Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,549
Wasalaam wanajukwaa,
Naweza kudiriki kusema kwamba kuna mahali kama taifa tumeshiba sana tuna la amani na ulivyo na amani tuliyonayo ndiyo maana kikundi kidogo cha watu wachache wasiofikiria mbali hakioni aibu kumbambikia kiongozi mkubwa kesi mbaya ya ugaidi ilimradi tu akose dhamana akae mahabusu asifanye kile ambacho kinawakera wao. Ubinadamu imetoweka kabisa, huruma haipo tena mtu haoni taabu kumtesa mwenzake ili yeye atulie afanye atakacho.
Hii haiingii akilini wala haieleweki kwa mtu ambaye alishawahi kuhudhuria moja ya mahakama nchini Kenya kusikiliza kesi za ugaidi zinazowakabili watuhumiwa walioshukiwa kua ni Al-shaabab agents, hakika angaweza kuona kituko kinachofanyika nchini mwetu.Ugaidi anaojiapisha kwa Mungu IGP wa polisi ni wa kufadhiliwa kwa shilingi 600,000? Ugaidi ni wa kupanga kwa bastola yenye risasi 3? Yaani gaidi upangwe kwa Sabaya ambaye ana kesi za uporaji mahakamani hivi sasa?
IGP umeliharibu sana jeshi la polisi wala hakuna mtu atakayekuamini tena wewe, ndiye IGP pekee ambaye jeshi la polisi limetuhumiwa na mkuu wa nchi hadharani kua na kesi nyingi za kubambikizia. Hii maana yake IGP hana weledi wowote wala hofu ya Mungu hana anafanya mambo kuridhisha waliomteua.
Tuache kuchezea sheria za nchi kukomoana na kutesa watu ikiwa tumepewa mamlaka la kulinda raia na mali zao, tuheshimu mhimili wa mahakama kwa kupeleka kesi zenye uhalisia ili kuepusha usumbufu unaojitokeza matumizi ya rasilimali za umma bila sababu maana kuna mambo mengi ya kufanya ya kulijenga taifa.Tunajenga chuki itakayolitafuna taifa miaka nenda rudi kwa sababu ya tamaa za madaraka kwa watu wachache.
Mwalimu Nyerere aliijenga nchi hii kwa gharama kubwa kwa misingi ya utu wa kuheshimiana, kutanguliza busara na hekima. Hakujenga kukomoana na wala hakuliandaa taifa la watu wanaobambikiza watu kesi kwa tuhuma za kutengeneza. Tuheshimu sheria za nchi ili tuweze kujenga taifa imara na lenye nguvu kubwa.
Huwezi kujiaminisha kua wewe ndio wewe kwenye taifaa watu milion zaidi ya 60 wanaofikiri tofauti, siku wakikuchoka utaelewa haya nisemayo.