Tuache longolongo, Je ni kweli Halima Mdee hajawahi kuongelea barabara?

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
321
448
Kama barabara za Kawe ni mbaya mchawi ni serikali ya CCM sio Halima Mdee. Kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake.

Sio kuongelea tunaongelea kuhakikisha zinatengenezwa mdomo mtu yeyoteaweza kuchonga
Mbowe alikuwa haongelei barabara jimboni kwake lakini kutwa Alikuwa akienda wizara ya ujenzi kipindi Cha Magufuli akiwa waziri ili kumshawishi barabara jimboni kwake zijengwe zikajengwa Mdee Hakuna kitu
 
Achilia mbali barabara kijana.

Huyo halima nilipewa taarifa zake majuzi na jamaa wa Dar kule boko basihaya kuwa hajawahi kukanyaga mtaa wao, ikizingatiwa asilimia kubwa mwenyekiti wa mtaa mpaka mbunge alikuwa chadema ila mbunge hainekani.

Jamaa anaendelea kudadavua, eneo lao wakati wa mvua maji yanajaa sana yakitokea wazo ila mpaka anakuja rais Kikwete (enzi hizo) kutatua na kuongea na wananchi mbunge aonekani.
 
Dada kumbuka kuwa wakuzitengeneza barabara ni serikali sio Mbunge. Pili serikali ambayo haisikii kwa taratibu za kibunge hadi uanze tena kuishawishi kvingine hiyo haifai kuwepo. Tatu, kuna wenzako wameanzisha uzi wanasema Mdee hajawahi kuongelea kabisa barabara, je hao pia unawakana au?

Haya kuna ushaiwish gani mwingine zaidi ya huu hapa chini au unataka hadi waziri ahongwe?

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.

MHE. HALIMA J. MDEE:
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru.

Kwanza nimshauri tu Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, usiige utamaduni wa mtangulizi wako wa kutuletea vitabu vikubwa ambavyo mtu akisoma between the lines kuna maneno mengi kuliko uhalisia. Ushauri wangu kwako tu, inawezekana huu ni mwaka wa kwanza bado una mihemko ya aliyekutangulia, kuanzia mwaka ujao uje na kitabu ambacho kinaeleza tumepanga nini na tutatekeleza nini kwa huo mwaka, hilo ni la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili watu ambao mnaongea sana, sijui Mheshimiwa Magufuli alivyokuwa Waziri kafanya nini, mwaka jana mwenyewe amekiri hapa, katika miaka kumi ya Ilani ya CCM, 2005 – 2015 ameweza kutekeleza asilimia 31 ya kile mlichotakiwa mkifanye. Sasa hivi nyie mtoto akifanya mtihani akipata 31 chini ya 100, hivi huyo amefeli amefaulu? Kwa hiyo, tuache kujikomba, unafiki, tusaidie Serikali ndilo jukumu letu kama Wabunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nina barabara zangu Jimboni, najua kuna wengine huko wanapata shida na barabara zao zimechokachoka, sisi wa town tuna nafuu kidogo. Lakini nimeahidiwa hapa, miaka mitatu iliyopita na Mheshimiwa Waziri, naomba utoe majibu. Kuna barabara za kupunguza foleni mkoa wa Dar es Salaam; barabara ambazo zinaunganisha Jimbo la Kibamba na Jimbo la Kawe; barabara ya Goba – Tanki Bovu; Goba – Wazo Hill –Tegeta, Gao – Goba – Makongo – Mlimani City.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba mkiwa mnanijibu hapa, msiniambie ujenzi umeanza, ninajua hizi ni barabara tatu tofauti zinazounganishwa na kipande kimoja. Sasa nataka leo msiniambie kwa sababu ukiangalia vitabu vya bajeti, na ndio maana nawaambia Waheshimiwa Wabunge,tuwe tunasoma, tukiwa hatusomi Mawaziri hawa wanakuja wanatudanganya. Miaka mitatu mfululizo hizi barabara zimetengewa fedha, kipande cha kuunganisha Jimbo la Kibamba na Kawe, Goba – Mbezi, Goba – Wazo Hill, Goba – Mlimani City, lakini leo ni mwaka wa tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaona kuna hela zimetengwa hapa, zipo, kama ambavyo mwaka wa jana Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa maneno haya haya kama ya kwako zilikuwepo lakini mwaka mmoja baadaye hakuna barabara. Sasa Waziri kesho ukiwa unajibu naomba uniambie kwa uhakika wananchi wa Kawe wasikie, kwa sababu wewe ni mwananchi wangu pia na Mbunge wako nikiwa nazungumza lazima usikilize hizi barabara zinakamilika lini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka wa juzi, wakati wanajenga hii barabara ya Mwenge – Tegeta – Kibaoni niliishauri Serikali nikaiambia wakati wa mvua kuna kiwango kikubwa cha maji kinachotoka ukanda wa Wazo huku juu Goba na ili barabara iweze kudumu kuna maeneo ambayo lazima mapokeo na matoleo ya maji yawe makubwa Ili tuweze kuelekeza maji baharini. Leo barabara imejengwa, mvua ikinyesha ukiwa pale Afrikana, Goigi ni majanga, hii barabara itakatika miaka mitano haitimii, kuna faida gani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi namuomba Mheshimiwa waziri akiwa anajibu, kwa sababu niliandika barua kama Mbunge nikiwaomba; mkasema ooh! huyu mjapani ambaye tumepewa msaada ana masharti tutatumia fedha za ndani kujenga mapokeo ya maji makubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo naomba niambiwe maana mvua ikinyesha yakitokea maafa Mheshimiwa Jenista Mhagama huyo, halafu mvua ikikauka na yeye anasepa, barabara iko vilevile. Sasa leo nataka mniambie mna mikakati gani, dhahiri, shahiri, kuweza kuokoa ile barabara ya mabilioni ya shilingi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu Rais ambaye watu tunaambiwa tusimtajetaje, tutamtaja tu kama alichemsha, msitutishe. Wakati tunapitisha bajeti ya barabara ya Mwenge – Tegeta ya shilingi bilioni 88 tuliambiwa hii barabara itajengwa vipande viwili, kwa matukio mawili. Moja ni Mwenge kwenda Tegeta ya pili ni Mwenge kwenda Morocco, bilioni 88. Sasa leo kuna uchafu unaendelea pale, kutoka Mwenge kwenda Morocco sijui mnatengeneza kichochoro, sijui mnatengeneza kitu gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninataka nijui zile shilingi bilioni 88 ambazo Mheshimiwa John Pombe Magufuli, katika Bunge hili akiwa Waziri alisema kazi yake ni kujenga hizi barabara mbili, ziko wapi? Nataka majibu. Na ule uchafu mnaojisifia sijui fedha za Uhuru, sijui fedha za nini, ile barabara ilikuwa na pesa; kwa hiyo msitafute ujiko kwa kuwa mmezitafuna zile pesa mnatuletea uchafu. Si hadhi ya Dar es Salaam kujengwa ibarabara zile na kama mnatuambia mnajenga kwa muda, hilo pia ni tatizo linguine, misuse of resources. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mafuriko. TANROADS walifanya upembuzi yakinifu sijui mnavyoita ninyi, wakatengeneza na michoro kwa ajili ya mfereji mkubwa kuzuia mafuriko ukanda wa Kunduchi, miaka minne imepita. Mwaka juzi alienda Mheshimiwa Pinda, akaambiwa mchoro huo upo, wakati wananchi wanaelea kwenye bahari ya mafuriko, mkasema itajengwa, itatengewa fedha, hakuna kilichofanyika, naomba nipate majibu kesho.
 
Kawe hawahitaji Hansard za bunge wanahitaji barabara usituletee Hansard za bunge barabara iko wapi?

Tunataka barabara sio makabrasha ya bunge.Hatukukutuma ukatuletee makabrasha ya bunge
 
BARABARA YA MAKONGO CCM NDO WAKULAUMU

Barabara ya makongo iko kisiasa sana
Issue kubwa ilikuw ni fidia, na serikali ilikua hautaki kulipa fidia, sabab barabara nzima ilikuw inapita kwenye nyumba za watu tena wakubwa

Kipindi cha chaguzi za serikali ya mtaa, makonda alipeleka mkandarasi wa kisiasa, akachimbuw mwanzo hapa ardhi baada ya uchaguzi kupita, akatokomea

Kuna kipindi issue ya madai ya fidia, ilisababisha mpaka Serikali kutishia kuhamisha mradi upitie changanyiken, kumbe ilikua propaganda za kumwekea ndalichako lami mpaka nyumbani wake, ilipofika tu kwake, ikaishia hapo

Halima alichokua anasimamia siku zote ni watu wa makongo wapate haki yao, ya kulipwa fidia kutokana na mradi huo wa barabara
 
Kawe hawahitaji Hansard za bunge wanahitaji barabara usituletee Hansard za bunge barabara iko wapi?

