Tuache kujibagaza, tukitaka kuwa wazalendo wa kweli tutafute suluhu ya kudumu dhidi ya mkulima Steyn

Kuhusu kuzuiliwa kwa ndege yetu huko Canada, swali la msingi la kujiuliza ndege zetu zitaendelea kuzuiliwa hata lini? Hii ni ndege ya 3 tangu zimeanza kuzuiliwa.

Ya kwanza ilizuiwa Canada kufuatia kesi iliyofunguliwa na kampuni ya ukandarasi ya Sterling Construction and Engineering Ltd (SCEL), nyingine ilizuiliwa Afrika Kusini kufuatia kesi iliyofunguliwa na mkukima Hermanus Steyn, na huyohuyo ndiye amezuia tena ndege hii ya sasa.

Tukitaka kuwa WAZALENDO wa kweli tutafute suluhu ya kudumu ya tatizo hili. Nimemsikiliza Prof.Kabudi akiongea na Rais JPM kwa kujibagaza kama kawaida yake. Akijitutumua na kuongea kwa tashwishwi na tamathali nyingi za semi, lakini hajatoa suluhisho la kudumu, badala yake ameishia kumpotosha Rais.

Kabudi ameongea kana kwamba tatizo la msingi ni Canada, na amefanikiwa kushawishi watanzania waamini hivyo. Akafika mbali na kusema alimuita Balozi wa Canada na kumwambia eti serikali imekasirika sana (hii kauli ya kifutuhi tuipuuze. Tuhesabu tu kwamba Kabudi alitaka kufurahisha umati kama kawaida yake).

Lakini je tatizo ni Canada. Jibu ni HAPANA. Tatizo si Canada, si Afrika kusini, wala si Chato. Tatizo la msingi ni kesi zilizofunguliwa dhidi ya serikali na serikali kuangukia pua. Kwa hiyo badala ya kudeal na Canada tudeal na kesi hizo. Unless otherwise ndege zetu zinaweza kukamatiwa hata Burundi.

Kwa mfano kesi iliyoshikilia ndege kwa sasa ni ya mkulima Hermanus Steyn. Huyu alikua mlowezi aliyemiliki mashamba makubwa sana ya kilimo mkoani Arusha. Mwaka 1982 serikali ya Nyerere ikataifisha mashamba yake, magari yake 250, ndege ndogo 12, mifugo na majengo.

Akafungua kesi mahakamani hapahapa nchini akidai fidia ya $36M. Mahakama kuu ya Tanzania ikampa ushindi na kumgrant "tuzo" hiyo ya $36M. Serikali ikasema haiwezi kumlipa pesa zote hizo. Ikaunda kamati maalumu ya kufanya tathmini ya mali zilizotaifishwa. Kamati hiyo iliongozwa na Mzee Chenge na Mkulo, ikapendekeza alipwe $20M kinyume na "tuzo" aliyopewa na mahakama ya $36M.

Serikali ya Rais Mwinyi ikamlipa $20M kama ilivyopendekezwa na kamati ya akina Chenge. Wakati huo sarafu yetu bado ilikua na nguvu. $20M zilikua kama TZS 44M hivi kwa wakati huo. Mkulima Steyn akapewa lakini hakuridhika. Akaendelea kudai kiasi kilichobakia. Na amekua akidai tangu wakati huo hadi sasa bila kulipwa. Kiasi kilichobakia kilikua $16M lakini kutokana na kukaa kwa muda mrefu pamoja na riba kimefika $33M, sawa na TZS 70 Bilioni kwa sasa.

Serikali ya Tanzania ilipoona anasumbua sana kudai fedha hizo ikampiga marufuku kukanyaga ardhi ya Tanzania. Steyn akaona atapoteza haki yake. Akachukua hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa ushindi na kwenda kusajili tuzo yake katika Mahakama ya Afrika kusini. The Arbitration act, cap.15 inamruhusu kufanya hivyo.

Akaomba mali za serikali ya Tanzania zilizopo Afrika kusini zikamatwe ili kufidia deni lake. Kifungu cha 30 cha sheria hiyo kinatoa masharti ya kufanya hivyo (conditions for enforcement of foreign awards). Na ndipo ndege yetu aina ya Airbus A220-300 ilipozuiwa nchini humo.

