tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,239
- 4,464
Nimekuwa nashangaa sana kuona wanasiasa wanajigamba majukwaani kwa utoaji wa vitambulisho vya Wazee kama utambulisho wa kupata huduma bure za matibabu pale waendapo hospitali za serikali. Ni wazo zuri lakini sio kwa namna hiyo.
Duniani kote, afya bure haijawahi kufanikiwa. Ukipewa kitambulisho cha kupata huduma ya Afya bure, nani atalipia gharama zako? Je, kuna mtu yeyote anachangangia kwenye hiyo pool ya wazee? Tuseme ukweli, Serikali haijakuwa mwaminifu kupeleka pesa kwenye hospitali zake za umma ambazo yamkini pamoja na kuhudumia hawa wazee wanaopewa vitambulisho zingeweza ku sustain service.
Afya bure bila ya mtu kuchangia gharama za yule anayehudumiwa bure, huishia kuua huduma nzima ya afya; na hivyo kuwaathiri hata wale wanaoendesha huduma za Afya kupitia cash au mifuko ya bima.
Kama serikali inaweza, ikawafungulie hawa wazee bima ya Afya. Tena sio zile CHF za kulipia elfu 5 kwa mwaka. Na ikiwezekana waachane kabisa na huo mpango wa pensheni za uzeeni bali wawasajili hawa wazee wetu kwenye mifuko ya bima.
Kutoa kitambulisho cha kupata huduma za afya bure bila mtu kuchangia, ni sawa na kumkamua maziwa ng'ombe bila kumpa majani.