TTCL waja na TTCL pesa, nawapongeza kwa hatua hii

Katika kampuni ambazo haziko siriaz na biashara hii nayo imo yani inafanya biashara kizamani mno, wenzao wanasambaza maflilensa mitaani wenyewe wamejifungia tu ofisini
 
Hii kampuni ikijiweka sawa itapata wateja saana, maana hakuna watu wanaopenda vyao kama waTZ.

Waendelee kujiweka sawa, atleast wawe na same service & quality na kampuni pinzani. then waone watakavovuna wateja
 
Kama ni kweli kuna TTCL pesa naanza kuiona maxcom ikipotea maana hizo kazi zoote zitachukuliwa na hawa jamaa.
 
Safi sana, mimi na wengi kwenye familia yetu bado ni wateja wazuri wa kuwa na landline. Huduma yao nzuri hadi leo na tumekuwq nao kwa miaka mingiiiiiiiiiii tangu enzi hizoooo.

Mitandao ikileta tabu mtu hupati wasiwasi kabisa 24/7.
 
Dah, afadhsli. Naamini TTCL watatitoza gharama nafuu zaidi za kutuma na kupokea pesa kuliko hizi kampuni za simu za mabwanyeye kutoka ughaibuni.

Vv
 
Bila kustaafisha wafanyakazi wote na kuanza na menejimenti mpya na wafanyakazi wapya, TTCL haiwezi kufika popote.

Hawawezi kuhimili ushindani wa kisasa kutoka katika makampuni binafsi ambayo yamewekeza sana katika menejimenti na rasilimali watu, kitu ambacho TTCL hawezi kumudu kutokana na muundo wao.
 
Elimu ndogo maana yake nini? Tz hatuna wasomi?
Hao waliopo Tigo voda zsin wametoka wapi?
Hiyo ndio furssa ya ajira.

Elimu ndogo maanayake ni kuwa na uwelewa mdogo katika tasnia husika. Mkuu ipogolo Tanzania wasomi wapo kwa kiasi chake.Tatizo hawapewi iyo fursa kutokana na walioshikilia nafasi hizo kwa sasa.

Pengine hujawahi kujua kwamba wafanyakazi wengi walioajiriwa na shirika la TTCL miaka ya 90 walitokea shirika la posta na simu la afrika mashariki. wafanyakazi hawa walichukuliwa moja kwa moja na TTCL kwa kigezo cha uzoefu wa hapo awali japo wengi wao walikuwa na elimu ya form four, la saba na certificate.

Jambo hili limefanya shirika kuwa na wafanyakazi mzigo wengi sana, ndiyo sababu nimesema watakapostaafu wote shirika likiajiri wasomi hapo litafufuka rasmi. N:B, TTCL wasomi wapo ila sio kwa kiwango cha kuridhisha.
 
Wamekumbuka shuka alfajiri! Wamezidiwa coverage na Halotel, kampuni ya serikali lakini imelala sana labda JPM akiisukuma ingawa kuna watu baada ya miaka 10 wanaweza kuiua, Dawa yake ijisajiri kwenye DSE ili watu waimiliki kwa walau 35%
Negative minds zimewaharibu sana
 
Wakiwa na huduma nzuri itabidi ninunue line yao kwa ajili ya miamala tu. Tigo WEZI jamani.
 

Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom