Tuache siasa kwenye ujenzi: Majibu ya nyufa hizi, yatolewe na The Professionals, AQRB, ERB, CRB, na sio mtuhumiwa TBA!

Yule jamaa wa TBA kanikasirisha sana eti ni kawaida kwa majengo marefu kupiga ufa...

Hadi sasa hivi nimeshangaa yupo duniani.. Tetemeko likipita hapo kuna idadi kubwa sana ya wanafunzi hapo kupoteza maisha, kwaajili ya ujinga ya msomi mmoja kuidanganya dunia kawaida ya majengo marefu kupiga ufa....
 
Tuliawaambia kuwa serikali inajidai kufanya kazi yenyewe uku ikiwa haina wataalamu wa kutosha wakakataa. sasa inabidi ata uchunguzi wa haya majengo ufanyike kule Kagera ihungo wanakojenga TBA, pale Magomeni kwenye majengo na kwingine kote wanakojenga TBA ili tupate uhalisia wa thamani ya fedha zilizotumika na ubora wa majengo. inabidi mkaguzi na mzibiti wa hesabu za serikali apewe ruhusa ya kukagua mahesabu na Pia watu wa procurement wapitie Tender aliyopatiwa mzabuni TBA ili tujue atalipa vipi hizo garama.
 
Rudia tena kusoma utaelewa alikuwa anamaanisha nini kuwahusu CRB
Rudia kusoma nilichoandika, sijakosea kuandika wala kusoma nilichokijibu.
Client wa yale majengo aliweka manager wake ambaye kwa sifa ni Muhandisi.

Huyo hakaguliwi na CRB.

Aulizwe mshauri mwelekezi kama manager alimanage na kusimamia ujenzi kama mshauri mwelekezi alivyoelekeza.
 
Ili mtoa mada ajibu swali lako nawe tumia verified ID kama yake..........
With or without verified ID Paschal haya ni yako wewe na babu yako. .Ila kuna siku isiyo na jina mtaumbuka tu. Kwa sasa hivi jibuni swali hili : Ni kwa nini mmeshupalia kuvunja jengo zuri La Tanesco lisilo na nyufa hata moja na linaloweza kubakia asset kwa Miaka 200 na badala yake mnajenga vijengo watu wanakaa wiki 2 tu navinabomoka ?
 
kaenda jioni tu jana bila kufanya any engineering analysis na anawaambia watu ati hizo ni "nyufa za kawaida tu". Tuache politic kweli. Huenda kitu kipo kinasink slowly. Ndo tabu ya Contractor huyo huyo kujifanyia consultation/supervision. Hakuna checks and balances kabisa.
Kweli mkuu aliyetakiwa kwenda kukagua ni structural engineer kutoka bodi nyingine huru sio washutumiwa ndiyo wanajikagua
 
Pascal Mayalla,
Paskali mimi si Mkadiriaji Majenzi ni Mhandisi lakini kwa uelewa wangu mdogo kwenye suala la gharama za ujenzi wa majengo haya sikubaliani na sitakubali kamwe kuhusu gharama ya bilioni 10 kama ndiyo iliyotumika hapa. Bwana Magogoni alidanganya umma lazima niseme ukweli.

Pili TBA kwa tabia yao haya walijitakia wenyewe sabb wamekuwa na mazoea ya kujikagua wenyewe kwenye mambo ya ujenzi suala ambalo ni kinyume na taratibu. Hiyo inayoitwa TBA brigade usidhani ni Kampuni ya nje bali ni jina tu lakini wajenzi ni hao hao TBA na ndiyo maana hao wanaojiita Consultant yaani TBA Dsm wanapokea malipo ya kazi husika sasa umewahi kuona wapi anayejenga ni Mkandarasi lakini anayelipwa kwa kazi iliyofanyika ni Mshauri?

Mwisho hizi Taasisi unazoztaja hata siku moja hawana ubavu wa kukanyaga miradi inayotekelezwa na Mkandarasi anayeitwa TBA brigade sabb wanajua fika anayefanya kazi hiyo ya ujenzi ni TBA Dsm na wanajuana vizuri hivyo suala la uchunguzi halitasaidia kitu
 
Pascal Mayalla,
Hizo bodi ulizotaja ni kama zipozipo tu. Wangekuwa wanaheshimu taaluma wasingekaa kimya kuhusu kauli za kisiasa kutawala kabla ya ujenzi. Sasa hivi ni too late, makosa yameshafanyika watabaki kutupiana mpira..
 
Back
Top Bottom