Tuache kujadili watu Tujadili ni Sifa zipi kiongozi awe nazo!!!

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,392
3,201
Kadiri siku zinavyosonga kukaribia uchaguzi mkuu 2015 ndivyo watu wanavyojadili vyama na watu binafsi na kuacha mambo ya msingi.
Nafikiri tungejikita kujadili ni sifa zipi mgombea awe nazo.
Mfano ni vp mgombea anauwezo wa kuziba nyufa ktk taifa letu, zipo nyufa kama matabaka ktk Elimu, Afya pamoja na huduma zitolewazo katika nyanja hzo.
Ufisadi, Dawa feki, Meno ya tembokuuzwa na majangili kila kukicha, Ufichwaji wa fedha nje ya nchi, Umilikaji sawa wa Ardhi, Utendaji mbovu kwa watumishi wa uma, Ukabila hasa kwenye suala zima la Ajira na UDINI. Hizo ni baadhi ya nyufa zinazolitafuna Taifa kwa sasa.
Pia akichanganya na weledi katika kusimamia Rasilimali za Taifa kwa manufaa ya wote hakika tutaweza kuwa na bandari za viwango vya juu, Reli kuunganisha jumuiya ya Afrika mashariki.
Akijumlisha uwezo wake wa usimamizi tutakuwa na shirika bora la ndege sambamba na viwanja bora angalau kwa kila Mkoa.
Uzalendo wake utatupatia barabara zilizobora, Nishati ya uhakika na Kilimo cha kibiashara.
Aweze kusimamia katiba safi na kujali demokrasi.
Hapo tunaweza kwa uchache kusema huyu ndiye MZALENDO anaeweza kuwa RAIS WA TANZANIA anayeweza kutukwamua hapa tulipokwama.
 

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,642
4,480
Mtu hawezi kuwa mzalendo kama anadanganya vitu rahisi kama umri, vyeti etc. Ndo maana mtu inabidi achimbuliwe kiundani zaidi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom