Tu Matajiri wa kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru kwa jinsi hii????

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Ni takriban miezi kadhaa sasa wizara na taasisi za serikali zimekuwa zikiteketeza mamilioni ya fedha kwa kile kinachoitwa sherehe za miaka hamsini ya uhuru. Hii ni pamoja na kuandaa mabanda ya maonyesho, kupamba kwa gharama, kutengeneza t-shirts na suti, kukodi vikundi vya sanaa kuburudisha kwa siku tatu, kurusha matangazo kwenye vyombo vya habari, kulipana posho nono, kuandaa tafrija kubwa mwisho wa maonyesho nk. Kila wizara imeandaa kwa siku tatu, kila mkoa una siku tatu zake, kila wilaya ina siku tatu na taasisi zote hizi hutumia fedha zetu katika vikao vya maandalizi na katika siku zenyewe. Nafikiria mpaka ifikapo terehe 9 Desemba ni kiasi gani cha fedha kitakuwa kimetumika. Bahati mbaya iliyoje ya kuwa sehemu kubwa ya watanzania hawajui kinachoendelea na maonyesho haya hayana tija kwao na si watu wengi wanokwenda kuangalia. Katika maonyesho yote haya sijaona kitu chochote ambacho Mtanzania anaweza kujivunia kuwa ni miaka 50 ya uhuru. Nilichoona ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi. Hivi fedha yote hii ingetumika kutatua sehemu ya shida hizi za wananchi:
1. Wanachuo wote pengine wangepata mikopo
2. Vijiji kadhaa vingepata vituo vya afya
3. Tungechimba visima kadhaa vya maji na kupunguza tatizo la maji
4. Wastaafu wa EA wangefuta laana yao kwa kiranja mkuu kwa dhuluma aliyowafanyia
5. Ongeza……..
Hivi ni nani ametulaani sisi watanganyika??????????
 
Labda Hata Hiyo Hela Ingewalipa Fidia Wanaoamishwa Kwa Nyumba Zao...
 
Back
Top Bottom