Tuache kuwalipa wabunge,tuwape nyongeza ya mishahara walimu wetu

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
11,495
24,174
Ukiangalia mchango wa zaidi ya 70% ya wabunge kwenye bunge letu ukilinganisha mishahara, posho na mafao yao utaona ni kiasi gani bunge linatia hasara Taifa letu. Wakati huu ambao Taifa linaendelea na miradi mikubwa ni vyema Ubunge ukawa ni kujitolea na tukasitisha malipo yote kwa wabunge na baadala yake hela yote ikaenda kuwa nyongeza kwenye Mishahara ya walimu na kuboresha maisha yao.

Mh Rais wetu wanyonge na Mzalendo namba moja ni vyema ukaamua hili haraka ili tuwaokoe walimu wetu na hali ,mbaya walionayo ukilinganisha na msaada mkubwa wanaoutoa, Makada wote wa chama kubwa aka chama tawala CCM ni vyema kwa nguvu yenu mkapigania hili kuonyesha uzalendo wenu na kuwajali wanyonge.
Wale wote tunaounga mkono juhudi tujitahidi na kushirikiana kupigania hili.
 
Mkuu tuwe wazalendo tutetee walimu wetu..
Siwezi mimi hao kila mwezi wanapata mshahara MI napigwa jua hapa makoroboi halafu pili hao ndo waliosimamia uchaguzi kura wakaiba wakampitisha uyo jamaa so acha awanyooshe
 
Sasa mwalimu wa nchi hii anahusika vipi na wewe kupigwa jua hapo makoroboi? Halafu umeshawahi kusimamia uchaguzi wowote ule ili utoe ushahidi ni kwa namna gani hao walimu wanavyoiba hizo kura? Mimi nimesimamia 2010 na sikuona ni kwa namna gani watumishi wa serikali wanavyoshiriki kuiba hizo kura! Zaidi niligundua tu vyama vya upinzani havina mizizi maeneo ya vijijini na pia matokeo mfano ya ubunge hutangazwa na mkurugenzi!

Sasa mwalimu hapa anahusika kwa namna gani? Ifikie wakati hizi propaganda ziishe! Na mfanyakazi kama walivyo watanzania wengine, wana uhuru wa kumchagua kiongozi wanayemtaka kutokana na ushawishi wa huyo mgombea hata kama atakuwa ni pasua kichwa kama huyu aliyesukumizwa!
 
Back
Top Bottom