Tuache masihara, idara ya FBI ya Marekani wako Sayari nyingine kwenye mambo ya uchunguzi wa makosa ya jinai

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Kuna kipindi nilisoma mtazamo wa mwenajukwaa huku anaitwa Nyani Ngabu kuhusu kesi ya mwanamuziki Robert Kelly ya unyanyasaji wa kingono, jamaa akasema FBI wakikushitaki uwezekano wa wewe kuchomoka ni chini ya 10% sikuamini saana. Akasema uwezekano wa R. Kelly kuchomoka ni mdogo sana sikutilia maanani sana.

Sasa kwa mwezi mzima huu nimekua nikiangalia documentaries za FBI files, kipindi cha matukio ya kihalifu yaliyochunguzwa na FBI na wahalifu kukamatwa, hakika nimeamini wale jamaa wako mbali sana, wako Sayari nyingine kabisa ya uchunguzi.

FBI wanaweza kukuchunguza kwa miaka 17 na mwisho watakukamata tu, ni nafasi ndogo saana watu kunusurika kutiwa nguvuni wakichunguzwa na FBI, wale jamaa wana matukio ya hadi ya miaka ya 30 na jinsi watuhumiwa walivyokamatwa kwa kweli wale jamaa hawafai.
 
Hapa kwetu kesi moja ya Billionea Msuya Watuhumiwa mmoja wao Jina limenitoka alifanyiwa mateso yalompelekea hadi kumpa mke wake Talaka akiwa wakati wa upelelezi maana asingeweza kuwa mwanaume tena.

Na baadae ushahidi ukaonesha yeye hakuwa na Hatia na kuachiwa.
Yapo mambo Yanafanyiwa umakini hapa kwetu ila Sehemu kubwa Ni kutumia Nguvu si akili
 
Kwa hiyo na wewe unaona umegundua jambo jipya, kwamba Idara ya Upelelezi ya nchi yenye Uchumi mkubwa kuliko yote Duniani inaongoza kwa upelelezi ? Basi hongera sana kwa kuligundua hilo labda utashinda nobel prize, who knows ?
tatizo lako hunawi, nilishakueleza
 
Ila mm nilipoiba $27228728b mpaka leo hawajajua n nani alifanya umafia ule
 
Maboresho kwenye jeshi la polisi ni mengi mno, kuanzia udahili wao, mishahara, makazi, tecnolojia za upelelezi, mahusiano yao na vyama vya siasa, mahusiano yao na raia, handling ya mahabusu, uendeshaji wa mashitaka, mahusiano ya wao kwa wao wawapo uraiani, mahusiano yao na vyombo vya habari, handling ya kesi kubwa na ndogo kwenye public nk so much more
 
Ungemsikiliza Peter Anett kuanzia kuanza kwa kumhoji rafiki wake wa zamani (Osama Bin Laden) mpaka anakuja kukamatwa ndio ungekiri zaidi kuwa USA ni super power
 
Kwa hiyo na wewe unaona umegundua jambo jipya, kwamba Idara ya Upelelezi ya nchi yenye Uchumi mkubwa kuliko yote Duniani inaongoza kwa upelelezi ? Basi hongera sana kwa kuligundua hilo labda utashinda nobel prize, who knows ?
Acha husuda dada
 
Kwa sababu ya fedha na technologia. Inawawezesha kufanya chochote kurahisisha mambo na pia kutoa mafunzo bab kubwa kwa wataalam wao.
Kingine ni kwamba wanashirikiana sana na taasisi au mashirika ya watu binsfsi hivyo kuwawezesha kuwa na access ya vitendea kazi vingi zaidi.
Zana walizo nazo hata ukiwapa wabongo nao wataonekana exceptional pia.
 
Kule file huwa halifungwi anapoingia mtu mpya anakabidhiwa faili anasoma baade anapitia kuona kama wa nyuma yake alipitwa na baadhi ya vitu.

Tukio lolote linapotokea linalinganishwa na matukio ya nyuma kama kuna mahusiano.

Recruitment process yao ni ya umakini wa hali ya juu pamoja na mafunzo yao huku kwetu wengi wanaoenda vitengo hivyo kiasi kikubwa ni connection
 
Kila jambo zuri linahitaji uwekezaji na ili uwekeze kwa usalama kuwe na macho ya kuangalia wajanja/mafisadi.Niliwahi kusikia mara kadhaa kulikuwa na uwekezaji katika mambo muhimu lakini wajanja wakajinufaisha kwanza.

Inawezekana kabisa kazi aliyopewa Lugumi na washirika wake ingetutoa kimasomaso kama ingefanyika kwa uadilifu na uzalendo.
 
Hapa kwetu kesi moja ya Billionea Msuya Watuhumiwa mmoja wao Jina limenitoka alifanyiwa mateso yalompelekea hadi kumpa mke wake Talaka akiwa wakati wa upelelezi maana asingeweza kuwa mwanaume tena.

Na baadae ushahidi ukaonesha yeye hakuwa na Hatia na kuachiwa.
Yapo mambo Yanafanyiwa umakini hapa kwetu ila Sehemu kubwa Ni kutumia Nguvu si akili
Mwafrika toka lini akaamini katika akili? Yeye kila kitu nguvu.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom