Tuache kufurahia mizaha mpaka kwenye mambo Matukufu ya Mungu

Unajuaje mtu anapokufa "kukata roho" si msemo tu wa kuelezea kwamba huyu hayuko hai tena?

Unaweza kuthibitisha hiyo roho ipo kweli?

Unaelewa kwamba mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo wala roho ipo?
Mungu na Roho wake wanajifunua na kujithibitisha wenyewe kwa kazi wanazotenda ikiwa ni pamoja na uumbaji. Hivi ulishawahi hata kujiuliza origin ya binadamu kwamba alitokea tu by chance, au kuna Mungu Mkuu ambaye alihusika katika uumbaji wa binadamu na viumbe wengine? kwa hiyo wewe mwenyewe jinsi ulivyoumbwa kwa namna ya ajabu kabisa ni uthibitisho tosha wa uwepo wa Mungu...
 
Kwa nini unazungumziwa kuheshimiwa kwa vitabu vya Biblia na Quran tu? Kwa nini sio pamoja na Tripitaka cha wabudha?
Hata kama haina uhakika kwamba Mungu yupo lkn mtoa mada kaongelea sana heshima juu ya Biblia. Biblia ni kitabu inachopaswa kuheshimiwa sio tu kwa sababu ya kuwa na connection na mambo ya kimungu lkn kwa sababu ni kitabu chenye mafunzo mengi, historia na maadili katika jamii. Ni kama vile ukute mtu anachezea kitabu cha katiba ya nchi. Kama katiba tu ni kitabu kinachoheshimiwa sembuse biblia ambayo watu wanatumia kuweka viapo vya maadili na uaminifu kazini?


Hata tukisema Mungu hayupo lkn biblia bado ina nafasi yake kwenye kuheshimiwa kama kitabu kilichobeba mafunzo mbalimbali katika jamii.

Ndio maana kwa upande wangu nikimuona mtu analeta mzaha khs biblia au quran namuona hajielewi au ana matatizo ya kiakili coz ndivyo vitabu ambavyo asilimia kubwa ya viongozi wanatumia kutuaminisha kwa kuweka viapo kutumia hivyo vitabu.
 
Mungu ni nini? Unaweza kuthibitisha yupo kweli na si hadithi tu?
Acha kutumia neno THIBITISHA narudia tena uwezi kutumia platform kutibitisha uwepo wa mungu miaka nenda rudi Mungu Yupo imani yangu Ufahamu wangu unaniaminisha hivyo.
 
Acha kutumia neno THIBITISHA narudia tena uwezi kutumia platform kutibitisha uwepo wa mungu miaka nenda rudi Mungu Yupo imani yangu Ufahamu wangu unaniaminisha hivyo.

Mimi ni mtu huru. Sitaki unipangie neno la kutumia.

Kwa hiyo wewe unapenda mambo ambayo hayana uthibitisho?

Unajuaje kwamba ni ya kweli bila uthibitisho?
 
Mungu na Roho wake wanajifunua na kujithibitisha wenyewe kwa kazi wanazotenda ikiwa ni pamoja na uumbaji. Hivi ulishawahi hata kujiuliza origin ya binadamu kwamba alitokea tu by chance, au kuna Mungu Mkuu ambaye alihusika katika uumbaji wa binadamu na viumbe wengine? kwa hiyo wewe mwenyewe jinsi ulivyoumbwa kwa namna ya ajabu kabisa ni uthibitisho tosha wa uwepo wa Mungu...
Hujathibitisha Mungu yupo.

Hujathibitisha roho ipo.

Unahubiri tu.

Sitaki mahubiri.

Nataka uthibitisho.
 
je hao waliomuona wanaishi hadi sasa?

Unaelewa nini ukisoma "hakuna aliyepata kumuona" akaishi? Kwani hata huyo Yesu anaishi hadi sasa? Je, walioishi naye enzi zake hawakuweza kuishi!!

Au unakopi vifungu na kufowadi tu, na hapo kila wiki unalipa hela kusomewa vifungu na mchungaji... jipe muda ukiweza umuulize huyo unayemlipa sadaka akusaidie.
 
Mungu ni Muumba wako wewe na mimi, aliyeumba kila kitu ambacho jicho lako linaviona na vingine huvioni.Akatuamrisha tumuabudi yeye tu, hana msaidizi wala mshirika
yani tusifanye kazi tumuabudu yeye tu
 
mungu ni muumbaji na anajithibitisha mwenyewe kwa vile ambavyo binadamu hawezi kuviumba kama jua mwezi bahari ,sayari nk
Unajuaje Mungu ni muumbaji na yupo kweli, na kwamba hiyo si hadithi tu ya watu walioshindwa kujibu swali la jua, mwezi, bahari, sayari n.k vimetokeaje?
 
anavyotafuta uthibitisho nawewe thibitisha Mungu hayupo na roho haipo?
Kwanza kabisa, nje ya logic, kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Kwa sababu hakipo.

Unaweza kuthibitisha "sjgwaklqnsde" haipo?

Pili, logically Mungu anaweza kuthibitishwa hayupo kama akiwa defined.Unataka nithibitishe Mungu yupi? Hata hujam define Mungu unataka nithibitishe kitu ambacho huja define ni kitu gani?

The same gies for roho.

Define Mungu ni nini. Define roho ni nini. Then niambie nithibitishe havipo.
 
Roho ni nini? Unaweza kuthibitisha roho ipo kweli na si hadithi tu?

Kwa nini Mungu wako ahitaji watu wasome kitabu ili kumuelewa? Alishindwa kutupa uelewa wa kumuelewa yeye bila kusoma kitabu?

Uelewa wako unaishia kwenye ukomo wa uelewa wako, huwezi kuelewa zaidi ya uwezo wako.... na uelewa wako sio uelewa wa juu kuelewa kila kitu.

Kitu pekee unapaswa kuelewa, ni kuwa kuna watu wanaelewa zaidi yako... keep stretching uwezo wako wa uelewa.

Kiranga: Define uelewa ni nini na thibitisha uelewa upo!
 
niliomba nipate kazi jumapili kwa kufunga, jumatatu kesho yake nikapeleka maombi office fulani nikaambiwa nianze kazi week linalokuja.....wewe thibitisha kama hayupo?
kwahiyo umeajiriwa na Mungu.
 
Unajua binadamu pia ana roho, ndo maana mtu akifa wanasema amekata roho? ni roho ipi unayotaka nithibitishe hasa. Kama ni Roho wa Mungu nimeshaongelea hapo juu, ni hali wanayo experience wale waliojenga imani katika neno la Mungu na siyo jambo la kusimuliwa. Roho wa Mungu anakuwa manifested katika nguvu, uweza, mamlaka, miujiza na maajabu ambayo yako beyond human comprehension.
mtu akifa ni amekata pumzi,hiyo kukata roho ni porojo tu hakuna aliyewahi kuionahiyo roho ikikata
 
Back
Top Bottom