Tuache kushabikia mambo yasiyo na maslahi kwa Watanzania

D

Danisamweswa

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Messages
453
Points
195
D

Danisamweswa

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2013
453 195
Ni wiki nzima sasa vyombo vya habari na wana Jamii forum wamekuwa wakizungumza habari za Zito, Mkumbo, Mbowe na Slaa. Hivi niulize umuhimu uliowekwa kwenye Maamuzi ya CC ya CDM kuwavua madaraka Zitto na Mkumbo vina maslahi kwa nchi hii?

Kama CDM kiliridhika kuwa uamuzi wa kuwavua madaraka ya hao watu kwenye chama kwa kukiuka kanuni na taratibu za chama kelele ni za nini? Kama waliovuliwa wanaona wameonewa kwa nini wasifuate taratibu zilizopo kwenye chama chao kudai haki yao kama haki yao imekanyagwa?

Mimi naona jambo hilo halina umuhimu wowote kwani kama watu walionekana waasi ni waasi tu hakuna lugha nyingine ya kubadili hilo. Jambo pekee linaoweza kuwaondoa katika hilo ni CDM iliyowaona kuwa wasaliti wajiridhishe kuwa tuhuma hizo siyo za kweli. Cha msingi muda waliopewa wa kujibu tuhuma zao wautumie kujibu tuhuma hizo kwa taratibu za chama chao. Na mwisho wa siku chama kitaamua hatma ya wanachama hao.

Watanzania tujifunze kutoshabikia mambo yasiyo na maslahi kwa nchi yetu. Zitto ni nani na Mkumbo ni nani hata wachukue muda wetu mkubwa kiasi hicho? Wanasiasa wa Tanzania wajifunze kuaminika na kuishi katika imani hiyo.
 

Forum statistics

Threads 1,326,853
Members 509,593
Posts 32,237,436
Top