Tuache kugawa pepo kwa sms tu, peponi si mchezo

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
ACHA TABIA YA KUTUMA SMS NA KUSEMA FORWARD KWA WATUM KUMI ILI UINGIE PEPONI

God is seeing you!

Utasikia watu, eti, watumie watu 10 utaingia peponi. Au mambo yako yatakuwa mazuri, hivi mnadhani Pepo mchezo!

Yohana mbatizaj aliishi hadi mapangon kwa kula asali na nzige kwa ajili ya kuitangaza injil

Mtakatifu Yohana yule mwanafunzi wa Yesu, alikaangwa kwenye mafuta yanayochemka, baadae akatupwa kwenye kisiwa cha mateso cha patmo mpaka akafunuliwa mambo mazito na magumu

Isaya aliuwawa kifo cha kukatwa vipandevipande kwa msumeno wa kukatia mbao akiwa hai.

Stephano alipigwa kwa mawe mpaka akafa

Daniel alitumbukizwa kwenye tundu la simba sababu ya kuishindania imani

Yusuph ilimbidi kwenda gerezani kwa sababu ya kuulinda utakatifu wake, shedrack, meshack na abelnego walitumbukizwa kwenye tanuru liwakalo moto. Yote hii ni kwa sababu ya kuisimamia imani

Leo hii anatokea, mtu, kwa msg yake isiyo na mashiko wala vina alafu anakutisha, anakulazimisha utume kwa watu 10 maisha yako yatakuwa mazuri, au eti mm ni Yesu/Mtume Mohammad S.A.W nakuagiza tuma ndani ya dk 3.

Unadhani mbinguni ni kariakoo? kwa sms yako tu ukale bata mbinguni, halafu unategemea uingie Peponi, tusidanganyane, Pepo sio mas'hara ndugu yangu, sio maneno matupu na sms nyingi.

Tumche Mungu kisawasawa.

WAKUMBUSHE WANAOGAWA PEPO KWA SMS..
 
Meseji za dizaini hiyo huwa nazifuta haraka sana zikishaingia kwenye simu yangu, halafu nampa onyo mtumaji asinitumie tena meseji za aina hiyo. SIPENDAGI UJINGA MIMI
 
Ungechelewa ningeanzisha thread kama hii.. Subiria pingamizi za watu weny imani ya kuhamisha milima
 
Watu wanapoozana wakizani kuingia peponi ni rahisi hivyo unatakiwa ujikane nafsi ndo uingie peponi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom