Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,604
- 3,163
Naleta mbele yenu kisa hiki ambacho kimenipata mimi mwenyewe. Ukipita mitaa mingi ya Dar Es Salaam kuna mabango kila mahali yanayoonyesha kwamba TTCL wanatoa huduma ya internet. Pamoja na kwamba kuna makampuni mengi sasa hivi yanatoa huduma hii, mimi nilishawishika kuwajaribu TTCL kwa maana nzima ya kulipiga tafu shirika letu la umma pamoja na kuonywa na rafiki yangu mmoja kwamba TTCL ni wasumbufu na kwamba itanichukua muda mrefu kupata huduma hiyo. Lakini kinachoendelea kwa sasa huwezi kuamini kwamba ndio watu wale wale walitumia mamilioni ya shillingi kuweka matangazo kwamba wanatoa huduma hii. Tarehe 21 December 2009 nilikwenda pale TTCL Ubungo plaza na kuulizia uwezekano wa kuunganishiwa internet nyumbani kwangu. Nilipewa fomu nikajaza na kuonyesha nitachukua package ipi kati ya zilizokuwepo baada ya kupewa maelezo na kushauriwa nitumie landline ili niweze kupata huduma nzuri zaidi. Niliwafahamisha kuwa ninayo landline nyumbani kwangu na hivyo nikaambiwa atatumwa fundi kuja kuangalia eneo. Ni kweli fundi alikuja na baadae walinitaka nikalipie. Nililipia connection fee ya Tshs. 25,000 na baada ya hapo ikawa kimya. Baada ya kuwafuatilia nikataarifiwa kuwa siwezi kupewa huduma hiyo kwa sasa kwa kuwa wameishiwa modem. Nikaulizia uwezekano wa kununua modem yangu mwenyewe wakasema sawa ninunue halafu niwataarifu waje kufunga. Pamoja na kulipia hiyo gharama ya internet ya mwezi mmoja tarehe 21 January 2010, mpaka leo fundi hajaja kuniunganishia hiyo huduma. Ukienda pale ofisini kwao wanakwambia fundi alikuja hakukuta mtu nyumbani, ukimpigia fundi simu kuuliza anadai alikuwa busy sana bado hajaja!!! (Contradiction)
Swali langu ni je hali hii imeishamkuta mtu mwingine au imetokea kwa bahati mbaya kwangu tu? Je hawa jama zetu kwa mtindo huu ni kweli wamejiandaa kufanya biashara kwa ushindani? Je wakubwa huko makao makuu wanajua madudu yanayofanywa na watendaji wao hawa?
Natabiri kufa na kuzikwa kwa TTCL muda si mrefu endapo hali hii haikutokea kwa bahati mbaya tu.
Tiba
Swali langu ni je hali hii imeishamkuta mtu mwingine au imetokea kwa bahati mbaya kwangu tu? Je hawa jama zetu kwa mtindo huu ni kweli wamejiandaa kufanya biashara kwa ushindani? Je wakubwa huko makao makuu wanajua madudu yanayofanywa na watendaji wao hawa?
Natabiri kufa na kuzikwa kwa TTCL muda si mrefu endapo hali hii haikutokea kwa bahati mbaya tu.
Tiba