Lakini ikaachiwa baada ya mahakama ya Guateng kujiridhisha kuwa Hermanus alikosea kusajili "tuzo" yake mahakamani hapo (procedural irregularities). Sasa mkulima huyo amesajili "tuzo" hiyo nchini Canada, na ndio maana ndege yetu nyingine imekamatwa.

Jambo ambalo Kabudi anapotosha kwa makusudi ni kusema kuwa tulimshinda mkulima Hermanus Steyn on merit. Uongo mtupu. Kama tulishinda on merit why the matter is not res judicata?

Hatukumshinda Steyn on merit. Yani hatukumshinda katika kesi ya msingi ya kutaka alipwe fedha anazotudai. Tulimshinda kwa "technicalities" za kisheria (procedural irregularities) baada ya yeye kukosea kusajili tuzo hiyo kwenye mahakama ya Guateng.

Kwa lugha rahisi ni kwamba Hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyompa Hermanus tuzo ya $36M bado haijabatilishwa. Na Hermanus anaweza kuisajili tuzo hiyo katika nchi yoyote ya Jumuiya ya madola. Kwahiyo hata ndege ikiachiwa Canada, anaweza kusajili tuzo yake India, Kenya, Zambia, Australia, au nchi yoyote yenye mali za Tanzania zinazoweza kufikia thamani ya tuzo hiyo, na mali hizo kukamatwa.

Kwahiyo Kabudi anapoishangaa Canada, ni kukosa umakini tu. Ameongea kama "layman" ambaye hajui sheria kabisa. Vijana wa LLB1 pale UDSM, Mzumbe au SAUT wanamshangaa.

Mali zetu zimekamatwa zaidi Canada kwa sababu ndio nchi yenye mali nyingi za Tanzania kwa sasa (ndege zote za Bombadier zinatengenezwa huko). Hata Brazil ambapo Kabudi anashauri tukanunue ndege, zinaweza kukamatwa pia kama Steyn akiamua kwenda kusajili tuzo yake kwenye mahakama za huko.

Hivyo basi tunahitaji kupata suluhisho la kudumu badala ya kupiga 'ngonjera' kwamba kuna watanzania wanatumiwa na mabeberu kutuhujumu. Hakuna cha "beberu" wala "mbuzi jike" anayetuhujumu, ni makosa yetu wenyewe. Tutafute mbinu za kuyatatua badala ya kujificha kwenye visingizio vya mabeberu. Na tusimpotoshe Mheshimiwa Rais.

Nini kifanyike?

1. Serikali imuondolee mkukima Hermanus Steyn marufuku iliyompiga ya kuingia nchini. Ikumbukwe anahangaika huko nje kwa sababu amezuiwa kuja nchini. Kabla hajapigwa marufuku ya kuja Tanzania alikua anakuja kudai haki yake hapa. Alipozuiwa ndipo akaamua kuichukua "tuzo" yake mahakama kuu na kwenda kuisajili huko nje.

2. Kamati ya Chenge na Mkulo iitwe na kuulizwa msingi wa kupendekeza Steyn alipwe kiasi kidogo tofauti na "tuzo" aliyopewa na mahakama kuu. Kama sababu hizo zitakua na mashiko, zitumiwe kumshawishi Steyn akubali kiasi alicholipwa na kufuta shauri hilo mahakamani.

3. Kama serikali haikubaliani na option hizo mbili hapo juu, basi ikate rufaa au iombe "judicial review" kupinga hukumu iliyotolewa na mahakama kuu ya kumpa Steyn tuzo ya $36M. Na maamuzi yatakayotolewa kwenye rufaa hiyo yaheshimiwe na pande zote mbili.

Vinginevyo tutaishia kuwalaumu "mabeberu", kesho tutawalaumu "majogoo", keshokutwa tutawalaumu "mitetea" pasi na sababu zozote za msingi. Kama mkulima huyu kudai haki yake ni ubeberu basi Mahakamu kuu ya Tanzania ndio beberu kuu maana ndiyo iliyompa ushindi wa tuzo hiyo. Tuache porojo. Tudeal na msingi wa tatizo.

Tuanzie na sababu za Nyerere kutaifisha mali za Steyn, kisha twende kwenye hukumu iliyotolewa na mahakama kuu na kumpa ushindi. Then tumalizie na ripoti ya kamati ya akina Chenge. Halafu tumuite Steyn tukae nae mezani tuyamalize. Tuache kurukaruka kama maharage yaliyokosa maji.!

Malisa GJView attachment 1270915

Hawa ndio tunaowategemea
 
Umeweka akili matakoni. Huyu jamaa kazuiliwa lipwa awamu hii hata kuingia awamu hii
Kwanini uzuiaji wa mali za Tanzania umeanza awamu hii ya 5?

awamu zingine alikua wapi maana hajafungiwa kuingia nchini awamu hii
 
Umeandika pumba nyingi badala ya kujibu hoja ,kwani asimkosoe profesa amekuwa Mungu?
Hajitambui kabisa. Ndiyo maana wenye akili wanamuuliza kamungu kake kasheria kabudi kwanini anailaumu Canada? Anashindwa kujibu.
 
Mshana.
Wakati mwingine ni vizuri kukushauri vizuri ili uelewe namna nchi zinavoendeswa.
Maelezo yako yapo kama vile hata ww huelewi maana ya sovereign state. Hujui kuwa nchi inapofanya biashara na makampuni ya nchi fulan, basi ni issue ya uhusiano wa serikali mbili. Wenzetu wamarekan wanajua sana haya mambo. Huwezi kuharibu biashara yoyote ya kampuni ya kimarekan halafu serikali ya marekan ikakuacha salama. Au uhusiano na nchi hiyo ukaendelea kuwa salama.

Suala la ndege zetu kuzuiliwa kule Canada linaleta maswali kuhusu uhusiano wa serikali ya Tanzania na Canada au uwezo wa serikali ya Canada. Kama una kumbukumbu nzuri sisi tulivozuia makinikia ni serikali ya Canada iliyoingilia kati kupitia balozi wake ingawa ugomvi ulikuwa na kampuni ya uingereza.

Ukitumia akili kidogo unaweza kuona kuwa kuna hatari ya kuharibu biashara ya kampuni ya bombadia na pengine kwa makampuni yote ya canada yanayo fanya biashara na nchi za kusin mwa Africa.

Hakuna nchi ambayo haidaiwi hapa Dunian. Marekan inadaiwa tena na makampuni. Mengine ya ndan na mengine ya nje. China pia wanadaiwa na nchi zote Dunian. Nchi za kiafrica ndo usiseme mpaka zingine zimekuwa hazikopesheki na zimeshindwa kabisa kulipa madeni.

Lakin huu utaratibu wa kukamata ndege au mali za serikali ni utaratibu ambao unaweza kuvunja uhusiano wa nchi na nchi kabisa. Unaweza kuleta mvurugano sio tu ndan ya nchi bali hata Dunian.

China inazidai nchi kadhaa lakin unasikia kuwa inafanya makubaliano ya kuachiwa vitega uchumi fulan fulan ili iweze kuviendesha na ku recover deni lake. Haina maana kuwa china imeshindwa kukamata ndege na baadhi ya mali za nchi inazozidai.

Haijafanya hivo kwa sbb watakapoanza kufanya hivo watakuwa wameharibu uhusiano na nchi kadhaa. Watavunja na kuua biashara za makampuni yao. Itakuwa ni kiama kikubwa kwao.

Lakin wenye akili Wanajua na wanatilia shaka uhusika wa serikali ya canada kwenye ku facilitate au ku intertain au kujaribu kuitisha serikali ili isiyasumbue makampuni yao yanapokuwa yanaiba mali zetu.

Katika hali kama hiyo ni vizuri kuonyesha wazi kuwa serikali haitishwi na hatua hizi zinakera kidogo na wanamashaka na uhusika wa serikali ya Canada. Kama unakumbukumbu vizuri Tanzania ilishawahi kuvunja uhusiano na uingereza. Hata Canada sio kitu cha ajabu kuvunja uhusiano nao na kuwatimua nchin.

Lakin ni kitu ambacho hakiingii akili kuona serikali ya nchi kubwa kama Canada kuanza kushirikiana na watanzania wachache kuihujumu nchi. Hii tu ikishakuwa proved ni sababu tosha kuvunja uhusiano nao na pengine kuzishawishi nchi za kusini mwa jangwa la sahara kuikomalia Canada.

Mimi binafsi naona wazi kabisa kuwa kuna ukakasi mkubwa kwenye kuzuiliwa kwa ndege yetu hasa baada ya kuahirisha kuifanyia testing ya mwisho mara kadhaa na baadae kuja kuambiwa et ndege imekamatwa. Ni lazima serikali ipige kelele kuilaumu serikali ya Canada na Dunia isikie . kama tuliweza kumfukuza baloz wa umoja wa ulaya na akaondoka na hata baada ya umoja wa ulaya kupiga kelele hatukuyumba ndo iwe kwa canada!??.

Serikali ichukue hatua stahiki. Na kama kuna watanzania wanashiriki basi adhabu kali ichukuliwe dhidi yao.
 
Mshana.
Wakati mwingine ni vizuri kukushauri vizuri ili uelewe namna nchi zinavoendeswa.
Maelezo yako yapo kama vile hata ww huelewi maana ya sovereign state.
Serikali ichukue hatua stahiki. Na kama kuna watanzania wanashiriki basi adhabu kali ichukuliwe dhidi yao.
ndio tatizo la kusoma nusunusu, uka PANIC na kujibu kireefu hii taarifa ni Copy & Paste
sio Mshana J jamani mbona imejieleza hapo chini ya Mada kuwa ni Malisa GJ
 
Kwenye suala la picha, body language hutazamwa ktk mazunguzo laivu au ktk video ya wanaoongea.
Ingawa una hoja kiasi fulnk, ila kuna nguvu ya ziada unaitumia pia ktk kupotosha.
Ulichoona ni picha tu! ila kwa sababu huna akili timamu hukuona maandishi wala ujumbe.
 
Maandishi yapi, hiyo plagiarism anayofanya au!?
Kama ni rahisi ku copy weka na wewe tuone!! Jamaa ni Critical Thinker na ndio maana huwa anatolea ufafanuzi kwa mambo ambayo watanzania wengi hawayaelewi au kupotoshwa,pitia page yake uone mambo mengi aliyotolea ufafanuzi ili hali waTZ wengi tulikuwa tunaingizwa chaka kwahiyo hauwezi kusema ni plagiarism.
 
Mshana.
Wakati mwingine ni vizuri kukushauri vizuri ili uelewe namna nchi zinavoendeswa.
Maelezo yako yapo kama vile hata ww huelewi maana ya sovereign state. Hujui kuwa nchi inapofanya biashara na makampuni ya nchi fulan, basi ni issue ya uhusiano wa serikali mbili. Wenzetu wamarekan wanajua sana haya mambo. Huwezi kuharibu biashara yoyote ya kampuni ya kimarekan halafu serikali ya marekan ikakuacha salama. Au uhusiano na nchi hiyo ukaendelea kuwa salama.

Suala la ndege zetu kuzuiliwa kule Canada linaleta maswali kuhusu uhusiano wa serikali ya Tanzania na Canada au uwezo wa serikali ya Canada. Kama una kumbukumbu nzuri sisi tulivozuia makinikia ni serikali ya Canada iliyoingilia kati kupitia balozi wake ingawa ugomvi ulikuwa na kampuni ya uingereza.

Ukitumia akili kidogo unaweza kuona kuwa kuna hatari ya kuharibu biashara ya kampuni ya bombadia na pengine kwa makampuni yote ya canada yanayo fanya biashara na nchi za kusin mwa Africa.

Hakuna nchi ambayo haidaiwi hapa Dunian. Marekan inadaiwa tena na makampuni. Mengine ya ndan na mengine ya nje. China pia wanadaiwa na nchi zote Dunian. Nchi za kiafrica ndo usiseme mpaka zingine zimekuwa hazikopesheki na zimeshindwa kabisa kulipa madeni.

Lakin huu utaratibu wa kukamata ndege au mali za serikali ni utaratibu ambao unaweza kuvunja uhusiano wa nchi na nchi kabisa. Unaweza kuleta mvurugano sio tu ndan ya nchi bali hata Dunian.

China inazidai nchi kadhaa lakin unasikia kuwa inafanya makubaliano ya kuachiwa vitega uchumi fulan fulan ili iweze kuviendesha na ku recover deni lake. Haina maana kuwa china imeshindwa kukamata ndege na baadhi ya mali za nchi inazozidai.

Haijafanya hivo kwa sbb watakapoanza kufanya hivo watakuwa wameharibu uhusiano na nchi kadhaa. Watavunja na kuua biashara za makampuni yao. Itakuwa ni kiama kikubwa kwao.

Lakin wenye akili Wanajua na wanatilia shaka uhusika wa serikali ya canada kwenye ku facilitate au ku intertain au kujaribu kuitisha serikali ili isiyasumbue makampuni yao yanapokuwa yanaiba mali zetu.

Katika hali kama hiyo ni vizuri kuonyesha wazi kuwa serikali haitishwi na hatua hizi zinakera kidogo na wanamashaka na uhusika wa serikali ya Canada. Kama unakumbukumbu vizuri Tanzania ilishawahi kuvunja uhusiano na uingereza. Hata Canada sio kitu cha ajabu kuvunja uhusiano nao na kuwatimua nchin.

Lakin ni kitu ambacho hakiingii akili kuona serikali ya nchi kubwa kama Canada kuanza kushirikiana na watanzania wachache kuihujumu nchi. Hii tu ikishakuwa proved ni sababu tosha kuvunja uhusiano nao na pengine kuzishawishi nchi za kusini mwa jangwa la sahara kuikomalia Canada.

Mimi binafsi naona wazi kabisa kuwa kuna ukakasi mkubwa kwenye kuzuiliwa kwa ndege yetu hasa baada ya kuahirisha kuifanyia testing ya mwisho mara kadhaa na baadae kuja kuambiwa et ndege imekamatwa. Ni lazima serikali ipige kelele kuilaumu serikali ya Canada na Dunia isikie . kama tuliweza kumfukuza baloz wa umoja wa ulaya na akaondoka na hata baada ya umoja wa ulaya kupiga kelele hatukuyumba ndo iwe kwa canada!??.

Serikali ichukue hatua stahiki. Na kama kuna watanzania wanashiriki basi adhabu kali ichukuliwe dhidi yao.
Mkuu unaweza kufafanua hapo uliposema test ziliahirishwa?! Una maana walikuwa wanaichelewesha ili wapate amri ya mahakama?
 
Hapo nmeelewa sabab ya mkulima kutudai, bado nasubir sababu ya nyerere kumpokonya mali.
Nahisi ilikuwa ni kipindi cha kuelekea UHUJUMU UCHUMI km utamkumbuka Mar E M Sokoine 1983
hebu anza na hii wakati tukirejea nyuma zaidi kutafuta Kisa kingine lkn kumbuka Hukumu ilitolewa na Mtanzania Jaji R.V. Makaramba Wakili wake ni Mtanzania Erick Namaryo ni Watanzania km Steyn mwenyewe, leo Prof P Kabudi atamtafutaje Mbaya wetu? ni haki itafutwe kkm Jaji alivyoamua

Kabla ya kukamatwa ndege

Mwaka 1983 kupitia Kifungu cha 3( 1 ) cha Sheria iliyoitwa Acquisition and Transfer Management Act, 1983 kampuni sita za Mzungu Hermanus Steyn ambazo ni Rift Valley Seed Ltd, Hashman Estate Ltd, Lente Estate Ltd, Loldebbis Ltd, Mayoka Estate Ltd na Tanganyika Air Ltd zilitaifishwa na Serikali ya Tanzania.

Baadaye Steyn alifungua malalamiko kwenye taasisi ya usuluhishi (arbitration) akiomba haki zake zote katika kampuni zote zilizotaifishwa, jambo ambalo alifanikiwa mbele ya Jaji R.V. Makaramba aliyeamua alipwe Dola za Marekani 36,375,672.81 (Dola milioni 36).

