Tuache kumlaumu Mwl. Nyerere! Kosa ni la kwetu wenyewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuache kumlaumu Mwl. Nyerere! Kosa ni la kwetu wenyewe!

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by eedoh05, Jun 15, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Inasikitisha kuona baadhi ya watu wakibedha uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. J.k. Nyerere kwamba alikuwa mbaguzi kwenye suala/tasinia ya elimu. Binafsi, naona ni kumvunjia hadhi na heshima hayati Mwl. Nyerere kwa mazuri aliyoyafanya kwa watanganyika. Tukumbuke kwamba kabla ya uhuru wa Tanganyika na baada ya uhuru sekta ya elimu ilikuwa ya kibaguzi; ililenga makundi mahususi ya watu. Ilizingatia udini na matabaka yaliyokuwepo wakati huo.

  Tabaka la udini lilikuwa bayana kabisa. Madhehebu ya Kikatoliki kupitia mashirika yake mengi ndio walikuwa na shule nyingi za msingi, sekondari na hata vyuo vya ufundi. Madhehebu mengine kama waluteli na waanglikana hakuwa nyuma. Kundi jingine ilikuwa ni wahindi ambao walikuwa na shule chache maeneo ya mijini.

  Wajerumani walipoanza kuitawala Tanganyika miaka ya 1880, gavana wao wakati huo Von Soden alitoa ruzuku kwa shule za misheni. Lengo ilikuwa kupata watu wachache watakao saidia utawala katika kazi zao za kila siku. Hadi kufikia 1911 serikali ya kikolloni ilikuwa na shule 83 na wamishenari walikuwa na shule takribani 918. Shule za serikali zilikuwa na wanafunzi 3,000 na missheni wanafunzi 65,000. Waingereza nao baadaye kuanzia 1918 wakaendeleza ya wajerumani kusaidia shule za misheni. Hawa wakawa waandalizi wa kuwaandaa watanganyika kupata uhuru wao. Wakaanza, kama wajerumani, kuwaandaa watanganyika wachache kushika madaraka ya nchi. Na ilikuwa ni kupitia elimu ya kimaghariibi tu kwamba watanganyika wangejitawala.

  Kwa mantiki hiyo, ni wazi kuwa watawala waliondaliwa na wakoloni wangetokea maeneo yale ambayo wamishenari wa kikristo walishajijenga na kuanzisha shule. Hapa ina maanisha kwamba watu kutoka Kilimanjaro, Arusha, Kagera, Mara, Ruvuma na Mbeya ndio waliokuwa wakipewa nafasi ya kuwa watawala wa Tanganyika huru.

  Baada ya uhuru mfumo huu ulionekana wazi ni wa kibaguzi. Mathalan, wamishenari wengi walijikita katika maeneo muhimu kiuchumi. Wakajenga makanisa na shule mikoa ya kaskazini, Kilimanjaro,Arusha. Kanda ya ziwa Kagera. Na kusini wakajenga Iringa, Mbeya,Ruvuma nk. Maeneo mengi ya pwani hawakujihusisha sana. Huko walibaguliwa na hawakupendwa sana na waislamu ambao walikuwa wengi maeneo hayo.

  Kwa hiyo, baada ya uhuru Mwl. Nyerere akaona ipo haja ya kufuta mfumo huo wa kibaguzi kielimu. Kupitia sera ya ujamaa na kujitegemea (1967)Mwl. Nyerere akataifisha shule na vyuo vyote vilivyokuwa vya wamishenari. Hapa akatoa haki kwa watanzania wote kupata elimu sawa. Kufikia mwaka 1977 Mwl. Nyerere akatangaza Elimu Kwa Wote (UPE) ndipo kila mkoa, kila wilaya, kila tarafa, kila kata kukawa na shule za msingi. Watoto waliofikia umri
   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Mohamed Said
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  naona inatofautiana na ya mwalimu wetu hunga kapungu.
   
 4. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Naomba nipate maoni kutoka upande wa wana JF:
  Nasikiliza Radio Imani hapa,hawa Maustaadh wanaamini kuwa Umaskini na matatizo waliyonayo yamesababishwa na Nyerere,naomba kuwauliza mambo yafuatayo:
  1.Awamu ya pili ya urais hapa nchini ilikuwa ya Mzee Mwinyi na Mshauri wa Uchumi alikuwa Mh Lipumba wao walirekebisha kitu gani katika makosa ambayo aliyafanya Nyerere?
  2.Awamu ya nne ni Mh Jakaya Kikwete ni mwenzao huyu,yeye amerekebisha kitu gani kibaya ambacho Mzee Mkapa aliwafanyia nyie waislamu?
  3.Zanzibar hakuna kiongozi hata mmoja Mkristo ambaye ameshawahi kutawala huko,mbona hatuoni maendeleo yoyote katika maeneo ya Zanzibar?
  Nahitajia Constructive ideas na sio matusi.
  Karibuni ma great thinkers!
   
 5. steveachi

  steveachi JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 4,129
  Likes Received: 1,732
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo kipindi cha ukoloni wa mwarabu nyerere aliwakataza wasijenge shule??
   
 6. m

  mishalejuu Senior Member

  #6
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wote tumesikiliza toka elimu bila mipaka. unataka nini tena mbona maswali hayo yamejibiwa vizuri na wana historia watalaam.
   
 7. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kila kitu Nyerere,ndo matatizo ya watu kukimbia vivuli vyao wenyewe
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmmhhh!
   
 9. MGANGA WA KIENYEJI

  MGANGA WA KIENYEJI JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NDUGU ZETU MNATUCHOSHA SANA. KILA SIKU TUNAELEZEA JAMBO HILO HILO. KWA UFUPI TU TAFUTA KITABU CHA Dr John Sivalon, ‘Kanisa Katoliki na Siasa Tanzania: 1953 -1985.