Tunataka barabara sio makabrasha ya bunge.Hatukukutuma ukatuletee makabrasha ya bunge

KWANINI UNAMDHALILISHA RAIS WETU MPENDWA KUTAKA KUWAAMINISHA WATU KUWA HALETI MAENDELEO?
 
Kawe hawahitaji Hansard za bunge wanahitaji barabara usituletee Hansard za bunge barabara iko wapi?

Tunataka barabara sio makabrasha ya bunge.Hatukukutuma ukatuletee makabrasha ya bunge

Sio kuongelea tunaongelea kuhakikisha zinatengenezwa mdomo mtu yeyoteaweza kuchonga
Mbowe alikuwa haongelei barabara jimboni kwake lakini kutwa Alikuwa akienda wizara ya ujenzi kipindi Cha Magufuli akiwa waziri ili kumshawishi barabara jimboni kwake zijengwe zikajengwa Mdee Hakuna kitu

Kwa Nini khs barabara usimuulize waziri wa ujenzi ambaye Ni wa CCM...
Mbunge hajengi barabara na Hana Hilo fungu kwa ujenzi wa barabara...
 
Achilia mbali barabara kijana.

Huyo halima nilipewa taarifa zake majuzi na jamaa wa Dar kule boko basihaya kuwa hajawahi kukanyaga mtaa wao, ikizingatiwa asilimia kubwa mwenyekiti wa mtaa mpaka mbunge alikuwa chadema ila mbunge hainekani.

Jamaa anaendelea kudadavua, eneo lao wakati wa mvua maji yanajaa sana yakitokea wazo ila mpaka anakuja rais Kikwete (enzi hizo) kutatua na kuongea na wananchi mbunge aonekani.

Umesahau Ile kauli ya Mwenyekiti...
Yale majimbo ya upinzani hatopeleka maendeleo.

Ile kauli Ni ya kibaguzi Sana.
 
Kwa Nini khs barabara usimuulize waziri wa ujenzi ambaye Ni wa CCM...
Mbunge hajengi barabara na Hana Hilo fungu kwa ujenzi wa barabara...
Kama mbunge hajengi barabara miaka yote 10 alikuwa akifanya Nini bungeni? Kula posho na kulala? Huyu Ni out Ina maana hata akienda Tena atarudi na hadithi hizi hizi Mdee out
 
Kama barabara za Kawe ni mbaya mchawi ni serikali ya CCM sio Halima Mdee. Kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake.

Kwa miaka kumi iliyopita hizi barabara zilikuwepo miaka yote hamsini Jimbo lilikuwa chibi ya ya mbunge wa ccm. Nilikwenda kongwa kwa spika, ni hatari.
 
BARABARA YA MAKONGO CCM NDO WAKULAUMU

Barabara ya makongo iko kisiasa sana
Issue kubwa ilikuw ni fidia, na serikali ilikua hautaki kulipa fidia, sabab barabara nzima ilikuw inapita kwenye nyumba za watu tena wakubwa

Kipindi cha chaguzi za serikali ya mtaa, makonda alipeleka mkandarasi wa kisiasa, akachimbuw mwanzo hapa ardhi baada ya uchaguzi kupita, akatokomea

Kuna kipindi issue ya madai ya fidia, ilisababisha mpaka Serikali kutishia kuhamisha mradi upitie changanyiken, kumbe ilikua propaganda za kumwekea ndalichako lami mpaka nyumbani wake, ilipofika tu kwake, ikaishia hapo

Halima alichokua anasimamia siku zote ni watu wa makongo wapate haki yao, ya kulipwa fidia kutokana na mradi huo wa barabara
Umesema yote
Kuna wengine wapo humu kuongea na kubeza
Halima amejituma sana
ccm ndio wa kulaumiwa si vinginevyo
 
Kama barabara za Kawe ni mbaya mchawi ni serikali ya CCM sio Halima Mdee. Kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake.

Yapo majimbo ya uchaguzi nilisha yasema hum kwamba hakuna mtu wa kuwazuia Rudi bungeni mmoja ni kawe ,Arusha,mbeya mjin ,hai ,kwa heche ,matiku n.k tatizo ccm walisha jiaminisha kwamba uchaguzi 2020 ni mwepesi mno kitu ambacho ilikua kosa kubwa la kiufundi Sana ,achana na uchaguzi mkuu kabisa
 
Uongo wa mchana kweupe , labda asiyefuata bunge , maccm yako bize kukusanya kodi tu za wana Kawe ila hayapeleki maendeleo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom