Tuache kumlaumu Mwl. Nyerere! Kosa ni la kwetu wenyewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuache kumlaumu Mwl. Nyerere! Kosa ni la kwetu wenyewe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Oct 16, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Inasikitisha kuona baadhi ya watu wakibedha uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k. Nyerere kwamba alikuwa mbaguzi kwenye suala/tasinia ya elimu. Binafsi, naona ni kumvunjia hadhi na heshima hayati Mwl. Nyerere kwa mazuri aliyoyafanya kwa watanganyika. Tukumbuke kwamba kabla ya uhuru wa Tanganyika na baada ya uhuru sekta ya elimu ilikuwa ya kibaguzi; ililenga makundi mahususi ya watu. Ilizingatia udini na matabaka yaliyokuwepo wakati huo.

  Tabaka la udini lilikuwa bayana kabisa. Madhehebu ya Kikatoliki kupitia mashirika yake mengi ndio walikuwa na shule nyingi za msingi, sekondari na hata vyuo vya ufundi. Madhehebu mengine kama waluteli na waanglikana hakuwa nyuma. Kundi jingine ilikuwa ni wahindi ambao walikuwa na shule chache maeneo ya mijini.

  Wajerumani walipoanza kuitawala Tanganyika miaka ya 1880, gavana wao wakati huo Von Soden alitoa ruzuku kwa shule za misheni. Lengo ilikuwa kupata watu wachache watakao saidia utawala katika kazi zao za kila siku. Hadi kufikia 1911 serikali ya kikolloni ilikuwa na shule 83 na wamishenari walikuwa na shule takribani 918. Shule za serikali zilikuwa na wanafunzi 3,000 na missheni wanafunzi 65,000. Waingereza nao baadaye kuanzia 1918 wakaendeleza ya wajerumani kusaidia shule za misheni. Hawa wakawa waandalizi wa kuwaandaa watanganyika kupata uhuru wao. Wakaanza, kama wajerumani, kuwaandaa watanganyika wachache kushika madaraka ya nchi. Na ilikuwa ni kupitia elimu ya kimaghariibi tu kwamba watanganyika wangejitawala.

  Kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa watawala waliondaliwa na wakoloni wangetokea maeneo yale ambayo wamishenari wa kikristo walishajijenga na kuanzisha shule. Hapa ina maanisha kwamba watu kutoka Kilimanjaro, Arusha, Kagera, Mara, Ruvuma na Mbeya ndio waliokuwa wakipewa nafasi ya kuwa watawala wa Tanganyika huru.

  Baada ya uhuru mfumo huu ulionekana wazi ni wa kibaguzi. Mathalan, wamishenari wengi walijikita katika maeneo muhimu kiuchumi. Wakajenga makanisa na shule mikoa ya kaskazini, Kilimanjaro,Arusha. Kanda ya ziwa Kagera. Na kusini wakajenga Iringa, Mbeya,Ruvuma nk. Maeneo mengi ya pwani hawakujihusisha sana. Huko walibaguliwa na hawakupendwa sana na waislamu ambao walikuwa wengi maeneo hayo.

  Kwa hiyo, baada ya uhuru Mwl. Nyerere akaona ipo haja ya kufuta mfumo huo wa kibaguzi kielimu. Kupitia sera ya ujamaa na kujitegemea (1967)Mwl. Nyerere akataifisha shule na vyuo vyote vilivyokuwa vya wamishenari. Hapa akatoa haki kwa watanzania wote kupata elimu sawa. Kufikia mwaka 1977 Mwl. Nyerere akatangaza Elimu Kwa Wote (UPE) ndipo kila mkoa, kila wilaya, kila tarafa, kila kata kukawa na shule za msingi. Watoto waliofikia umri wa miaka 7 kwa zaidi ya 10% wakaandikishwa shule.

  Uendeshaji wa shule hizi zote ulitumia fedha za serikali. Wizara ya Elimu ya Taifa iliendesha shule hizi pasipo ubaguzi wa dini wa ukanda ama matabaka. Ila katika baadhi ya maeneo ya Tanzania bado mwamko wa elimu ulikuwa duni na bado hadi leo ni duni. Sababu kubwa ni mbili. Ama shughuli za kiuchumi ama sababu za kiimani. Mfano, katika mikoa ambayo ufugaji umekuwa nguzo kuu ya uchumi wa jamii, elimu haijapewa mkazo sana, maeneo kama Shinyanga, Mwanza, Arusha, Singida na Dodoma. Wasukuma na wamasai wanapeleka watoto machungoni badala ya kuwapeleka shule. Maeneo mengine, shule zinaonekana kukinzana na utamaduni na imani za jamii. Shule huonekana kubomoa maadili ya dini yao.

  Aidha, ikumbukwe kwamba, shule za awali kabisa za kimishenari wa kikristo zilianzia Zanzibar na mikoa ya pwani. Wenzetu hawa hawakuzipokea kama zilivyopokelewa huko bara. Pale Zanzibar watumwa waliokombolewa toka utumwani ndio waliofaidi elimu ya kimagharibi. Wenyeji walizingatia elimu ya dini,shaaria za kiislamu na lugha ya kiarabu. Kwa mfano, wanawake wa pwani hawakuhamasishwa kabisa kusoma katika shule za wamishenari wa kizungu. Kwa madai kwamba huko wangefundishwa maadili ya makafiri na kulishwa nguruwe.

  Katika vigezo kama hivyo, si dhani kama ni halali kumlaumu Mwl. Nyerere. Yeye kama mchungaji aliwapeleka mbuzi mtoni, kwa hiyo ni utashi wa mbuzi kunywa maji au kutokunywa. Mwl. Nyerere amefanya makubwa mno kuwasomesha waislamu. Ila wao wamekuwa na mwitikio mdogo, kufikia miaka ya 1980 ndipo wakaanza kuja juu kuchangamkia elimu ya kimagharibi. Hata hivyo, katika shule zao nyingi mkazo umebaki kwenye somo la dini na lugha ya kiarabu.

  Hebu tuache kumlaumu Mwl. Nyerere! Kosa ni la kwetu wenyewe. ​
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ni kweli mkuu, hata performance ya waislam ilishuka pale Prof. Malima alipobadilisha majina kwenye mitihani na kuwa namba. vitendo hutoa ujumbe mzuri zaidi kulika maneno. na serikali ya mwl. ilionekana mwa matendo yake, kama bon mwaitege alivyotuimbia. matendo... jamani matendo..... tafuta hiyo single mkuu utanisoma ninachomaanisha.
   
Loading...