Tuache kudanganya watanzania na pima joto kama za kina Maggid Mjengwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuache kudanganya watanzania na pima joto kama za kina Maggid Mjengwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gokona, Sep 7, 2011.

 1. G

  Gokona Member

  #1
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu kamwe Tanzania haitapiga hatua kama wale wanaojiita wafikishaji taarifa kwa wananchi watafanya hivyo kwa ushabiki.

  Nimeona niliseme hili hasa kwa huyu ndugu yangu Mjengwa na pima joto yake feki tena yenye chembechembe za ukanda,ubaguzi na uchochezi maana Igunga hachaguliwi Rais wa Tanzania ila kinachofanyika igunga ni uchaguzi wa Mbunge sasa tuwaachie wana igunga ndio wanaojua chama gani kina maslahi kwao na chama gani kina taka nafasi hiyo kwa ajili ya ushabiki na si kwa maslahi yao.

  Sasa pima joto kama wanaopiga kura ni wa njombe, tarime, Arusha, Pemba, Mwanakwerekwe, Mchamba wima au Dole unaweza ukajiita wewe unafanya tafiti au ni akili mbaya ya kishabiki/ Tena mtu mzima anaendelea kusema kama CUF ingewaachia CHADEMA ingekuwa safi ili CCM apate wakati mgumu sasa mimi nasema kamwe huwezi kumnyonyoa jogoo manyoya ya kwenye mabawa yake na kumfunga miguu ukasema umemficha maana atawika na watu watajua pale pana jogoo kawekwa.

  Mjengwa na watu wa aina yake ni wauwaji wa demokrasia maana CHADEMA ni chama cha siasa kama vingine na ndio maana vinapata ruzuku ili wakati wa uchaguzi vishiriki na vishinde ili viunde serikali sasa wewe unataka CHADEMA ole wako na subiri kwa unavyojidanganya 2015 UNAPOTAKA KUCHUKUA FORM UGOMBEEUBUNGE SASA KWENYE ZA KURA ZA MAONI ZA CHADEMAkama hujaambiwa hapa kawe ni kwa MDEE,UBUNGO kwa MNYIKA,KIGOMA KWA ZITO,HAI KWA MBOWE,ndio peoples power utaijua nenda kaulize Uchaguzi wa CDM KILIMANJARO KWANI WALIOPO NI KINA NDESA PEKE YAO HAKUNA WENGINE?

  MBONA MWALIMU HAKUWAWEKA KINA JOSEPH NYERERE KWENYE NAFASI ZA CHAMA WAKAWEPO KINA AMIR JAMAL? AKILI KUMKICHWA.

  NA SASA TUNAPATA MAJIBU MAANA WATU WANAPANIA MAMLAKA NA SIO NIA NJEMA KWA TAIFA MAANA HATA DAVID BEKHAM AKITOKA UWANJANI ANAVUA JEZI NA AKIALIKWA HARUSINI ANAVAA MAVAZI YANAYOTAKIWA NA YANAYOENDANA NA MAHALI SASA UKISHAPANIA JAMBO ndio kama wanavyofanya.TUMESHAWAELEWA TUTAFANYA MASAHIHISHO TU.
   
 2. L

  Losemo Senior Member

  #2
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu, Najua kunyang`anywa tonge mdomoni kunauma sana, Umekuwa kama huelewi kitu kabisa, Alichofanya Mgengwa ni KIPIMA JOTO narudia KIPIMA JOTO, Sio lazima ufanye kipima joto pale tu unapokuwa mpiga kura wa pale. Katika nchi za wenzetu hicho ni kitu muhimu sana maana ni mara chache sana kubadilika. Kama wewe ni mdau kafunge mkanda utafute pa kutokea maana kengele ishalia
   
 3. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  duh! Nimetoka Kapa....
   
 4. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Naomba utuelezee kwa kifupi hadithi yako inazungumzia nini hasa.
  Yani mi naona maneno yanapiga tu sarakasi na kukanyagana.kama huna cha kuandika kaa kimya.
   
 5. W

  We know next JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Pole sana! inaonekana uwezo wako wa kupembua mambo si mpana sana kufahamu Mjengwa alikuwa ana maana gani! Nadhani ungemuuliza swali alikuwa ana maana gani, ingekuwa vyema kabla ya kuanza kujidhalilisha hapa jamvini.
   
 6. T

  Tata JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,734
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Nakushauri uvute pumzi na kutoa kama mara tatu hivi. Baadaye tulia kama dakika tano hivi kisha uandike upya. Kwani kwa jinsi ulivyoandika hujaitendea haki thread yako kwani ni vigumu sana kujua hasa ni ujumbe gani ulilenga kuufikisha.
   
Loading...