SoC04 Tuachane na itikadi ya uchumi wa amri au "command economy" ili tuelekee uchumi wa masoko huru au "free market economy"

Tanzania Tuitakayo competition threads

YNM

New Member
May 28, 2024
1
2
Habari Wanajukwaa wote!

Poleni na hali ya kimaisha ambayo tumekuwa tukiishi nayo kwa muda mrefu ambayo haikuwa na budi kutokea ila imefika wakati inabidi kuachana nayo kwa ustawi wa kila mmoja wetu ili kuendana na uchumi wa kudunia unaoendelea hivi sasa.

Rejea na kichwa cha andiko hili, nchi yetu ya Tanzania imejengwa kwa mfumo wa kijamaa katika nyanja za kiuchumi, kiutawala na kijamii. Mfumo huu umekuwa na matokeo chanya mengi miongoni mwao ni kuleta umoja na mshikamano miongoni mwetu kutokea kupata Uhuru wetu ambapo hatuna budi kuwa na shukrani kwa Waanzilishi wa mfumo huu.

Matokeo hasi ya sera ya uchumi wa amri;
Sera hii imedumisha maendeleo lakini ilibidi itumike mpaka Watanzania wote wapate elimu na maarifa. Hakuna shaka kwamba hilo limetimizwa kwa kiasi kikubwa.

Matokeo hasi ya sera ya uchumi wa amri ni;

(i) Kukosekana kwa ubunifu katika uzalishaji na utoaji huduma; Serikali imekosa watu walio na mawazo huru wa kusaidia utendaji kwasababu shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zimeshikiliwa na serikalii. Mfano katika uchukuzi wa anga Ripoti ya CAG inaonesha "Air Tanzania" inaingiza hasara karibu kila mwaka. Serikali imeingilia biashara ya korosho na pamba na kuleta changamoto lukuki bila kusahau shirika la TANESCO na kukatika kwa umeme.

(ii) Kuongezeka kwa vitendo vya rushwa; Sera ya uchumi wa amri haitabiliki hivyo wafanyabiashara na wawekezaji wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa ili kufanikisha mambo yao. Hii ni kutokana na mfumo kubadilika kila mara uongozi mpya unavyoingia. Rushwa ni adui wa haki ila inatendeka kwasababu ya mifumo mibovu ya kiutendaji kwasababu kila mmoja anataka apate kwa namna anavyoweza yeye. Mamlaka ya Mapato (TRA) imekuwa ikikinzana na wafanyabiashara kwasababu hakuna suluhisho la kudumu. Tulishuhudia 2023 Wafanyabiashara wa Kariakoo wakigoma sababu ni ongezeko la kodi na ushuru bandarini.

(iii) Kudumaza uchumi; Uchumi wa nchi haukui kwasababu ya sera ya uchumi wa amri. Watendaji wa serikali wakiwa hawana Mawazo huru ni ngumu kuendelea. Kukosekana kwa ushindani kunachewesha maendeleo. Wasomi wamekuwa wengi hivyo ni muda sahihi wa Serikali kuruhusu sera ya uchumi wa soko huru.

(iv) Kukosekana na demokrasia na haki za kiraia; Kwa miaka mingi tumeshuhudia Demokrasia na Haki za Kiraia zikivunjwa kwa namna fulani lakini hizo ni zama zilizopita, wakati tulionao sio wa kukumbuka tulikotoka lakini ni muda sahihi wa kurekebisha tulipokosea na kuanza upya kulingana na wakati tulio nao. Tumeshuhudia Kesi ya kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi ya jinai Namba 456 ya mwaka 2016 iliyokuwa inamkabili Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Bwana Maxence Melo na Bwana Micke William Pamoja na kesi nyingine. Binafsi siyo Mwanasheria ila najaribu kuelezea kesi kama hizi zilivyokuwa zinatokea dhidi ya Waandishi Wa Habari na Serikali ya Tanzania. Ripoti ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ya August 2017 ilisema Jamii Media ina watumiaji milioni 2.4 ambao wako huru kujielezea, sasa tujiulize hiyo ni miaka sita iliyopita, Je hivi sasa watumiaji wapo kiasi gani?

Wengi ni mashuhuda wa jinsi Shirika la Utafiti la TWAWEZA lilivyokuwa likipitia kipindi kigumu na Serikali ya Tanzania, Taarifa ya kutoka DW ililipoti habari hii mnamo 3/08/2018 na katika taarifa yake ilisema siku ya August 1, Mkurugenzi wake Bwana Aidan Eyakuze alizuiliwa kusafiri kwakutumia pasi ya dharura iliyotolewa kwa utaratibu ulipo ili aweze kushiriki mikutano ya kikazi kwenye ofisi za TWAWEZA kwenye miji ya Nairobi, Kenya na Kampala,Uganda, sikuweza kujua sababu za Serikali kupitia Msemaji wake wa Idara ya Uhamiaji Bwana Ali Mtanda lakini lazima tujipange upya katika miaka ijayo.

Kwahiyo tunaona kwamba watu wote wana haki ya kupata habari endapo watahitaji na Vyombo vya Habari viwe huru kufanya kazi yake ili watu husika waweze kupata habari mbali mbali zinazowahusu yaani watu wapate habari kadri ya mahitaji yao na Waandishi wa Habari waruhusiwe kufanya kazi yao na kuripoti matukio yote nchini pasipo kuzuiwa au kutokea kwa mauaji ya Waandishi wa Habari kama zamani, watu wapate habari kwa kadri ya matukio yanayoendelea bila pingamizi kwamaana kila taarifa ya habari ina mlengwa kwahiyo hakuna budi Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari kuwa huru ili kuwafikia walengwa. Pia Haki za Kiraia zilindwe pamoja na Utawala wa Kidemokrasia.

MAXENCE MELO.jpg


Picha kutoka GLOBAL PUBLISHERS ikimwonesha Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums Bwana Maxence Melo na wenzake wakijadiliana jambo.

AIDAN EYAKUZE.jpg


Picha kutoka todayspro.blogspot.com ikimwonesha Mkurugenzi wa Shirika la TWAWEZA Ndugu Aidan Eyakuze akizungumza katika kongamano.

(v) Kutotimiza wajibu miongoni mwa viongozi na raia; Kwakua Serikali inamiliki au kushikiria karibu kila nyanja ya uchumi. Wengi wanakuwa hawajishughulishi na hivyo kuendelea kutoa lawama. Wote tujiulize tumeifanyia nini Tanzania kabla ya kulalamika. Serikali isitengeneze mazingira ya kulaumiwa na kila mtu atimize wajibu wake.

Ninashauri;
(i) Serikali iruhusu Wawekezaji wengi na mazingira wezeshi kwa Vijana; Teknolojia mpya zitumike kufufua na kuongeza uzalishaji wa ndani, Serikali isiingilie uzalishaji wala masoko yenyewe bali iweke mazingira wezeshi na kudai kodi tu. Miradi endelevu kama SGR, bwawa la Nyerere isibezwe. Tanzania isiwe sehemu tu ya kuagiza bidhaa kutoka China na nchi nyingine ila na sisi tuweze kutengeneza vya hapa hapa nchini na au kupitia wawekezaji na kuuza nje.

DSC_0027.JPG

Picha hii imepigwa na mimi ikionesha ujenzi wa Kituo cha Masoko,Ubungo

(ii) Kuweka mifumo imara ya kulipa kodi; Taarifa ziwe za wazi na kila mtu azijue anapotaka kuwekeza isiwe kutumia makadirio kitu ambacho kinapelekea rushwa. Kuruhusu mifumo mingine ya kutuma na kupokea fedha kama "wire transfer"na "paypal", Bank Kuu iwekeze katika teknolojia mpya za kifedha. Kila tasnia ihusishe taaluma na itambulike na mamlaka husika.

(iii)Kuruhusu masoko huru ya bidhaa na huduma; Kila biashara ijisimamie yenyewe na wahusika wake kutokea uzalishaji mpaka masoko. kwasababu kila kitu kitakuwa na thamani kadri ya mahitaji ya watu (law of demand and supply).

HITIMISHO;
Dunia inasonga mbele na kila uwekezaji unahitaji faida, zama zimebadilika kila mtu itabidi ajitambue ana uwezo gani. Tanzania imekuwa nchi ya kukuza chapa za kampuni za nje kwa muda mrefu, wenye chapa zao wanajipangia bei zao, Tusiwe watu wa kupokea tu na sisi tutengeneze chapa zetu ili pato letu likue. Vyombo vya Habari vitumike kutoa taarifa mbali mbali bila kikwazo.

Ninawapongeza sana JamiiForums na Shirika la TWAWEZA kwa kazi zao za kuibua kero mbali mbali na kusaidia kupaza sauti na kuongeza uwajibikaji wa Serikali na watu wake nchini, Asanteni.
 
Back
Top Bottom