha sekta binafsi kwa riba isiyozidi asilimia 10 kwa mwaka. Hatua hii itaongeza ukwasi na kupunguza riba za mikopo kwa sekta binafsi"
 
Kwa maana hyo ni hiari kuchukua huo mkopo, kwa hyo ukichukua vigezo na masharti kuzingatiwa na benki zisipochukua Ina maana hawalazomishwi kufuata hyo masharti.
 
Tz mizinguo sana, eti hiyo ni kwa special customers walio na minimum risks ya ku default the likes of Bakhresa na Asas. Serikali inabidi itafute solution ya mikopo iwe kwa riba rafiki, riba za Tz ni wizi mtupu, mtu anapewa mkopo riba 18% halafu non reducing rate, after 5yrs analipa 90% ya mkopo kama riba so kama alichukua 100m, atalipa riba 90m, jumla aliyolipa 190m, huu kama sio wizi ni nini kwa kweli ?
Mkuu tuseme wewe ndio unakopesha una kamtaji kako..., unadhani kwa risky involved kwa watu ku-default Bongo ungeweza kufanya hizo Biashara kwa riba ndogo ukizingatia majority wanaweza wasilipe ?

Kumbuka hii ni Biashara na kutokana na Risky inabidi rates ziwe accordingly ama sivyo na wewe unaweza kujiunga na hao wakopaji soon or later kwa kufunga biashara yako na kutafuta mkopo...

Ingekuwa watu wengi ni Credit Worthy Benki zenyewe zingepanga foleni kubembeleza watu na kushusha riba to the minimum
 
Uwezo wako wa kulipa au kurudisha deni( ability to pay back) uko vipi, Pia thamani yetu ya pesa pia baada ya muda fulani( Time value of money)

Nakukopesha Leo million 7,je baada ya miaka mitatu milion7 thamani yake Itakuwa hivyo hivyo au itashuka

Vitu vinavyonunuliwa kwa million 7 mwaka huu 2021 vitaweza kununuliwa kwa milion7 mwaka 2022

ili kufidia thamani ya pesa Isipotee kwa mkopeshaji unafidia kwenye riba pia

Thamani yetu ya pesa haitabiriki pia

Fikiria shs 10 na shs 20 ya Leo hazina thamani tena hata Pipi ya mtoto huwezi Nunua, Miaka 10 iliyopita Pipi zilikuwepo za shs 10 na 20.Kufidia huu utofauti unaongeza kwenye riba pia

Sent using Jamii Forums mobile app
una akili sana aise
 
Mkuu tuseme wewe ndio unakopesha una kamtaji kako..., unadhani kwa risky involved kwa watu ku-default Bongo ungeweza kufanya hizo Biashara kwa riba ndogo ukizingatia majority wanaweza wasilipe ?

Kumbuka hii ni Biashara na kutokana na Risky inabidi rates ziwe accordingly ama sivyo na wewe unaweza kujiunga na hao wakopaji soon or later kwa kufunga biashara yako na kutafuta mkopo...

Ingekuwa watu wengi ni Credit Worthy Benki zenyewe zingepanga foleni kubembeleza watu na kushusha riba to the minimum
Vipi kwa wafanyakazi wa serikali ambao wanakopea mishahara , na wenyewe wana risk ? Tz banks are just too greedy, wanataka over profit, hii sawa, serikali ilinde watu wake.
 
Back
Top Bottom