Muda ukapita, lakini baadaye Mei 2011 Mzungu huyo akaamua kuisajili hiyo hukumu ya taasisi ya usuluhishi katika Mahakama Kuu ya Biashara ili iwe hukumu ya mahakama, hivyo iweze kutekelezeka.

Julai 2012 wakati akiwa katika mchakato wa kufuatilia utekelezaji, serikali na Mzungu huyo wakaingia makubaliano kuwa aachane na hiyo hukumu ili imlipe Dola za Marekani 30,000,000 ( Dola milioni 30) badala ya zile 36,375,672.81 zilizoamuliwa awali.

Mzungu akakubali na makubaliano yakasainiwa, na makubaliano hayo yakasajiliwa na mahakama, hivyo yakasimama kama hukumu mpya ya mahakama.

Kufikia Machi 2016, serikali ikawa tayari imemlipa Mzungu huyo Dola za Marekani 20,099,155.12 (dola milioni 20).

Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo, serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 Mahakama Kuu ya Biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua Mzungu kulipwa Dola za Marekani 36,375,672.81, kwa hoja kuwa ilikuwa na upungufu wa kisheria.

Desemba 2018, Jaji B.K. Philip alitoa uamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo, kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na Mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani, hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.

Katika maombi hayo serikali iliwakilishwa na Wakili Jacqueline Kinyasi, wakati Steyn aliwakilishwa na Wakili Erick Ng’maryo.

Hoja kuu ya Wakili Erick hapo mahakamani ilikuwa kwamba uamuzi wa taasisi ya usuluhishi (arbitration) ulishakufa na haupo, na kuwa uamuzi huo uliuliwa na makubaliano kati ya mteja wake na serikali, ambapo makubaliano hayo nayo yalisajiliwa yakawa hukumu mpya ya mahakama, hivyo serikali kuiomba mahakama ifanye marejeo ya hukumu hiyo ya awali ni sawa na kuiomba irejee kitu ambacho kilishakufa na hakipo.

Mahakama ilikubali hoja hii ya Wakili Erick na kumpa ushindi kwa hoja hii. Kumbuka huyu Erick ndiye anayetajwa kuongoza mchakato wa kuzuiwa kwa Airbus Afrika Kusini.
@kajekudya
 
Kama ni rahisi ku copy weka na wewe tuone!! Jamaa ni Critical Thinker na ndio maana huwa anatolea ufafanuzi kwa mambo ambayo watanzania wengi hawayaelewi au kupotoshwa,pitia page yake uone mambo mengi aliyotolea ufafanuzi ili hali waTZ wengi tulikuwa tunaingizwa chaka kwahiyo hauwezi kusema ni plagiarism.
Naandika Sana na maandishi yangu Kuna kipindi mlikuwa mnayalipia whattap, na Kuna mengine yaliwahi kuibwa huko na kuletwa humu watu wakidai ni yao. No doubt on than uliza kingine. Na hapo mwisho nasisitiza ni mbumbumbu Kama wewe tu anayeweza kukubaliana na Bwana Mnafu dhidi ya Prof. Kabudi kwenye swala la kisheria, nasisitiza ni Mpumbavu pekee!
 
Kumbe serikali inatumia mkono wa chuma kudeal na wapinzani? Na linakufurahisha?
Tatizo kubwa ni kuwa wengi waliyo na mawazo kama Malisa wanataka na kuombea Serikali ya awamu ya tano ishindwe kwa kila jambo itakalofanya. Mtu akishakuwa na kitu kama hicho moyoni, hawezi kueleweshwa chochote akaelewa. Na mbaya zadi hawajui kuwa hayo wanayoombea yatawaathiri wao na ndugu zao. Hata kama mtu hakubaliani na uongozi wa Magufuli lakini kuombea mabaya yaipate nchi yetu ni uhayawani na ubinafsi wa hali ya juu. Jambo la kijinga kama hili linanifanya hata mimi nifurahi ninapoona serikali inatumia mkono wa chuma ku deal na wapinzani wake.
 