  YOU CAN ONLY HIDE THE TRUTH FOR SOME TIME, BUT HISTORY WILL REVEAL IT.

  ALHAJI MWINYI NA WENGINEO KAMA KIGOMA ALI MALIMA, WAMESAIDIA SANA KATIKA HALI YA WAISLAMU WALIOPO SASA. ILE NYIMBO YENU MAARUFU KUA WAISLAMU HAWAJA SOMA, NADHANI SASA IMESTOP. SASA NYIMBO MPYA NI UGAIDI. WALE LAYMEN WA KIKIRSTO TU BADO WANAFIKIRI BADO WAISLAMU HAWAJA SOMA. POLE SANA. WHAT YOU SEE IS JUS A FRACTION OF MUSLIM ELITES ACTIVITIES.

  THE DICE HAS ALREADY BEEN CAST. IT IS TOO LATE NOW TO STOP THE SUN FROM RISING.
   
 10. m

  mishalejuu Senior Member

  #10
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usisikitike, ufisadi unaowatesa watanzania aliutengeneza kuurithisha JK Nyerere....... jifunze historia kama huwezi fahamu sikiliza Iman FM, utangundua kuwa ni tofauti na tulivyofunzwa shuleni hapo zamani. true story kutoka kwa waliomkaribisha Julius Nyerere akitokea Tabora kuja Dar in the early 50s. Fumbuka ewe mtanzania ili tulikomboe taifa hili kutoka mikononi mwa mafisadi
   
 11. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sikilizeni radio imani msikie nyerere,wakristo,wakatoliki na chadema wanavyotukanwa
   
 12. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,179
  Likes Received: 1,260
  Trophy Points: 280
  Alizuia pia mikoa iliyokuwa na wasomi isipige hatua ili isije wazidi zaidi waliokuwa nyuma!
   
 13. Cheche Mtungi

  Cheche Mtungi JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,487
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Sasa mbona mlalamika kuwa Nyerere aliiwanyima haki ya ki elimu?leteni facts hapa mtuambia kuna hiki na kile sio mpige kelele tu.
   
 14. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,179
  Likes Received: 1,260
  Trophy Points: 280
  Imani FM radio ya Fitna na majungu TZ! inakumbusha jinsi radio moja ilivyohamasisha mauaji Rwanda, burudi na juzi kenya!! beware Radio imani inahubiri fitna tu!!
   
 15. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kama kuamka ndio kuua hata shule chache mlizonazo (mfano Kinondoni, Bondeni ya Arusha, Jabal-hilal n.k) basi endeleeni kuamka!

  By the same reasoning - on books I mean- tuchukulie kuwa Satanic Verses ni authoritative reflection ya uislamu?
   
 16. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yaani wewe ni mmbeya.Harusi yako lini.
   
 17. m

  mishalejuu Senior Member

  #17
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona hakuna matusi pale, yote yanaongelewa ni ukweli. wanatueleimisha mambo ambayo wengi hatuyafahamamu
  Umesikiliza vizuri? au huwezi tofautisha matusi na asiyo?
  Q
   
 18. m

  mishalejuu Senior Member

  #18
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la watanzania hasa wengi wa humu JF ni wanaiki tu..... hatuwezi kupiga hatua ya kimaendeleo kwa kufumbia macho mambo mabaya yaliyotokea nyuma na yanayoendela kutokea. Kwanini humu jamvini wengi ni washambiki wa CDM? simple reason ni kwamba wanaamini CDM can change the "power status quo" into a positive economically strong direction. Kama mnaamini hayo ni kwamba tukubali kuwasema mafisadi kwa majina ili waache ufisadi.... Iman FM is all about this? na si vinginevyo... hakuna uchochezi hapo..... kama mnafikiri ni hivyo then you are NOT READY to liberate this country! waongo!
   
 19. MGANGA WA KIENYEJI

  MGANGA WA KIENYEJI JF-Expert Member

  #19
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa ndugu yangu mbona huelewi. Tatizo lenu hata uwezo wa kuchanganua mambo hamuezi. Nisalimie ndalichako.
   
 20. MGANGA WA KIENYEJI

  MGANGA WA KIENYEJI JF-Expert Member

  #20
  Oct 14, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  So low man. Kwahiyo, hivi unafikiri Wasomi wa Kiislaamu wamesoma shule hizo. Je hizo ndio shule zotee unazo zijua za kiislamu. How do u judge a book? Satanic verse is just an insult on the islamic faith. Dr. Sivalon book was written in the life time of julius nyerere himself. Even in his life time never a single day, Nyerere or Catholic Church denied what is written in the book.

  Matusi ni tofauti na ukweli. Au jaribu kuuliza nini kimewatokea Balozi wa Marekani nchini Libya na Makondoo wake wanao mlinda baada ya Marekani kuruhusu na kuto kukemea filamu iliokusudiwa kumkashifu Mtume Muhamad (s.w.a). Hata wewe unaweza kutokana yeyote unae mtaka kumtukana. Then ni juu ya ulie mtukana kujua nini cha kukufanya.

  Lakini sisi waislamu hua tunajadiliana kwa hoja, sio matusi.

  Kwa mfano. Yesu sio Mungu, Mungu sio watatu na Yesu ni mwana wamungu kama walivyo wachamungu wengine.

  Tunatoa hoja kwa kutumi biblia hiyo hiyo.

  Kwa mfano. Yesu anaposema Mungu wangu Mungu wangu mbona unaniacha. Hapo nani ni Mungu sasa?

  So mnaweza kukimbilia mtusi na kejeli, lakini kwa watu wenye akili timamu hata siku moja hawawezi kusema 1+1+1 = 1.
   
Loading...