Tuachane Kabisa na tabia hizi za kidikteta

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,496
19,332
Imekuwa ni kawaida kusikia kuwa baadhi ya mamlaka nchini zimekuwa zikizuia biashara halali za vyombo mbalimbali vya habri vinavyobeba habari zinazogusa maslahi ya mamlaka hizo. Mwezi October kabla ya uchaguzi mkuu, mtoto wa Rais Kikwete aliripotiwa kuizuia ITV isirudie matangazo yake yenye mahojiano na Dr. Slaa kuelekea uchaguzi mkuu bila kuwepo sababu yoyote ya kisheria.

Wiki mbili zilizopita iliripotiwa kuwa Lowasa alizuia magazeti ya Raia Mwema yasichapishwe kwa vile yalikuwa na habari iliyohusu mtoto wake; alifanya hivyo bila kuwa na sababu yoyote ya kisheria. Wiki hii, inasemekana mtoto wa Rais tena amezuia usambazi wa magazeti ya Raia Mwema kwa vile yalikuwa na habari inayohusu mgogoro wa UVCCM ambao yeye binafasi anahusika; hilo pia lilifanyika kinyume cha sheria.


Hii ni tabia ya kidikteta ambayo inabidi ikome mara moja. Ni tawala za kidikiteta tu ndizo zisizovumilia kuona habari zinazotofautiana na matakwa yao. Kwa vile Tanzania ina vyombo huru vya habari, ni lazima watawala na familia zao wajifunze kutokuingilia vyombo vya habari. Iwapo wanadhani vyombo hivyo vimepotosha ukweli, mahakama ziko wazi kusikiliza malalamiko yao.

Kuzuia gazeti lisiuzwe ni kosa kubwa sana kwa vile siyo tu kujenga tabia ya kuzuia wananchi wasipate habari mbalimbali, bali pia ni kuingilia biashara halali za gazeti husika ambalo linalipa kodi zote za serikali pamoja na gharama nyingine za uendeshaji kama vile kodi za pango la ofisi, gharama za umeme, simu pamoja na kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.
 
Back
Top Bottom