Naandika Sana na maandishi yangu Kuna kipindi mlikuwa mnayalipia whattap, na Kuna mengine yaliwahi kuibwa huko na kuletwa humu watu wakidai ni yao. No doubt on than uliza kingine. Na hapo mwisho nasisitiza ni mbumbumbu Kama wewe tu anayeweza kukubaliana na Bwana Mnafu dhidi ya Prof. Kabudi kwenye swala la kisheria, nasisitiza ni Mpumbavu pekee!
Ndio maana Malisa alisisitiza kwa wenye akili timamu tu ila kama haujamuelewa bandiko lake ni wazi kwamba HUNA AKILI kama Prof wako wa MAJALALANI.
 
Ndio maana Malisa alisisitiza kwa wenye akili timamu tu ila kama haujamuelewa bandiko lake ni wazi kwamba HUNA AKILI kama Prof wako wa MAJALALANI.
Nyie ndio vilaza, Kama unaamini Malisa ni great thinker basi wewe akili yako inakuwezesha tu kuvuka barabara. Kwa ufupi hapo kwenye legal aspect ya kilichotokea South Africa na kesi kufaunguliwa tena Canada, amechemka, kwenu Mbumbumbu mnaona kapatia ila wanaojua wanacheka kwa dharau, hasa pale degree ya Mbege inapotaka kuingia kwenye mambo ya sheria. Mtafute akufanunulie hiyo sijui Resjudicata, akueleze applicability yake na aifafanunue in respect ya kile kilichotokea South Africa na what is likely to happen kwenye kesi mpya Canada. Shida most of you uwezo wenu wa kuchakata Mambo ni mdogo ndiyo maaana ni rahisi Sana kufanyiwa propaganda na mkaingia kichwa kichwa. Yaani ni kichekesho Prof. Wa sheria aseme hiki kiko hivi, halafu mtu mwenye degree ya Mnafu aje apinge alichosema Prof. Wa sheria na watokee vilaza waungane na Mr. Mnafu, halafu wazungu wakiwaambia nyie mabwege mnalalamika.
 
Sasa nyie wenye uwezo na kujitapa mmeshinda kesi south mbona styne kawanyoosha tena? Ni jinsi gani inaonyesha mlivyo zero brain prof wa majalalani kaja kawalisha matango pori mkamuamini kweli kesi imeisha hahahaaaa LIPENI DENI.
 
Nyie ndio vilaza, Kama unaamini Malisa ni great thinker basi wewe akili yako inakuwezesha tu kuvuka barabara. Kwa ufupi hapo kwenye aspect ya kilichotokea South Africa na kesi kufaunguliwa tena Canada, amechemka, kwenu Mblegal umbumbu mnaona kapatia ila wanaojua wanacheka kwa dharau,
mbona bado unajichanganya Mkuu
Hapahapa Tanzania serikali ilishindwa Kesi hiyo mwaka jana 2018 ikaambiwa imlipe pesa yote, mbona unarukia ya Canada na South Africa? anza na Majaji wazalendo ndio uwaite wapumbavu
Mwaka 2018 wakati malipo yanaendelea kidogo kidogo, serikali ikasitisha malipo na kufungua maombi namba 168/2018 Mahakama Kuu ya Biashara Tanzania. Ikawa inaiomba mahakama iifanyie marejeo hukumu ya taasisi ya usuluhishi iliyoamua Mzungu kulipwa Dola za Marekani 36,375,672.81, kwa hoja kuwa ilikuwa na upungufu wa kisheria.

Desemba 2018, Jaji B.K. Philip alitoa uamuzi kwa kukataa maombi ya serikali ya kuifanyia marejeo hukumu hiyo, kwa hoja kuwa hukumu hiyo haipo na ilishakufa baada ya serikali na Mzungu kuamua kuelewana na kuyasajili maelewano hayo mahakamani, hivyo kuyafanya maelewano hayo kuwa hukumu mpya.
 
kuna siku Zero IQ alianzisha uzi kuhusu madeni nilikua sijui babu mkulima anadai mahela yote hayo,by the way umakini unahitajika kwenye maamuzi mazito,waliotaifisha mali zake kama wangejua madhara yatakua hivi wasingegusa mali za mkulima.
 
Back
Top Bottom