Mjuni Lwambo
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 9,402
- 8,866
Mimi nimeuliza swali, unasema ni ubishi wa kijinga! Kwako wewe mtu akikuuliza swali anakuwa ni mbishi wa kijinga!?Sipendi ubishi wa kijinga. Mi siyo mjinga. Umeshinda mkuu. Nakupa kombe🙌 🙌
Ok! mimi sijui kama wewe ni mjinga au siyo mjinga ila ninachojua umeshindwa kujibu swali langu.
Ukisema umri mdogo, kuna mtu anamaanisha miaka mitatu hadi kumi, mtu mwingine hadi miaka 17 ni "kuwa mdogo", Kuna sehemu hadi umri wa miaka ishirini na tano(25) bado unachukuliwa ni mdogo!
Daniel Everret alizaliwa mwaka 1951, mnamo mwaka 1977 alifika katika kijiji kidogo cha Piraha kilichoko kwenye misitu ya Amazon.. Wapiraha ni jamii iliyokuwa inaongea lugha ngumu kabisa kuwahi kutokea. Lakini Daniel Everret akiwa na mkewe Keren Graham walifanikiwa kujifunza Kipiraha kwa ufasaha wakiwa katika umri wa kiutu uzima(miaka 26+) na kufanikiwa kuandika biblia ya kwanza kwa lugha ya Kipiraha.
Lakini pia, ukienda kusoma Urusi au China, ni ĺazima ujifunze lugha yao kwanza ndio uanze masomo halisi, kwa lugha yao, wengi tu wanakwenda kusoma katika hizo nchi kwa level ya Postgraduate, kwa maana wengi ni watu wazima tayari, na wanazielewa hizo lugha.
Kwa hiyo ndugu yangu usiyependa ubishi wa kijinga kwa sababu unadai kwamba wewe siyo mjinga, maelezo kwamba ili uelewe lugha inabidi ujifunze "ukiwa mdogo", ambayo kiuhalisia ni maoni yako binafsi, hayana msingi wowote, hivyo basi, NINAYAPUUZA!
Hisia zake, watu wazima wanasoma kingereza kwa Ras Simba